Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi niliamulia ugomvi wa gelofriendi wangu na shosti yake enzi hizo. Baada ya wiki mbili shosti wa gelofriendi wangu akanizawadia papuchi kama shukrani ya wema wangu.Kuna watu hatupendi wengine waonewe hivyo tunaingilia ingilia sana ugomvi wa watu. Magu anasema 'Kuwashwa washwa' anyway wakati mwingine show unayoiingilia jukwaa ni kubwa show ndefu halafu wewe pumzi ndogo.
Nina visa vingi vingi (si unajua ukiwa mlinzi wa club eeh? Au kuishi uswazi?) Basi nitaandika kimoja kimoja kadri nitakavyokumbuka.
Nilipanga chumba maeneo fulani hivi kulia napakana na mshkaji bachela kama mimi kushoto yupo jamaa na mkewe na kachanga nahisi kama miezi miwili haizidi minne.
Basi siku hiyo usiku kama saa nane nikawa nasikia mwanamke anamwambia mwanaume (hakuna ceiling board)
"Mi sitaki bwana niache" nasikia jamaa akinong'ona kwa besi akili yangu ikaniambia jamaa anataka tendo.
Kisha nikasikia kilio cha binti kile chembamba cha chini chini lakini cha kwikwi.
Akili yangu ikaniambia jamaa anaomba jicho nini analila kilazima. Kisha sauti ikaongezeka halafu nikasikia chombo cha udongo kinavunjika halafu zikafuatia purukushani na mwanaume akitukana, hapo nikashtuka.
Nikafungua mlango, nafika sebuleni nakuta wapangaji wengine walikua hapo muda tu, wamama wawili na yule mshkaji wa kulia kwangu.
Basi nikajitia ujasiri nikaenda kugonga mlango purukushani zikakoma nasikia kilio tu cha binti. Nikazidi kugonga mara mlango ukafunguliwa akatoka yule mwanamke mbio jamaa akaja mlangoni kufunga mlango.
Tukakutanisha macho, hakusema kitu na mimi kimya tunatazamana tu. Akafunga mlango.
Wamama wakasema yule binti atakua kakimbilia ukweni kwake.
Nikarudi kulala..........
Hahaha kwahiyo ugomvi wa Humble na CCNP kwako hauna faida?Mi niliamulia ugomvi wa gelofriendi wangu na shosti yake enzi hizo. Baada ya wiki mbili shosti wa gelofriendi wangu akanizawadia papuchi kama shukrani ya wema wangu.
Tangu siku hiyo niko makini sana kufuatilia gomvi za jinsia KE. Huwezi jua mipango ya shetani, naweza nikalamba bingo tena
Acha wauane tuzidi kuwa wachacheHahaha kwahiyo ugomvi wa Humble na CCNP kwako hauna faida?
Hahaha mngetoka ndukinakumbuka mwaka 2013 life la chuo na ujana damu inachemka kila weekend club..
tulikuwa washkaj watatu mimi gatsby..bruno..na masai mmoja tulikuwa tunamuita pede
tumekula bia za kutosha pale Club Wantansh kwa nje mida ya saa saba na nusu usiku tukasema ngoja tuzame ndani kubambia na ikiwezekana kung'oa wadada wa masaki (maana kama mara mbili mimi na bruno tulitunukiwa na wadada wakubwa wakubwa kiumri baada ya kudance nao)
ile tumezama ndani tukaanza kucheza huku tunaendelea kula bia ikafika mida ya saa 8 na nusu yule mwenzetu masai pede akazima tukamuweka kwenye sofa sisi tukaendelea kula maisha
gafla tunaenda kumchek tunakuta anakula mate na lishoga jamaa hajielewi hapo anajua kaopoa demu nikamwita bruno tukaenda pale cha kwanza hatujauliza tukampa yule shoga vibao vya maana ..akasepa
gafla karudi na mashoga wenzake kama sita wametujalia pale kwenye sofa wanaanzisha utata mmoja akasema au mnamuonea gere mwenzenu na nyir mnataka gafla akamrukie bruno akampusu mdomon mamaaeee tukaachia bonge la ngumi yule shoga chali
hata mabaunsa walipotokea wakaanza kutupa za chemba mimi na bruno wakatubeba juu juu wakaenda kututupa nje hapo tumechezea za uso tumevimba
kumbe bwana meneja wa pale wantanshi anapenda mashoga yawepo mule ndan ili kuvutia wazungu waje pale... kesho yake hatukwenda chuo maana bado tulikuwa tumevimba yule maasai pede tunamsimulia kisa kilichofanya tupigwe anabisha eti kuwa ajaliwa mate na shoga [emoji23][emoji23][emoji23]
Halafu kipigo cha mtu anayeingilia hua kinakua cha mwana ukome ili siku nyingine usirudieIyo inaitwa "KUNUNUA UGOMVI"
ebwana kuna jamaa alinunua ugomvi wa rafiki ake aliyekua anapata kichapo na raia wenye hasira kali...
Jamaa katokea from nowhere kanunua ugomvi...akitegemea ataungana na yule aliyekua anapigwa..
Basi bwana yule aliyekua anapigwa kapata lifetime chance akachomoka akamuacha mnunuzi......
Ebwana zile Raia zikamshuhulikia yule mnunuzi wa ugomvi kwa kipigo cha mbwa mwizi!
Akaapa kamwe hatakaa anunue ugomvi tena maana aliingia kwa nia njema ya kumuokoa rafiki ..rafiki akamkimbia..
Akazidi kusema kua ."......kwa kumsaidia mtu kama anapigwa eti ataenda kutoa taarifa nyumbani kwao kua ndugu yenu anakufa kule kaamueni.."
Sent using Jamii Forums mobile app
ilikuwa ambush kaka 😂😂 sisi tupo bize tunawapiga wale mashoga gafla mbavu zimeingia bila hata kuuliza tukaanza kuchezea ...tulivyoona hawa hatuwawez tukajilaza chini ndio wakatubeba wakatutupa njeHahaha mngetoka nduki
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hilo ambush si mchezo unaweza kuona unakimbia unawaponyoka kumbe ndo unaelekea upande waoilikuwa ambush kaka [emoji23][emoji23] sisi tupo bize tunawapiga wale mashoga gafla mbavu zimeingia bila hata kuuliza tukaanza kuchezea ...tulivyoona hawa hatuwawez tukajilaza chini ndio wakatubeba wakatutupa nje
Ulikuwa mdoogo km piritonKuna rafiki yangu anamiliki video library so anaburn miziki na watu wa ofisi hizi hua wanaweka sauti za muziki juu sana.
Basi tumekaa hapo mara akaja jamaa, mtu wa makamo kama miaka 45 hivi mfupi, mweusi, mwili mdogo mdogo, akauliza.
"Nani mhusika hapa?"
Mshkaji akajibu "Mimi"
Jamaa akaendelea "Watu wanasema wamekufuata kama mara nne upunguze sauti"
Mshkaji wangu akajibu "Hapana hapa hajaja mtu au Castr umemuona mtu?"
Nikajibu "Hapana" (Ni kweli hakuja mtu)
Akaendelea yule jamaa "Basi sawa, punguza sauti"
Mshkaji wangu akamjibu "Siwezi kupunguza, wateja wanatakiwa wajue kua nipo"
Yule jamaa akajibu sawa akaondoka, baadaye kidogo akarudi na mtu mwingine. Wa makamo pia ila ana mwili kumzidi huyu, mrefu na mweupe lakini anaonekana kalewa au ni mlevi wa kila siku.
Jamaa wakaanza tena utata juu ya sauti. Mimi nikasema kwani mbona mnamsumbua mshkaji wangu shida nini. Yule mwenye mwili mdogo akajibu "Haikuhusu kaa pembeni"
Nikasimama nikapeleka kitasa, kikampata yule mlevi wa kila siku akasema "Wewe unaipiga serikali?" Nikamwambia "We mwenyewe unasemaje?"
Hapo watu wakawa washajaa, si unajua uswazi? Kwahiyo nikawa nakula ujiko natamba. Nikamwambia "Toeni vitambulisho basi kama nyie serikali"
Nilikua sijui serikali hua inaajiri walevi mbwa kwa ajili ya kazi zao, hivyo sikudhania kuwa hawa wanaweza kua watumishi wa serikali.
Vitambulisho vikatoka.
Mweupe ni mtendaji wa kata ya Mwananyamala kwa Kopa na mweusi ni askari kanzu wa kituo kidogo cha Kwa Kopa.
Nilinywea.
Natamani kukimbia lakini nahofia watu wataona kumbe jamaa muoga.
Niliyempiga kitasa akatoa pingu,nikavalishwa mpaka kituo kidogo cha kwa Kopa.
Mizunguko miiiiiiingi lakini nikatoa hela ndiyo nikatoka.
AiseeSiku moja nipo ofisini. Kuna binti anarushia watu chupa obviously ilitakiwa azuiliwe kabla sijamfikia mlinzi mwenzangu akawa kashamfikia kambeba yule binti anaenda kumtoa nje.
Bwana ake akamkwida mlinzi mwenzangu huku anatukana "M**nge ku****ako unaingilia ugomvi wa mademu si uwaache wapigane?" Mimi nikamtight jamaa tukatoka hadi nje.
Jamaa brazamen tu kavaa jinzi inabana nyeupe fulana nyeupe kapelo nyeusi na converse nyekundu. Demu wake katia gauni fupi jeusi kama sundress hivi.
Kwahiyo hawakuonyesha kama ni threat kivyovyote. Yule mlinzi mwenzangu akaanza kumpaka jamaa "We ku*a tu nikiamua nato**ba wewe na huyo demu" mimi hapo namwambia mshkaji "Hoya jikatae hatutaki washamba wa starehe humu"
Mshkaji akajibu "Nyi was**nge tu, miili tu hiyo hamna kitu" hapo watu washajaa tayari.
Tukamwambia jaribu kutugusa basi.
Akageuka akaenda kwenye gari alivyorudi akachomoa pistol akaionyeshea upande wetu.
Hata sielewei ilikuaje nikajikuta nimeganda sauti haitoki mshkaji wangu kashapiga magoti mikono juu.
Binti akaanza "Was*nge nyinyi kelele nyingi mbona mpo kimya?" Kwa unyonge nikafunguka "Dada tafadhali mwambie braza atusamehe"
Mara kaja supavaiza akamplease jamaa akamuelewa yule supavaiza, akaingia kwenye ndinga akasepa.
Sele bujeeeeNiko form two naelekea shule kuna washkaji wanne wakawa wanataka kupanda gari konda anawazuia. Ugomvi ukalipuka na mimi nikaunga kwenye ugomvi..
Washkaji hawanijui siwajui. Tukamtembezea kichapo konda safi kabisa.
Safari inaendelea ndani ni kutemeana maneno ya shombo tu akatuambia subirini mtanielewa tu.
Gari kufika Tandale Kwa Mtogole. Konda akashuka akaanza kuita "Sele Bujeeee, wee Sele Bujeeee njoo huku" dereva akawasha gari akaanza kuondoka akawa kama hataki ile ishu. Konda akadandia gari.
Sele Buje akadandia carrier ya nyuma ya gari, kituo cha Sweet Corner watu wakashuka Sele Buje akaingia ndani kwenye gari.
Ana muonekano wa kibabe knuckles zimechacha vibaya.
Anamuuliza konda "Nani analeta vurugu?" Konda katuonyeshea sisi, akaanza kutusogelea. Mimi hapo nakokotoa namna gani naweza kuruka kutoka dirishani nitue kwenye lami bila kugongwa kisha nikimbilie mitaa ya Manzese.
Hesabu hazijakaa sawa. Sele Buje kafika tu anakutana na dogo kutoka wale wanne wanasalimiana "Master vipi?" Sele buje anajibu "Shwari mbona mnakua wakorofi?" Dogo anajibu "Tumechelewa master sasa jamaa akawa anatuzuia ndiyo tukalazimisha kuingia"
Sele Buje akamgeukia konda "Hawa wadogo zetu bwana hawana shida"
Turns out Sele Buje alikua ni mwalimu wa boxing wa yule dogo.
Ila nilitetemeshwa sana.
Hahaha umeninukuu vibayaInaelekea we jamaa unapenda ugomvi saana
Ukikaa mwezi bila kupigana mwili unakuwasha
Sent using Jamii Forums mobile app