umewahi kusahau kuwasha ama kuzima pasi, jiko, hita ya maji, rice cooker. n.k na ukaondoka... nini ulikikuta uliporudi ?

umewahi kusahau kuwasha ama kuzima pasi, jiko, hita ya maji, rice cooker. n.k na ukaondoka... nini ulikikuta uliporudi ?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
1. kusahau kuwasha

kuna siku niliweka mchele kwenye rice cooker nikawasha switch ila pale kwenye rice cooker sehemu ya cook sikubonyeza ,nikaenda kuanangalia muvi kwenye tv ,imefika saa 2 hivi nikasema ngoja nipakue nile nilale, naenda kufunua nakuta mifuta inaelea hakuna kilichopikika na nina njaa si mchezo, nikawasha upya huku nikiwa nimebanwa na njaa na hasira,

2. kusahau kuzima

kuna siku niliamka asubuhi kupasi nguo kabla sijamaliza kupasi umeme ukakatika, kwa vile nlikuwa na haraka nikasahau kuzima soketi ukutani nikaondoka. kurudi jioni kumbe umeme ulirudi!! yani nilikuta pasi imekuwa nyeusi tii na pale kwenye soketi pameungua pamepia shoti!! mama mwenye nyumba akiondoka na akiona hakuna mtu kabaki huwa anazima kule kwenye main switch, hio siku vinginevyo ningeunguza nyumba ya watu aisee
 
Niliweka maji kwenye jiko la gesi,Ka sufuria kadogo...nikajisahau nikaenda chuo kutokea Kimara....Niko Chuo nikashtuka sikuzima gesi....dooh nilitoka baru kama kichaa...chukua bodaboda na kupigia jirani nafika home maji yote yemekauka sufuria ndo ilikuwa inapigwa Moto sasa.Daah ilikuwa hatare na nusu.
 
Almanusura niunguze nyumba ya watu! Nashukuru kwamba dogo ambaye nilikuwa nakaa naye kwenye hilo ghetto alikuwa anaenda hospitali, sasa kufika njiani akakumbuka hajachukua kadi ya bima, akarudi home fasta kuja kuchukua. Mimi wakati huo nimeshakimbia darasani. Kumbe huku nyuma niliweka heater kwenye maji ili nikimaliza kuoga yatakuwa yamechemka niyaipue. Nimemaliza kuoga tu nakavaa na kukimbia darasani, weee dogo akakuta yanakaribia kuishia! Ilikuwa majanga!
 
Nilisahau pasi ya nguo on ,yaani nimenyoosha shati nikaenda chuo pasi bado iko kwenye umeme ,nilikuwa nikienda chuo Mornie kurudi hadi saa12 ingawa chuo kilikuwa karibu kama viwanja viwili vya mpira, siku hiyo kama nilichezwa machale nikarudi saa 6 namkuta mwenye nyumba anataka arekebishe sehem ya floor ilikuwa na tobo ambalo huwa linapitisha nyoka kutoka nje ,kulala na nyoka room ilikuwa ni daily sasa baada ya kuingia room naiona pasi inawaka taa nyekundu nikajua hapa kimeumana maana mwenye nyumba alikuwa anajua nilikuwa chuo tokea asubuhi, kitu kizuri alikuwa very humble naona alikaushia tu ,other wise ingekua msala
 
Jamaa yangu anafanya shughuli za ujenzi,siku moja karudi gheto kwake yuko hoi,akasema abandike mihogo ale alale,
Akatia kwenye jiko la gesi,kashika simu kitandani ana browse akasinzia bana akalala.
Kuja kuamka aliamshwa na harufu kali ya moshi usiku sana.
Maji yamekauka,mihogo imegeuka mkaa kabisa,sefuria jekunduuuu lote.
Akalisukumia huko hata kuzima gesi ilikuaa tabu,mana kiwashio kilichemka sana.
Sefuria halikufaa kitu lilitupwa kabisa.
..
Ukiwa msahaulifu Epuka sana kuwashawasha vifaa vya moto na umeme kama unajua una ratiba ya kutoka dakik 15 zijazo.
 
Kuna siku nilikuwa na kazi nyingi nikaamua nikeshe nikifanya kazi, maana asubuhi zingehitajika, ilipofika saa 4 usiku nikawasha gesi nikabandika kahawa. nimefanya kazi imefika saa kumi hivi nikaenda jikoni maana nilikuwa chumbani nafanya kazi, nikakuta sufuria imekuwa nyeusi tii kahawa imekauka.
 
WiFi enu alisahau kuzima rice cooker asubuhi then kaenda chuo,kurudi jioni rice cooker imeungua
We muongo rice cooker inajipimia yenyewe moto. Kwenye cook ikishawaka muda kadhaa hujiset yenyewe kwenye warm. Utakachokuta ni ubwabwa kuwa umekuwa na mvuke mwingi hadi kutepeta lakini sio kuungua mkuu.
 
mwananngu mmoja wakuitwa khalifa hizo show za kuacha mlango wazi, tv wiki nzima iko standby..kuacha pasi on..kwake issue za kawaida. kinachotokea watu wake wa karibu ndo tunakua makini kumkubusha..
Namchukia Sana mtu (Mpumbavu) wa hivi.
 
Duuh! Haijawahi kunikuta maana kila nikifanya kitu kwa haraka hua nazima hapohapo ila mi nimsahaulifu wakati nachezea cm au nikimpa kitu mtu huku naongea na mtu usingizini ndio kabisa naweza toa siri za kambi zote
 
Kabla ya kulala niliweka simu chaji nikasahau kuwasha socket asubuh mkurupuko wa kuwahi mishe nakuta simu asilimia 5% na umeme wa mgao maumivu yake si ya kitoto
 
Niliwasha electronic Egg cooker nikatulia kidogo kusikilizia dk chache nikasinzia kuamka masaa manne yamepita ndani kunanuka kama kiwanda cha kuunguza mpira.
Kuangalia mashine imeungua inayeyuka pia mayai yameungua
 
1. kusahau kuwasha

kuna siku niliweka mchele kwenye rice cooker nikawasha switch ila pale kwenye rice cooker sehemu ya cook sikubonyeza ,nikaenda kuanangalia muvi kwenye tv ,imefika saa 2 hivi nikasema ngoja nipakue nile nilale, naenda kufunua nakuta mifuta inaelea hakuna kilichopikika na nina njaa si mchezo, nikawasha upya huku nikiwa nimebanwa na njaa na hasira,

2. kusahau kuzima

kuna cku niliamka asubuhi kupasi nguo kabla cjamaliza kupasi umeme ukakatika, kwa vile nlikuwa na haraka nikasahau kuzima soketi ukutani nikaondoka. kurudi jioni kumbe umeme ulirudi!! yani nilikuta pasi imekuwa nyeusi tii na pale kwenye soketi pameungua pamepia shoti!! mama mwenye nyumba akiondoka na akiona hakuna mtu kabaki huwa anazima kule kwenye main switch, hio siku vinginevyo ningeunguza nyumba ya watu aisee
Utazoea ubachela kama hutaki bugudha
 
Nilitaka kuunguza room yetu UDOM, wakati naenda pindi mshkaji wangu nae alikuwa anatoka akakuta meza upande umeungua ndo linaanza godoro (PASI)

MAHARAGE, nyumba ya watu kidogo iishe (kimsingi iliisha) gesi hiyo.

Sio poa wazee
 
Nunueni pasi zinazojikata moto zenyewe
 
Nishawahi liwasha jug la maji nikizani kunakitu chakuchemshwa.

2754471_JamiiForums-1361292337.gif
 
Back
Top Bottom