Umetimiza ndoto zako?

Umetimiza ndoto zako?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Nakumbuka nilipokuwa form 2 nilianza kupenda sana majibizano na wenzangu kuhusu siasa, yaani ilitokea napenda sana kukosoa serikali kwa kuwa ndiyo kitu simple sana kuliko kusifia sababu ni kwamba toka tunavyopata uhuru fikra zetu zimejengwa kuwa Wazungu(watawala) ni wanyonyaji na wabaya sana.

Kwangu ilikuwa nyepesi kuorodhesha points kama vile
  • Cheap labour
  • Land allienation
  • Forced labour
  • Area for market n.k
Kusema kweli nilishawishika kuijua na kuitambua siasa kwa undani, basi nilijitahidi kusoma post nyingi za Jamii Forums, pia magazeti pamoja habari nyingi zinazochapishwa facebook za wapinzani kwa kuipenda siasa.

Matarajio yangu siku moja nitakuja kuwa Mbunge au Waziri ila kwa bahati mbaya ndoto zangu hazijatimia sababu sipo interested na makundi, yaani sipendi muingiliano na watu pia napenda sana kujitenga ila naumia sana ndoto zangu hazijakamilika.

Ushauri wako please, pia upande wako vipi, umetimiza ndoto zako?
 
Nakumbuka nilipokuwa form 2 nilianza kupenda sana majibizano na wenZangu kuhusu siasa yaani ilitokea napenda sana kukosoa serikali kwa kuwa ndiyo kitu simple sana kuliko kusifia sababu ni kwamba toka tunavyopata uhuru fikra zetu

Ushauri wako please pia upande wako vipi umetimiza ndoto zako?
Una degree?
 
Kuibgia kwenye siasa Tanzania na ukang'aa ni wepesi sana.

Wapo wazee wa vibahasha akina Pascal Mayalla, watayarishie vibahasha vyao iwatakupamba na kukupaisha tu.

Vibahasha tu, hakuna zaidi.
Ndugu pascal mayalla(Bw njaa) hana populality kihivyo zaidi nitapoteza muda.
 
Back
Top Bottom