Chamoto
Platinum Member
- Dec 7, 2007
- 9,883
- 22,310
.Hivi ikitokea gari ikaongeza fuel consumption huwa shida ni nini? Before 14-15km/hr now around 12 km/hr.. Toyota belta 2006 model
Sent using Jamii Forums mobile app
Sababu ya kwanza inaweza kuwa ni tatizo la emission.
Inaweza kua 'fuel filter' imeziba, kama haujabadilisha fanya hivyo. Pia 'throttle body' inaweza kuwa chafu na inatakiwa kusafishwa. Air cleaner au MAF (mass air flow sensor) pia inaweza kua chafu. Kuna 'spray can' ya kuisafisha MAF au unaweza tumia 'rubbin alcohol'. Ukaiweka (rubbing alcohol) kwenye spray bottle halafu unapulizia kwenye MAF kwa ndani kuisafisha, rubbing alcohol ita dissolve dust particles zote na kuzi-evaporate.
Pia inaweza kuwa kuna tatizo la 'vacuum leaks', ile mipira inayozunguka kwenye engine inasaidia kuiambia 'computer ya gari' kiasi cha air/fuel mixture inayotakiwa. kama imetoboka/imakatika mahali basi 'computer ya gari' inaweza fikiri engine inahitaji mafuta mengi kuliko kawaida.
Sababu ya pili inaweza kuwa ni 'compression'.
Hili ni tatizo la ndani ya engine. kunatakiwa kuwe kumezibwa vizuri. kama kuna sehemu ina 'leaks' basi nguvu ya engine itapungua kiasi fulani na hii itasababisha utumie mafuta mengi kuliko kawaida.
Sababu ya tatu inaweza kutokana na auto transmission (kama unatumia) kuwa mbovu ambapo gari haibadili gear inavyotakiwa kwa kuishia kwenye low gears. Hii hufanya engine itumie mzunguko mkubwa (high revolutions) kuliko kawaida ambapo husababisha mafuta mengi kuchomwa.
Vile vile Kuna baadhi ya magari yanakuwa na 'sports mode' ambapo ukibonyeza ki-button inazuia 'tranny' ku shift kwenda 'overdrive' na hivyo kufanya iishie kwenye low gears (zinakula mafuta). Jaribu kuangalia 'owners manual' ya gari lako kama ina 'sports mode option'.