Ndugu yangu mmoja alipata ujauzito akaishi nao vizuri lakini kwa bahati MBAYA kwake ulikua n mimba ya kwanza hivyo hakuwa anacheki mara kwa mara kama mtoto akicheza.
Hivyo last time Kabla ya kujifungua alihisikia vibaya na akapelekwa kliniki lakini muda aliokuwa anajisikia vibaya kumbe mtoto aliokuwa tayari amepata tatizo tumboni alikosa virutubisho muhimu kwa AJILI yake hvyo ikapelekea mama kuzaa mtoto ambaye amekufa tayari.
Hivyo tunasikitika tulimpoteza mtoto mzuri kwa kosa la mama kuwa Hana uzoefu au ni uelewa juu ya ujauzito.
Hii pia iwafikie mabinti wenye mimba za kwanza wajue umuhimu wa kucheki afya ya mtoto mara kwa mara kwa wataalamu Kabla ya tatizo kutokea.