Umewahi kufanya kitu gani cha maendeleo katika jamii yako?

Umewahi kufanya kitu gani cha maendeleo katika jamii yako?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
WanaJf,
SALAAM!

Jukwaa hili linaundwa na watu mbalimbali wa lika, na jinsi tofauti - wa elimu na ufahamu tofauti - wa viwango na nafasi tofauti.

Wote wetu tumegeuka kuwa wakosoaji wazuri wa masuala hasa ya kijamii na kiuchumi. Ni jambo zuri kukosoa lkn ni jambo zuri zaidi kuonesha njia kwa kufanya vitu vikubwa, vya kati, au basi vidogo ilimradi vichangie ukuaji wa kiuchumi na kijamii.

Sasa mimi au wewe kipi ulichofanya ktk jamii yako kiasi kwamba hata ukifa leo jamii itabaki ikijivunia?? Si vibaya ukikitaja na kutaja sehemu kilipo.

Msakila Kabende
Kakonko.
 
WanaJf,
SALAAM!

Jukwaa hili linaundwa na watu mbalimbali wa lika, na jinsi tofauti - wa elimu na ufahamu tofauti - wa viwango na nafasi tofauti...
Hizi K Vant nazogida, ni mishahara ya madaktari na walimu wengi.

Hizi kodi nazokatwa, wallah nimechangia kusomesha wanafunzi wengi sana bure.

Hizi tozo nazokatwa kuna barabara zinajengwa kwa jasho langu japo mafisiem wanamsifia rais eti katoa hela ya kujenga barabara.

Sadaka nazotoa kanisani wachunngaji na mapadre wananenepa kwa jasho langu.

Ving'amuzi navyolipia...... kuna wafanyakazi wa AZAM na DSTV wanaserebula kwa kazi ya mikono yangu.

Haya mabando ya Simu jamaa zangu wa Voda kuna mtu kanunua kibajaji kwa jasho langu.

Sijui niendelee au inatosha kwa leo?
 
Kitu cha kijamii nlichowahi kukifanya niliwahi kupanga nyumba moja nikakuta maji ya shida mpaka uwende kwa jirani nikavuta Bomba mpaka hapo nlipopanga nimeishi miaka mitatu nikahamia kwangu mpaka leo Ile nyumba maji yapo wanaenjoy
 
Back
Top Bottom