Umewahi kuingilia ugomvi usiokuhusu halafu yakakukuta makubwa?

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
35,012
Reaction score
70,201
Kuna watu hatupendi wengine waonewe hivyo tunaingilia ingilia sana ugomvi wa watu. Magu anasema 'Kuwashwa washwa' anyway wakati mwingine show unayoiingilia jukwaa ni kubwa show ndefu halafu wewe pumzi ndogo.

Nina visa vingi vingi (si unajua ukiwa mlinzi wa club eeh? Au kuishi uswazi?) Basi nitaandika kimoja kimoja kadri nitakavyokumbuka.

Nilipanga chumba maeneo fulani hivi kulia napakana na mshkaji bachela kama mimi kushoto yupo jamaa na mkewe na kachanga nahisi kama miezi miwili haizidi minne.

Basi siku hiyo usiku kama saa nane nikawa nasikia mwanamke anamwambia mwanaume (hakuna ceiling board)
"Mi sitaki bwana niache" nasikia jamaa akinong'ona kwa besi akili yangu ikaniambia jamaa anataka tendo.
Kisha nikasikia kilio cha binti kile chembamba cha chini chini lakini cha kwikwi.

Akili yangu ikaniambia jamaa anaomba jicho nini analila kilazima. Kisha sauti ikaongezeka halafu nikasikia chombo cha udongo kinavunjika halafu zikafuatia purukushani na mwanaume akitukana, hapo nikashtuka.
Nikafungua mlango, nafika sebuleni nakuta wapangaji wengine walikua hapo muda tu, wamama wawili na yule mshkaji wa kulia kwangu.

Basi nikajitia ujasiri nikaenda kugonga mlango purukushani zikakoma nasikia kilio tu cha binti. Nikazidi kugonga mara mlango ukafunguliwa akatoka yule mwanamke mbio jamaa akaja mlangoni kufunga mlango.
Tukakutanisha macho, hakusema kitu na mimi kimya tunatazamana tu. Akafunga mlango.

Wamama wakasema yule binti atakua kakimbilia ukweni kwake.

Nikarudi kulala..........

 
Hahahaha ni kipi kikakusibu sasa mana umenifanya nisome had mwisho halaf haijaisha
 
Sasa natakiwa kwenda Kigamboni asubuhi nikawa nipo Mwananyamala A nasubiri gari la Stesheni upande wa pili namuona yule mshkaji.
Mshkaji kuniona akaanza kukimbia, sijui ujinga niliutoa wapi, nikamuunganishia bwana.

Nikaenda kumkamata pale shule ya Kisiwani. Basi ile kumfikia na kumshika tu jamaa kilimtoka kichwa hiko kikatua moja kwa moja kwenye paji la uso.
Bado mawenge yamenivaa nashangaa nipo chini, kumbe nimekula mtama.

Ghafla jamaa yuko juu anapeleka mikono mvururu usoni, hapo naomba Mungu wasamaria waje. Wakaja kumtoa nipo chini hoi shenzi mimi.

Nyumbani tulipofika hatukuongeleshana.

Huo ugomvi namba moja.
 
Kuna rafiki yangu anamiliki video library so anaburn miziki na watu wa ofisi hizi hua wanaweka sauti za muziki juu sana.

Basi tumekaa hapo mara akaja jamaa, mtu wa makamo kama miaka 45 hivi mfupi, mweusi, mwili mdogo mdogo, akauliza.
"Nani mhusika hapa?"
Mshkaji akajibu "Mimi"
Jamaa akaendelea "Watu wanasema wamekufuata kama mara nne upunguze sauti"
Mshkaji wangu akajibu "Hapana hapa hajaja mtu au Castr umemuona mtu?"
Nikajibu "Hapana" (Ni kweli hakuja mtu)
Akaendelea yule jamaa "Basi sawa, punguza sauti"
Mshkaji wangu akamjibu "Siwezi kupunguza, wateja wanatakiwa wajue kua nipo"

Yule jamaa akajibu sawa akaondoka, baadaye kidogo akarudi na mtu mwingine. Wa makamo pia ila ana mwili kumzidi huyu, mrefu na mweupe lakini anaonekana kalewa au ni mlevi wa kila siku.

Jamaa wakaanza tena utata juu ya sauti. Mimi nikasema kwani mbona mnamsumbua mshkaji wangu shida nini. Yule mwenye mwili mdogo akajibu "Haikuhusu kaa pembeni"
Nikasimama nikapeleka kitasa, kikampata yule mlevi wa kila siku akasema "Wewe unaipiga serikali?" Nikamwambia "We mwenyewe unasemaje?"

Hapo watu wakawa washajaa, si unajua uswazi? Kwahiyo nikawa nakula ujiko natamba. Nikamwambia "Toeni vitambulisho basi kama nyie serikali"

Nilikua sijui serikali hua inaajiri walevi mbwa kwa ajili ya kazi zao, hivyo sikudhania kuwa hawa wanaweza kua watumishi wa serikali.

Vitambulisho vikatoka.

Mweupe ni mtendaji wa kata ya Mwananyamala kwa Kopa na mweusi ni askari kanzu wa kituo kidogo cha Kwa Kopa.

Nilinywea.

Natamani kukimbia lakini nahofia watu wataona kumbe jamaa muoga.

Niliyempiga kitasa akatoa pingu,nikavalishwa mpaka kituo kidogo cha kwa Kopa.

Mizunguko miiiiiiingi lakini nikatoa hela ndiyo nikatoka.
 
Enheeew endelea siku nyingine ikawaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…