Naanza na mimi!!!
Wakati niko darasa la tatu nilimuomba jirani yetu hela nikatumie shuleni akaniambia njoo kesho kabla hujaenda shule... Nyumbani tulishakatazwa kuombaomba hela kwa watu [emoji3] [emoji3] Sasa mimi kesho yake nikaaga nyumbani mapema kua naenda shule, nikapitia kwa jirani na kumsubiri anipe hela... Nimekaa kama nusu saa, ile nageuza shingo namuona mama yulee anapita... Akanichunia na kupita kimya kimya.
Nilivyorudi jioni... Nilidakwa na fimbo kuanzia getini... Mama yule alinichaaapa fimbo zilivyokatika akachukua ndala... mpaka nikajikojolea ...
Yaani milele sintasahau kike kipigo.