Umewahi kuingiliwa biashara na jirani / mshindani anaeuza kwa bei za chini mno ili kukuibia wateja, kukuondoa, kukuumiza , n.k. ulitoboa?

Ongea nae pengine hofu na ugeni kwenye biashara inamfanya ashushe bei, mfano mimi nilivokua naanza biashara ya hardware mshindani wangu aligoma kabisa kunipa ushirikiano wa bei, matokeo yake akawa analalamika mimi nauza vitu bei chini na mafundi pia walitumia ugeni wangu kwenye biashara kunilaghai kuhusu bei utasikia mwenzio yule anauza iki kitu bei fulani(bei ya chini)
Saiv nimekuwa mkongwe kwenye biashara hata mshindani wangu ashushe bei hainisumbui nafanya research je tunako nunua mzigo bei zimeshuka??
Je mwenzangu anauza bei hizi je yeye anausafiri wake binafsi wa kutoa mzigo kiwandani au mkoani

Baada ya hapo napata jibu kwambe hizi bei ni za upepo au za kudumu
 
Mimi nilianzisha mashine ya kukoboa na kusaga ya disel huko kijijini mkoa wa Tabora sasa nikakuta jamaa alikuwa nakoboa na kusaga kwa 1200 kwa debe.
Nilipoanzisha mimi nikaanza na bei 1000 nikakomba wateja woote alivyoona hivyo bila kuniuliza akashusha bei 800. Nami nikaona isiwe tabu nikashasha kukoboa na kusaga iwe 500 jamaa akchananyikiwa akashusha ikawa mia tatu.. mimi nikaweka utaratibu kukoboa na kusaga ni bure ila pumba unaacha. Jamaa alipandisha mikono juu na hadi leo nakoboa na kusaga buree ila pumba wanaacha. Nasafirisha tone za pumba kweli kweli
 
Kwa kiingereza inaitwa CUT THROAT COMPETITION (Ushindani wa kuchinjana makoromeo)

Ni aidha
  • jirani biashara imemshinda anaanza kuuza kwa bei za chini amalize mzigo
  • Mbinu ya kukuibia wateja kwa kuwauzia kwa bei rahisi kuzidi zako
  • Anataka uhame atawale soko hio sehem
  • Anataka kukutia adabu / kukukomesha / kisasi
N.k.
Binafsi nina jirani anauza kwa bei za chini mno
Simamia uhalali utashinda ni swala la muda tu
 
Mimi nilianzisha mashine ya kukoboa na kusaga ya disel huko kijijini mkoa wa Tabora sasa nikakuta jamaa alikuwa nakoboa na kusaga kwa 1200 kwa debe.
Nilipoanzisha mimi nikaanza na bei 1000 nikakomba wateja woote alivyoona hivyo bila kuniuliza akashusha bei 800. Nami nikaona isiwe tabu nikashasha kukoboa na kusaga iwe 500 jamaa akchananyikiwa akashusha ikawa mia tatu.. mimi nikaweka utaratibu kukoboa na kusaga ni bure ila pumba unaacha. Jamaa alipandisha mikono juu na hadi leo nakoboa na kusaga buree ila pumba wanaacha. Nasafirisha tone za pumba kweli kweli
Hahaha
 
Back
Top Bottom