Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Mapema wiki hii, Tyrese aliingia kwenye Instagram Live ili kuangazia zaidi uhusiano wake na Zelie Timothy—mwanamitindo ambaye walianza mahusiano mnamo 2021.
Alipoulizwa jinsi wawili hao walikutana, Tyrese aliwaambia watazamaji kuwa yeye ndiye alianza kumDM dada huyo hata hivyo Zelie aliingilia na kudai kuwa Tyrese hakuwa "type yake hata kidogo," na akafichua kwamba hapo awali alivutiwa zaidi na nyota mwingine wa Fast & Furious.
"Type yangu ilikuwa Paul Walker. Pumzika kwa amani,” Zelie alisema kuhusu marehemu mwigizaji huyo huku akimpapasa kichwa mpenzi wake. "Lakini [Tyrese] hakuwa type yangu hata kidogo. Ninasema tu nilipendezwa zaidi na Paul.”
Tyrese alionekana kukasirishwa na maoni hayo, na akamwambia mpenzi wake, "Usiniguse." Zelie alipuuza dalili hizo na kuendelea kuzungumza
"Hata nilipokutana na [Tyrese], nilisema, 'Eh, yeye ni mzee,'" aliendelea. "Ninapenda tabasamu lake. Ni poa sana. Pia personallity yake.”
Tyrese alionesha kuchukizwa zaidi na maneno hayo, hivyo akaaga na kutaka kutoka live, lakini Zelie aliendelea,
Watumiaji wengine wa Instagram walitaja matamshi ya Zelie kuwa "mbaya" na "ya kukosa heshima," wakati wengine walisadiki kuwa wapenzi hao walikuwa wakitania tu.
Je, ungekuwa wewe ni Tyrese ungefanyaje?