Umewahi kuchapwa/kupigwa na mzazi/mlezi?

Umewahi kuchapwa/kupigwa na mzazi/mlezi?

Hivi wazazi wa kipindi hiki wanapiga watoto kama zamani? Mimi nimepigwa ila kuna rafiki wakati tupo shule ya msingi alipigwa na mzee wake sijawahi kuona kipigo kile ingekuwa leo yule mzee jela ingemuhusu kabisa jamaa aliletwa shule hawezi kutembea amekatwa sikio, alama za visu mgongoni na bado akampiga mbele ya mwalimu mkuu walimu wakamuombea msamaha jamaa angekufa. Wakati mwingine wazazi wetu walitumia vibaya nguvu zao kutuabuse. Mada imenigusa mno
Dah umenikumbusha far,kuna mzee mmoja alikua ni anatembeza kipondo heavy,namaanisha kipondo heavy kwelikweli,akimchapa mwanae,mtoto lazima ajinyee au ajikojolee.Yani mke wake akisikia mtoto anakula kichapo anachemsha maji ya moto kabisa kwa ajili ya kumkanda kanda mtoto,

Yule maza alikua analia sanah mtoto wake akiwa anachezea kichapo,mana vichapo vya huyo mzeee daah.Mpaka nikawa nawaza au sio watoto wake mana sio kwa kipondo kile
 
Back
Top Bottom