Umewahi kuibiwa gari?

Umewahi kuibiwa gari?

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
5,771
Reaction score
17,849
Kuna jamaa alitoka Arusha kwenda nairobi na gari yake. Sasa akawa amepark sehemu ili akaulizie hoteli na aliporudi akakuta gari haipo!

Katika kuchanganyikiwa jamaa akampigia simu rafiki yake wa arusha na kumuuliza 'aise, hivi jana tulipoondoka pale bar, uliondoka na gari yangu eh?' vipi, we/jamaa yako amewahi kuibiwa gari? Reaction yako /yake ilikuwaje?
 
Mi kuna siku nilipaki kagari kangu sehemu, akaja jamaa akapaki pembeni ila kwa upande niliokua natokea, gari yangu ikawa haionekani. Yani kama haipo vile. Nakuambia miguu yote iliishiwa nguvu, jasho mwili mzima..
 
Nilishamuona Mdosi aliyeibiwa Gari lake alichanganyikiwa na kuanza kulitafuta mifukoni na uvunguni mwa magari mengine...

Me ilishanitokea kusahau nilipo park gari langu airport na pia Kuna siku niliendesha Honda nikaipark BP nikaingia supermarket then nikatoka na kuiacha pale nikaenda job hadi jioni ndio nikaanza kuitafuta then nikakumbuka nilipoiacha oi..
 
Ndio matatizo ya kutembelea gari yenye 3rd part insurance, huwi na amani
 
Aisay sijawahi lakini kuna mdogo wangu aliwahi kunichemsha.....Niliwacha gari yangu iko on, nikaenda kwenye super market moja.

Time narudi nikaona gari halipo kijasho chembamba kikanza kunitoka mara jasho la mvua.

Kumbe dogo ananicheck tu pembeni niikatoa simu ile kutaka kuwapigia simu police...Akatokeza brother vipi nikajua ni yeye tu kisha chemsha.

Aisay huyu dogo wangu matata sana.
 
nishaporwa gari chini ya mtutu wa bunduki. Nilichanganyikiwa sana. Namshukuru Mungu nimepata jingine lkn siwezi sahau tukio hilo.
 
yaani, alinimaliza kabisa.
Simu ya kitochi inatunza hadi scanned docs

Haahhahaa..na ina antivirus ya kutosha!...Na hizi simu za kitochi za siku hizi unaweza uka-install ubuntu..
Mtu akiiona ataidharau kumbe ina vitu vya kutosha.. Pole kwa kweli..
 
Jamaa yangu aliibiwa gari ya 20M alikosa usingizi kwa mda mrefu sana
 
​sio swala dogo unaweza toa haja ndogo na kubwa kwa wakati mmoja
 
Haya mambo ya kuibiwa haya sio mazuri kbs,
Niliwahi kuibiwa simu enzi hiyo ya simems ile ya kidole gumba nikiwa natoka likizo narudi shule pale iringa stend,
Nilichanganyikwa nililia mpaka nafika bwenin usiku kucha sikulala kesho yake mapema nikapanda basi kurudi dar,
Nimefika huku watu wananishangaa niliingia hm kwa anko nakilio cha haja,wakanihurumia ila akaninunuliwa nyingine nikarudi shule,
Huwa wananikumbushaga na kunicheka sana!!
 
Back
Top Bottom