Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] nataka kuzimiaMi baba aliwah nipiga mpaka kuhisi kuzimia ,hadi nikawa namuambia baba nataka kuzimia ,,tokea hapo hakunipiga tena ,nimekumbuka nimejisikia vibaya lo
Nimekumbuka hii "Nyani Ngabu, ulinemelwa ng'wanone"Sikuwahi kabisa kupigwa na mzazi.
R.I.P Mzee!Mimi nilikuwa Mtundu sana. Hii ilisababisha mpaka nikapelekwa shule ya boarding nikiwa na miaka minne pekee.
Siku moja ambayo mama na baba walinichangia ni siku ambapo nilienda kumtega mzee kipofu na kumwangusha. Nilitengeneza kamba alafu nikaitegesha njiani, mzee kipofu alipokuja anatembea na mkongojo wake nikainyanyua na kumuangusha. Nikabaki hapo pembeni nacheka kwa nguvu.
Asee, hiyo kipigo nilichopata sitakaa nisahau asee. Nilichapwa fimbo za kutosha maana nilishakuwa sugu kwenye mkanda.
Mungu anisamehe kwa niliyomtendea yule Mzee. Naamini hata huyo mzee kanisamehe pia, nilikwenda jumuomba msamaha kabla hajafariki, RIP.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] pole mkuunikiwa Std 3,nilimwandikiaga babe barua ya jinsi gani ananifanya nashindwa kusoma sasa badae nikawa sikuipeleka ile barua kwa shost nikaisahau kwenye mfuko wa kaptula ya shule sasa wakati bi mkubwa anafua akaiona ile barue,AISEEE!!! hiyo kichapo nilitembezewa sitakuja kusahau,ingekua ni leo nahisi wimbo wa Moyo sukuma damu si vingine ungekuwa my favority song,maana nilishushiwa kipigo cha maana
Duu!!!Wee yan hapo ndo penyewe sasa mimi nilikuwa nahesabiwa makosa yakifika matatu ndugu hicho kipondo lazima uombe poo..Kuna wamama wanajua kupiga jaman kwanza unapewa msosi ule ushibe halaf huo mziki wake mpaka maji ya baridi unamwagiwa baada ya kipigo
[emoji23] [emoji23] [emoji23] pole mkuu
Tuliibaga wengi kumbe wakati wa kujipikilisha [emoji3][emoji3]Kwenye hii michezo ya kujipikilisha kwenye njeka nilikua napenda sana...
Siku hiyo nimetegea mama kaenda kazini nikaenda kuiba mafuta na chumvi ndani na nilishaonywa hiyo tabia nikawa nafanya kisirisiri
Siku hiyo natoka shule mama kanipokea na kichapo juu juu,alinichapa sana tokea siku hiyo nikaacha udokozi wa vitu ndani tunapocheza...