Umewahi kupitia msoto maishani hadi ukajuta kuzaliwa?

dah inafikia hatua unawalaumu walokuleta duniani bila hiali yako,chamsingi ukishafika kwenye dunia hii ni kukaza tu hakuna kuludi nyuma matatizo ni sehemu ya maisha yetu kuna vipindi vichache vya kicheko na vipindi virefu vya majuto.
 
Sometimes Mungu anatupitisha kwenye tanuru la moto ili tuujue ukuu wake.
Yani kuna wakati mtu unapitia magumu mpaka unahisi Mungu kakufungia vioo.
Sitokaa niusahau mwaka 2021.
Nashukuru Mungu nilisimama tena.
Sasa kama huyo Mungu anapitisha watu kwenye shida, Shetani yeye Huwa anapitisha watu kwenye nini ? Je ubaya wa Shetani ni nini
 
Usithubutu kukata tamaa kaza mpk kieleweke pia jitaidi kufanya ibada njia zitafunguka hutoamini itabaki story amini nikwambiayo ndg!
 
Mwaka wa tatu huu sina kazi ya kueleweka, nafanya vibarua tu mara saidia fundi, mara kutindua kuta za nyumba na mafundi umeme, kukatia fensi, kupalilia majani kwenye makazi ya watu, kuchimba mashimo ya vyoo, kubeba tofali,kusomba mchanga.Nina mke na watoto 2 bado nina mtoto wa nje ,kuna wakati nawaza mpaka napitiliza naanza kuongea mwenyewe, kifupi mimi ni kichaa ambae sijaanza okota makopo
 
 
Hela haitafutwi na ukiitafuta hautaipata kamwe.
 
dah inafikia hatua unawalaumu walokuleta duniani bila hiali yako,chamsingi ukishafika kwenye dunia hii ni kukaza tu hakuna kuludi nyuma matatizo ni sehemu ya maisha yetu kuna vipindi vichache vya kicheko na vipindi virefu vya majuto.
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…