Umewahi kukutana na utapeli wa aina gani?


Hao wenyeviti ungeanza nao,
 
Umewakomesha! Hivi dola 5,000 zitumwe kwenye box ulisikia wapiii???( In Bwege's voice)
Mtu anakutumia USD 5000 sawa na 11M TSh wapi na wapi? Hiyo faida ya kufika Mil 11 unakuja ipata lini?
 
Mimi nafatwa Sana inbox wasap wengine tupo nao memba baadhi ya magroup wananitaka urafiki, tusave contact zao, tujuzane hapa
 
Kuna mtu kanitumia hii meseji whatsupp alianza hivi

"Hello my dear beautiful lady [emoji257][emoji112]you are here honestly looking good"

Code ya namba yake ni +229,nilipomwambia kwamba mimi sio lady umekose namba,akasema Okay, haina shida hata tukiwa marafiki tu,nikamwambia haina shida ,baadae akajitambulisha jina lake akasema anaishi Italy-liverpool.

Mimi sikutaja jina ila nilimwambia naishi Tz,basi kashukuru kwa kumuelewa.

Baadae usiku akanitumia tu meseji ya Goodnight brother,nilikuwa sijawasha data kwahio niliikuta asubuhi yake.

Baada ya hapo hajatuma tena meseji yoyote tangu siku hio Jan 22 2022.


Nilijaribu kuangalia hio code mtandaoni nikakuta kama ni nchi ya kiafrika hivi,kwenye Profile photo yake ameweka Mzungu.

Sasa huyu sijui nae ni tapeli au alikosea tu namba tu? na hio ni code ya nchi gani?
 
Hatarious

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Nina eneo mkuu,tujenge then tuishi wote.pole sana
 
Pole sana mkuu
 
+229

Nchi ya Benin
 
Aisee huyo mtu kwa jins nilivyo sijui kama hadi saa hii angekua anaona dunia tamu
 
Ujinga wa wabongo ni kudhani kila mzungu ana hela ilihali kuna wazungu wana njaaa kushinda wabongo
Yaani wewe umeangalia tu hayo maandishi ukagundua ni mzungu? (Maana sidhani hata kama umesoma ukaelewa) ila kwa kuwa umesikia usa,umesikia kilichoandikwa ni kiingereZa basi ume conclude ni mzungu? Ninyi ndo hutapeliwa kirahisi sana. Maana hamjui kitu.na mnajua kila anayezungumza kiingereza ni mzungu 🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…