Umewahi kujaribu kupika dagaa kwa mtindo huu?

Umewahi kujaribu kupika dagaa kwa mtindo huu?

Hujakutana na mafundi tu mkuu. Hata hiyo roast iliyopikwa hapo naona wengi hawajawahi kuila ndio maana wanadhani itakuwa imedodekwa karanga hadi ikakureketa kooni.

Nishapikiwa hivyo na sister mmoja wa kanda ya ziwa. Mchuzi unakuwa mzito na bila kuambiwa huwezi kusikia ile ladha ya karanga kabisaa
Hawajuhi utamu wake
 
Kuna dagaa ndizi tena mama alikua akipika hii kitu kila mtu anatoweka , tunashindia parachichi kutwa , mpka ratiba nyingine tena kwa sababu ratiba ya siku ya chakula gani alikua kabandika ukutani mwa jiko , siku ya choroko haoni mtu😁 Makiwendo
😂😂😂😂Hata Mimi choroko sizielewag kabisa
 
Hawajuhi utamu wake
Mtu anaeshangaa dagaa kuwekwa nyanya chungu na bamia. Bila shaka hajawahi kukanyaga kanda ya ziwa na hata dsm uswazi hajawahi kuishi maana huko hata nyama nusu inawekewa bamia na nyanya chungu ili mboga itoshe hadi usiku 😁😁..

Umejitahidi, hapo mchawi ni ugali laini tu uliomixiwa na unga wa muhogo
 
Kiufupi dagaa nyasa huwa nawakaanga kwanza theni naunga nyanya na kitunguu kwa juu(hoho huwa sipendi natupa kule) then nafunika nakuja nageuza inakuwa IMEISHAAA HIYOOOO kwani ugali uko wapi? 😂😂😂😂
Au sweery babe unasemajeee?
 
Mtu anaeshangaa dagaa kuwekwa nyanya chungu na bamia. Bila shaka hajawahi kukanyaga kanda ya ziwa na hata dsm uswazi hajawahi kuishi maana huko hata nyama nusu inawekewa bamia na nyanya chungu ili mboga itoshe hadi usiku 😁😁..

Umejitahidi, hapo mchawi ni ugali laini tu uliomixiwa na unga wa muhogo
Kunde, nyanya chungu aisee tupa kuleeee
 
Kula nyanya chungu zinasaidia kwenye memory na akili inakuwa sharp 😁😁
Daaah huwa nikila nahisi mwili unasisimkaa inavopita kwenye koo kuelekea tumboniii 😊🙌😬😬
 
Back
Top Bottom