Umewahi kufanya kazi gani yenye hatari kubwa ambayo kidogo ikutoe uhai?

Umewahi kufanya kazi gani yenye hatari kubwa ambayo kidogo ikutoe uhai?

Pole sana mkuu, ila hayo ni mambo ya kawaida kwa watafutaji,

Nimechimba sana madini huko Chunya...na niliyoyaona na yaliyonipata nikiwa huko, yalinipa Trauma....

Kuna wakati huwa siamini kuwa nipo hai...maana kuna muda nakurupuka hata usingizini, na kwa-kiasi kikubwa sana nimepoteza hata Uwezo wa Kulala.,.

Naangazia kuja kuandika Uzi hapa jukwaani, ila kwasasa nipo bize kiasi...

Duh pole sana mkuu maisha ni safari.
 
Mimi si mwandishi mzuri ila nitajaribu kuandika niwezavyo.

Mwaka 2018 niko kisiwani, nilikuwa nikinunua samaki wabichi(sato) napeleka mwanza, siku hiyo mida ya jioni napigiwa simu na wavuvi wa kisiwa cha jirani kuna mzigo mkubwa tu nikafuate.. nikaomba mtumbwi wa kasia kwa jamaa yangu mmoja nikachukua na mshkaji mmoja ili anisaidie kupiga kasia tuelekee maeneo hayo nikachukue hizo samaki.

Tumetembea kama dk30 wakati sasa tumeshaanza kukiona hiko kisiwa cha jirani aiseee lilikuja wimbi moja lilipiga ubavu wa ule mtumbwi tukazama ndani ya maji asee ishukuruwe tu wakati ule ulikuwa ni muda wale wavuvi wa sangara ndio wanaingia ziwani(doro) walitupita tukiwa tunatapatapa na ndio tukaokolewa namna hiyo..

Hii kitu imenifanya kuogopa maji sana mana siku hiyo ndio ilikuwa niagieni kabisa
 
Pole Sana asiseee.


Mm kidgo nife hapa African sijuwagi yule nilite butuwa na lory lilofeli breki Yuko api
 
Pande za mwanza nyegezi corner mtaa wa swila, kuna siku tuko kwa mtanga ubalozini aisee walitokea mapoti from nowhere watu tulitawanyika kama upepo kuna milima na mawe makubwa ndo siku nilipanda jiwe bila kupenda dadeki jiwe la mwisho lilikua kubwa almanusura linishinde mana mixer pumzi kukata na naona hapa nikteleza naumia vbaya au kifo nyuma naona mapoti na nyungu wanaongezeka, real fvckn movie!
ndio maana unajiita man rody

Mwisho wa siku uliwachenga ama walikukamata?
 
Sitosahau siku nilipotaka kufa pale kiwandani​

Ilikua mapema tar. 1/June 2022 nilipitia kipindi kigumu sana baada ya kuyumba kiuchumi na degree yangu mkononi ikanilazimu kujizima data na kutafuta kazi yoyote iwe rasmi au isiwe rasmi. Nikazama zangu JF ndipo nikapata muongozo wa kwenda kiwanda cha unga kwa kurubuniwa kwamba kwa siku malipo inafika hadi buku 8 nikajipa moyo.

Basi nikafata tafatibu zote siku ya pili nikaenda na barua ya mtendaji then nikaambiwa siku ya pili usiku nikaanze kazi. Basi bwana nikazama zangu pale mida ya saa 1 jioni nikawakuta wenzangu wapo tayari wanasubiri kuanza kazi.

Wakagawa msosi pale ndani kila mtu sahani ya wali(upo kama makande) na maharage na ndizi mbivu. Kwa kua ni siku ya kwanza nikawa na uoga uoga wa kula ule msosi na niliogopa kuja kukatwa kwenye malipo.

Jamaa wakawa wananishangaa huyu msela vipi huu msosi ni lazima kuchukua haijalishi unataka au hutaki. Basi kuna jamaa akasema chukua nipe mimi nitakula, wakawa wanagombania nipe mimi nipe mimi. Basi nikachukua ule msosi nikampa jamaa mmoja akala na wa kwake.

Kimbembe kilianza baada ya masaa mawili viroba vilipoanza kushuka toka kwenye vinu vinashuka kama mvua na vinu vipo vya kutosha mule ndani. Ili kusubiria viwe vingi ndio kazi ianze wale jamaa wakasema tuchezeni boli humu ndani (mpira wa makaratasi).

Basi tukagawana huku na huku tukaanza kucheza mpira.Katika harakati za kuucheza ule mpira nikajibamiza vibaya sana kwenye kinu kipo kama upinde afu kule mbele kama wembe kwa makali yake.

Ghafla bin vuu nikajikuta nipo chini nimezungukwa na watu kibao damu zinavuja kama kuku katoka kuchinjwa. Aisee nilijua leo ndio siku yangu siwezi kutoboa maana nilipasuka katikati ya kichwa. Wakaniinua pale sina hata nguvu wakasema nikapumzike pale kazi inataka kuanza. Nilishindwa coz damu zilikua zinavuja sana kuna jamaa akanielekezaa bafu akasema nikaoge ili niwe sawa.

Nilijivuta nikaenda kuoga kule bafuni maji yote yalijaa damu tu yani ili siku ilikua ndio bye bye sema Mungu hakupanga tu. Nikarudi kule ndani jamaa ndio wanagawana watu kwa makundi waanze kazi. Cha ajabu na mimi nikaitwa nikapangiwa kundi nibebe viroba.

Nikawaeleza siko sawa damu zinavuja sana lakini hakuna aliyeelewa. Wakasema humu ndani ni lazima kila mtu afanye kazi. Kazi ikaanza nikaambiwa na mm nibebe kichwani zile kilo 25 kwa 50 yena viwili trip moja.

Ilikua ngumu sana kubeba lakini sikua na jinsi nikajaribu tripu moja nakashindwa kichwa kilikua kinauma sana. Wakanibadilisha section wakasema niwe nawapakia watu kichwani wenyewe wanaita kijiko, yani unabeba viroba viwili pale chini na kumpa mtu kichwani.

Nimefanya mara moja tu kuna jamaa akanigusa pale kichwani na kiroba basi damu zikaanza upya kutoka nikaamua kuacha nikasema liwalo na liwe cha kufia nini. Basi nikatoka pale nikaenda nje kukaa toka ile saa 4 mpaka saa 12 asubuhi jamaa wanabeba tu vile viroba.

Walikua kama 30 hivi lakini viroba walivyobeba ni zaidi ya 6,000 yani kila mmoja kama mia 2 hivi. Asubuhi ya saa 1 tukaitwa wote kwenye mgao wa pesa. Kaja kiongozi wao akasema leo kazi hamna hivyo kila mtu atapata elfu 2,aisee nilichoka mwili na akili yani kazi yote ile mtu alipwe elfu 2.

Kuna watu walikua wanapinga mimi kupewa ile elfu 2 kisa sijafanya kazi. Sema jamaa akanipa ile buku 2 akasema ukatibiwe. Nimetoka pale naona kama ndoto nikarudi zangu geto ile pesa nikafanya nauli sikubakiwa hata na senti.

Nimefika home kichwa chote kimeloa damu na nimepasuka vibaya sana. Sikua na pesa hivyo nikachukua chumvi na beseni nikaanza kujisafisha huku nikipata maumivu makali sana. Sikwenda kabisa hospitali hadi leo hii na nilipona kwa uwezo wa Mungu baada ya mwezi kupita. Leo nilipita ile njia ya kiwandani nikakumbuka kuleta kisa hiki.
Nimeamua nilete uzi kamili maana nili reply tu kwenye uzi wa kazi za viwandani huko nyuma.

Je, ni kazi gani ushawahi kufanya ilikuwa na risk ya kupoteza kitu au uhai kwenye maisha yako?
Maisha haya,pole sana jamani
 
Nilikuwa nafundisha shule moja katika halmashauri moja nchini ina mazingira magumu balaa. Nilikuwa nakaa kijiji cha pili na kulazimika kuvuka mito yenye mamba na viboko wengi. Ningepoteza maisha waajiri wangu wangesema ni uzembe nimetaka mwenyewe kutokukaa shuleni.
Kumbe wewe ni mwalimu
ndio maana una makasiriko kila siku....
 
Back
Top Bottom