umewahi kusahau kuwasha ama kuzima pasi, jiko, hita ya maji, rice cooker. n.k na ukaondoka... nini ulikikuta uliporudi ?

umewahi kusahau kuwasha ama kuzima pasi, jiko, hita ya maji, rice cooker. n.k na ukaondoka... nini ulikikuta uliporudi ?

Nilibandika sufuria kwenye gas nikatia mafuta nikajipumzisha dakika kadhaa

Nilipokuja kuamka naona moshi kidogo ila sufuria bado nyeupe haina weusi wowote

Basi nikazima gas fresh tu sekunde chache nashangaa moto ukawaka katikati ya sufuria

Nikashangaa huku natafuta njia ya kuuzima kwa haraka

Wazo la kutumia maji likaja nikachota ile namimina

Uliwaka moto nikahisi niko bwawani naogelea moto yaani macho yanaona mawimbi tu ya rangi nyekundu

Nikajua leo ni mwisho wangu pamoja na kila kitu

Tuwe Makini jamani!!
 
Back
Top Bottom