Umewahi ishi na mtu ambaye akilewa ni Kiingereza tu?

Umewahi ishi na mtu ambaye akilewa ni Kiingereza tu?

Ila wanywa pombe some times ni raha kuwatizama wakati wamelewa. Anaongea english nzuri hadi raha.

Hivi pombe na kiingereza ni mapacha?

Rafiki yangu shoga yangu wa ukweli (RIP) alikuwa akilewa watu wote walokaa pembeni ya meza yetu lazima wageuke kusikia nani anaongea. Mimi situmii pombe. Hata wahudumu anawaongelesha kiingereza 🤣🤣
Lakini akiwa hajatumia pombe hakuna cha kiingereza wala nini.
Siku moja tukiwa chuo zile group presentation nilikuwa nae group moja. Mara tukasimanishwa kama 7 hivi , wanaume wakasema mdada atuwakilishe yesuuuuuu nani wa kuongea mbele ya darasa zima?

Tukaanza kubishana tunaongea pole pole
Shoga yangu akasema my wiiii present wewe mimi siwezagi kuongea mbele za watu. Nikamkubusha akiwa amelewa mbona anawakomesha hadi wahudumu? Akasema my wii acha ujinga hapo si ninakuwa nime bust? Sasa hapa macho meupe hivi nitaanzaje 😜. Tulibishana mwisho aka present wa kiume.

Situmii pombe ila na enjoy mtu akilewa nimtizame machoni na wanavyoimba nyimbo ambazo hazina ushirikiano😆
 
I see myself 😅, nikifika chupa ya 5+ lugha inanyooka kama nimetoka birmingham city leo.
 
Pombe bhn...Me kuna mmoja namjua akilewa anaanza kutaja marehemu wote na kilio JUU
 
Back
Top Bottom