Umewahi kukutana na watu wa ajabu kwenye maisha yako? Walikuwa watu wa aina gani?

Umewahi kukutana na watu wa ajabu kwenye maisha yako? Walikuwa watu wa aina gani?

Kulikuwa na mtu huyu, wakati wa kusoma chuo cha ufundi, alikua ni mtu ambaye tulikuwa darasa moja pindi tupo chuo, alikuwa ni mkimya sana na hajawahi kuchangia chochote wala kuzungumza na mtu yeyote darasani.

Alikuwa Hana makundi, alikuwa hana ushirikiano, alikuwa hana marafiki. Hakuna mtu aliyejua sehemu alipokuwa akiishi, hakuna mtu aliyejua chochote kuhusu huyu mtu isipokuwa jina lake. Tukiwa darasani alikuwa hajibu maswali ila mitihani alikuwa anapata alama za juu sana.

Alikuwa kwenye group la whatsapp la chuo na hakuwahi ku-comment chochote na siku tulipomaliza chuo alileft Group, Alikuwa haendi Kanisani/msikitini na wala hakujihushisha na dini yoyote. Tangu ile siku ya mtihani wetu wa mwisho, hakuna mtu aliyemwona au kusikia Alipo.

Alikuwa hazungumzi kamwe labda tuaze sisi kuzungumza naye, na mda mwingine anaweza kukupuuza. Kama kutakuwa na tukio fulani maeneo ya chuo mara nyingi alichangia mchango kuazia Tsh. 40,000 na zaidi, na alipenda kutumia jina la mtu asiyejulikana, hata akichangia hakuwahi kuhudhuria sherehe/tukio hilo.

Wasichana katika darasa letu walimchukia sana , kwa sababu hawakuweza kuwa naye kwa namna yeyote ile.

Wengi wetu tuliamini kuwa yeye ni Afisa Usalama anayefanya kazi katika serikali ya Tanzania ambaye lengo lake labda lilikuwa ni kufuatilia usimamizi wa chuo. Alijifanya kama mcha Mungu na aliheshimiwa na kila mtu.

"Obidux Baljidanz" alikuwa mtu asiyejulikana.

Je, ni watu gani wenye mambo ya ajabu, ambao umekutana nao?

🙏🤔🤔🤔🤔
 
Alikuwa mcha Mungu ila hajawahi kuhudhuria msikitini wala kanisani. Alikuwa haongei na mtu kabisa ukajuaje ni mcha Mungu?

Alikuwa mcha Mungu ila hajawahi kuhudhuria msikitini wala kanisani.
Hayo maneno umesoma wapi mkuu,??? 🤔

"Alijifanya kama mcha Mungu na aliheshimiwa na kila mtu."
 
Kuna mwanangu anaitwa Erick huyu jamaa hatari kwa kumbukumbu .Mpaka saa kaimeza yote kichwani.Hata umuamshe usiku ,umuulize saa ngapi sasa hivi.Utajibiwa tu ni saa saba na dk 14 ukicheki kwenye simu ni kweli.Sijui ni jini huyu au alien.
 
Back
Top Bottom