Umewahi kuingilia ugomvi usiokuhusu halafu yakakukuta makubwa?

Umewahi kuingilia ugomvi usiokuhusu halafu yakakukuta makubwa?

Siku moja nipo ofisini. Kuna binti anarushia watu chupa obviously ilitakiwa azuiliwe kabla sijamfikia mlinzi mwenzangu akawa kashamfikia kambeba yule binti anaenda kumtoa nje.

Bwana ake akamkwida mlinzi mwenzangu huku anatukana "M**nge ku****ako unaingilia ugomvi wa mademu si uwaache wapigane?" Mimi nikamtight jamaa tukatoka hadi nje.

Jamaa brazamen tu kavaa jinzi inabana nyeupe fulana nyeupe kapelo nyeusi na converse nyekundu. Demu wake katia gauni fupi jeusi kama sundress hivi.

Kwahiyo hawakuonyesha kama ni threat kivyovyote. Yule mlinzi mwenzangu akaanza kumpaka jamaa "We ku*a tu nikiamua nato**ba wewe na huyo demu" mimi hapo namwambia mshkaji "Hoya jikatae hatutaki washamba wa starehe humu"

Mshkaji akajibu "Nyi was**nge tu, miili tu hiyo hamna kitu" hapo watu washajaa tayari.

Tukamwambia jaribu kutugusa basi.

Akageuka akaenda kwenye gari alivyorudi akachomoa pistol akaionyeshea upande wetu.
Hata sielewei ilikuaje nikajikuta nimeganda sauti haitoki mshkaji wangu kashapiga magoti mikono juu.

Binti akaanza "Was*nge nyinyi kelele nyingi mbona mpo kimya?" Kwa unyonge nikafunguka "Dada tafadhali mwambie braza atusamehe"

Mara kaja supavaiza akamplease jamaa akamuelewa yule supavaiza, akaingia kwenye ndinga akasepa.
Ha ha ha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2006 kuna mwanangu wa dhahabu (R.I.P hommie) alikua anapiga kazi kwenye supermarket ya wazungu sasa mazoea ya utoto wa mtaani mwanangu ikawa daily anakwara bidhaa fulani muhimu anatuletea wanae maskani iwe bure au kwa bei ya chini ikawa neema kwetu kuliko maelezo,kumbe kuna mkolombwe mmoja alikua anapiga nae kazi akashtukia mchezo,siku mwana kavusha mzigo yule jamaa na mwenzie wakamtaiti nje tu ya ofisi wakampa option ya kuachiwa mzigo au wakaseme kwa watasha mwana aka-surrender akawapa mzigo walivyo wakuda wakampa kibano kikali sana na vitisho juu.
Basi swahiba kaibuka uswazi akatupa mkasa huwezi amini watu 4 tukasema kesho tuna dili na uyo bwege kweli tukaibuka super-market tukasubiri anachomoka na sisi tukazama nae kwenye daladala iyo iyo basi kushtuka jamaa kashuka Mtogole pale nasi tukashuka hatukumsogeza mbali tukampa kibano tukiwa na swahiba wetu kumbe yule mbwee kwao sio mbali si akapiga kelele za wezi wananiua sijui maraia walitokea wapi ila nilijiona nina kundi la watu nyuma yangu wana jazba haswaaaa na mitaa siijui nikazama kwenye jumba bovu moja nikapokelewa na wahuni wanakula kaya uku wanacheza kamari ile wakanituliza tayari raia wako nje jamaa wakaniuliza kulikoni nikawapa mkasa basi mtabe 1 akatoka kuwasambaratisha raia nikatulizwa kama saa 1 mle ndani wakaniambia unaelekea wapi usindikizwe duh huwezi amini niliwacheulia wale jamaa mapene yangu yote nikabaki na nauli kwa shukrani wakanipitisha vichochoroni mpaka kituo kingine nakadandia chuma mpaka home,uwoga ukawa kusema kuhusu wale wenzangu ila nashukuru mpaka kufika usiku wote tulikua salama ingawa kila mtu alitimkia kwake.
Huo ndio uwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2006 kuna mwanangu wa dhahabu (R.I.P hommie) alikua anapiga kazi kwenye supermarket ya wazungu sasa mazoea ya utoto wa mtaani mwanangu ikawa daily anakwara bidhaa fulani muhimu anatuletea wanae maskani iwe bure au kwa bei ya chini ikawa neema kwetu kuliko maelezo,kumbe kuna mkolombwe mmoja alikua anapiga nae kazi akashtukia mchezo,siku mwana kavusha mzigo yule jamaa na mwenzie wakamtaiti nje tu ya ofisi wakampa option ya kuachiwa mzigo au wakaseme kwa watasha mwana aka-surrender akawapa mzigo walivyo wakuda wakampa kibano kikali sana na vitisho juu.......

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Pole sana
 
Kuna mpangaji mwenzangu ana mke na mtoto mmoja nahisi ni wa miaka minne yule mtoto.

Jamaa shughuli zake ni ufundi, kwahiyo akitoka kurudi usiku sana. Siku hiyo kawahi kurudi akakuta mkewe kapakatwa na kinyozi mmoja hivi barabarani. Jamaa hakuongea kitu.

Alfajiri ya saa 10 kelele za 'Nakufaaaaa' zikaanza. Mimi nakaa chumba cha nje miongoni mwa vyumba vitatu vya nje hawa mke na mume wanakaa vyumba vya ndani.
Hadi uingie ni lazima ufunguliwe mlango.

Basi washkaji wa vyumba vitatu wote tumetoka tunamsihi jamaa amuache binti. Huku tukwapigia kelele wa vyumba vingine wafungue. Mmoja wetu akaenda dirisha la mwenye nyumba ili afungue mlango.

Nikaona wanachelewa nikaanza kupiga mateke mlango. Bwana muvi zinadanganya kumbe mlango ni mgumu baada ya mateke kama nane nikaona nitajivunja nisubiri kwanza.
Mwenye nyumba akafungua mlango nikatangulai kufika mlango wa chumba cha jamaa. Kama kawaida yangu mateke tu, nabadilisha miguu tu.

Yule jamaa alivyofungua mlango akatoka ni kisu akanichana kwenye triceps kidogo coz niliwahi kutoa mkono. Binti akapata upenyo wa kukimbia mi nikamtight mshkaji akanyang'anywa kisu.

Mchana nimelala nagongewa na watu kama wanne natoka askari kanzu watatu, mmoja ana sare na yule jamaa. Jamaa anadai nimempiga asubuhi. Nikabebwa hadi kituo kidogo.

Mwisho askari wakasema ok huna kosa unatuachaje? Ikanitoka 20K narudi nyumbani mwenye nyumba ananiambia mateke yangu yamemharibia milango hivyo natakiwa nigharamie ama milango mipya au ile iboreshwe.

Mie hoi.
Hahaha....eti movie zinadanganya, wewe ulifikiri mlango ni sawa na pazia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nakumbuka mwaka 2013 life la chuo na ujana damu inachemka kila weekend club..

tulikuwa washkaj watatu mimi gatsby..bruno..na masai mmoja tulikuwa tunamuita pede

tumekula bia za kutosha pale Club Wantansh kwa nje mida ya saa saba na nusu usiku tukasema ngoja tuzame ndani kubambia na ikiwezekana kung'oa wadada wa masaki (maana kama mara mbili mimi na bruno tulitunukiwa na wadada wakubwa wakubwa kiumri baada ya kudance nao)

ile tumezama ndani tukaanza kucheza huku tunaendelea kula bia ikafika mida ya saa 8 na nusu yule mwenzetu masai pede akazima tukamuweka kwenye sofa sisi tukaendelea kula maisha

gafla tunaenda kumchek tunakuta anakula mate na lishoga jamaa hajielewi hapo anajua kaopoa demu nikamwita bruno tukaenda pale cha kwanza hatujauliza tukampa yule shoga vibao vya maana ..akasepa

gafla karudi na mashoga wenzake kama sita wametujalia pale kwenye sofa wanaanzisha utata mmoja akasema au mnamuonea gere mwenzenu na nyir mnataka gafla akamrukie bruno akampusu mdomon mamaaeee tukaachia bonge la ngumi yule shoga chali

hata mabaunsa walipotokea wakaanza kutupa za chemba mimi na bruno wakatubeba juu juu wakaenda kututupa nje hapo tumechezea za uso tumevimba

kumbe bwana meneja wa pale wantanshi anapenda mashoga yawepo mule ndan ili kuvutia wazungu waje pale... kesho yake hatukwenda chuo maana bado tulikuwa tumevimba yule maasai pede tunamsimulia kisa kilichofanya tupigwe anabisha eti kuwa ajaliwa mate na shoga [emoji23][emoji23][emoji23]
Hahaha.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umenikumbusha miaka 8 iliyopita, ilikuwa mdogo wangu anapokea kipondo kutoka kwa baunsa flani kwa kumtusi mke wake basi mm kuona mdogo wangu anapokea kipondo nikaumia sana na kama ujuavyo "damu nzito kuliko maji" , si ndo nikajitosa ulingoni kumpiga tafu dogo ili baunsa tumchape kwa ushirika!! Ile napanda tu ulingoni kupiga tafu basi dogo akarudi benchi na kuniachia msala ulingoni.. Kipigo nilicho pokea anajua muumbaji. Ila sikujutia kumtetea dogo japo nae nilim-mind balaa.!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] dah pole sana mkuu
 
Ugomvi sio mzuri jamani ila nimecheka sana ila wanaume wa dar amna msimamo wa kiume unaoneshewa bastola unaanza kuomna msamaha na kuna mwingine kamng'ata mwanamke meno[emoji38][emoji38][emoji38]. Mimi sio mgomvi ila nilishirikishwa ugomvi mmoja na mshikaji wangu nayeye alinichukulia tu poa nilichoenda kukifanya mpaka alienialika alijuta kuniita akaniambia kumbe Haa mym una roho mbaya hivi.
 
Sasa natakiwa kwenda Kigamboni asubuhi nikawa nipo Mwananyamala A nasubiri gari la Stesheni upande wa pili namuona yule mshkaji.
Mshkaji kuniona akaanza kukimbia, sijui ujinga niliutoa wapi, nikamuunganishia bwana.

Nikaenda kumkamata pale shule ya Kisiwani. Basi ile kumfikia na kumshika tu jamaa kilimtoka kichwa hiko kikatua moja kwa moja kwenye paji la uso.
Bado mawenge yamenivaa nashangaa nipo chini, kumbe nimekula mtama.

Ghafla jamaa yuko juu anapeleka mikono mvururu usoni, hapo naomba Mungu wasamaria waje. Wakaja kumtoa nipo chini hoi shenzi mimi.

Nyumbani tulipofika hatukuongeleshana.

Huo ugomvi namba moja.
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ugomvi sio mzuri jamani ila nimecheka sana ila wanaume wa dar amna msimamo wa kiume unaoneshewa bastola unaanza kuomna msamaha na kuna mwingine kamng'ata mwanamke meno[emoji38][emoji38][emoji38]. Mimi sio mgomvi ila nilishirikishwa ugomvi mmoja na mshikaji wangu nayeye alinichukulia tu poa nilichoenda kukifanya mpaka alienialika alijuta kuniita akaniambia kumbe Haa mym una roho mbaya hivi.
Acha mkwar wako wewe hebu tuambie ulifanya nini
 
Ugomvi sio mzuri jamani ila nimecheka sana ila wanaume wa dar amna msimamo wa kiume unaoneshewa bastola unaanza kuomna msamaha na kuna mwingine kamng'ata mwanamke meno[emoji38][emoji38][emoji38]. Mimi sio mgomvi ila nilishirikishwa ugomvi mmoja na mshikaji wangu nayeye alinichukulia tu poa nilichoenda kukifanya mpaka alienialika alijuta kuniita akaniambia kumbe Haa mym una roho mbaya hivi.

Usiichukulie poa gun aisee achana na unavyoviona kwenye movie.
 
Back
Top Bottom