Umetafuta Fundi wa gari yako? Uliza chochote kuhusu gari lako

Huyu mnaemuuliza maswali atakuwa ni mmasai mbona kala nduki.
Hivi level ya oil ikipungua kidogo sana kuna shida?
Yeyote anaejua tuachane na huyo baba yoyoo
Hakuna shida sana kwa level ya oil kupungua kidogo, ukiangalia kwenye ile deep stick ya oil utaona kuna vi mistaking vya vipimo vya oil. Kuna mstari wa juu kabisa ambao unaonyesha oil ikiwa imejaa nomal, kuna mstari mwingine wa kati, kisha kuna mstari mwingine wa Mwisho, huo ndo denger zone, oil haitakiwi ishuke zaidi ya hapo utakaanga Mashine, na pia yaa ya oil lazima itawaka.
Angalizo ukiona oil inapungua Mara kwa Mara jaribu kufuatilia kuna sehemu lazima inavujisha oil, check oil seals zote...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Noah 3s engine. Nikifika speed 100 pale vingunguti kuelekea tazara sterling inashake kama tetemeko la ilma. Tatizo nini mkuu. ?

Naomba pia kujuzwa mambo ya tierod hand na ball joint

Pia mambo ya wheel balance na wheel alignment.


Afu noah yangu sikuhizi nikiweka kiroba cha pumba ina gonga kwa nyuma utafikiri nimebeba gearbox ya scania.

Afu naskia kuna eneo wanasafisha engine kitaalam yaani wana safisha hadi betri na mifumo mingine. Sijajua ni wapi kwa dar es Salaam.


Afu pale ulivyojibu kuhusu overdrive sina uhakika kama ukiweka overdrive inapunguza makelele.
Mi naitumia sana Safari za masafa nikiendesha nikaona gari inayumba sana naweka ile pale......
Kelele zinazidi lakini gari inakuwa nzito inatulia barabarani ndo kazi yake kubwa.


Naomba majibu yaukweli hasa lile la sterling kushake.

Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh hapo kwenye moshi mweusi umechapia ila sio mbaya umekosea mahala padgo tu

Moshi mweusi husababishwa na hewa kuwa chache

Moshi wa bluu ndio hiyo oil inakua imejipenyeza kutoka kwenye piston and combustion ring

Moshi mweupe ni dalili ya maji au unyevu unyevu kuingia kwenye combustion chamber

Nawasilisha
 
Mh hapo kwenye moshi mweusi umechapia ila sio mbaya umekosea mahala padgo tu

Moshi mweusi husababishwa na hewa kuwa chache
.
Ndiyo maana nikasema mwanzoni kabisa kuwa sababu ni kuwa na "incomplete combustion", maana yake hewa chache.

CH4 + O2 = C + 2H2O + Heat

Ila nimerekebisha kidogo kurahisisha maelezo. Pamoja!
 
Kawaida gari inatakiwa itumie umbali gani kwa lita moja ya mafuta
 
Gari inachelewa au kugoma kuingia via namba mbili,ikikubali tu zile mbili zingine zinaingia bila shida,ni automatic gear box.
 
Gari inachelewa au kugoma kuingia via namba mbili,ikikubali tu zile mbili zingine zinaingia bila shida,ni automatic gear box.
Gari aina gani? Ukishindwa kutoa maelezo vizuri utashindwa kusaidia.

Ww unasema utafikiri wote tunafaham gari yako ni aina gani au unafikiri magari yote automatic ufanyaji kazi wa gear box ni sawa
 
MSAADA JAMANI TOYOTA IST SPEED MITA INAGANDA GARI IKISHA TEMBEA UMBALI MREFU YANI UNAKUTA NIKIFIKA KWENYE VIBAO VYA SPEED 50 NIKIPUNGUZA UNAKUTA BADO INA SOMA SPEED 80 ILA GARI IKISHA POA INARUD KAWAIDA NIKITEMBEA TENA UMBALI MREFU TATIZ ILO ILO MATRAFIC WANAKULA SANA ELA YANGU Msaada wa haraka
 
Natafuta switch ya Taa (demmer switch Toyota vitz DBA - KSP90)
 
Gari aina gani? Ukishindwa kutoa maelezo vizuri utashindwa kusaidia.

Ww unasema utafikiri wote tunafaham gari yako ni aina gani au unafikiri magari yote automatic ufanyaji kazi wa gear box ni sawa
Mkuu gari ni Nissan Wingroad ya 2002,kuna wakati kuhama gear number moja kwenda mbili inasumbua Ila ikishaingia mbili hizo zingine hazina shida, ni automatic transmission
 
Kwa nini ushushe vioo? Mi gari yangu toka nmenunua niliwah jaribu tu kuona kama vioo vinashuka toka hapo sijawah shusha.washa AC emdesha gari .

Gari inakosa nguvu, nikiwasha ikawaka nikitaka kushusha vioo inazima, nimebadil plug bt bado inasumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Jamaa mhuni sana. Kafungua uzi halafu anakaa anachungulia tu posts za watu anakaa pemben. Anafurahia kuona watu wakielezea matatizo ya gari zao.... Ha ha ha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…