hoof eater
Member
- Jun 11, 2024
- 35
- 71
Habari za wakati?
Pengine kwa umri wako,nafasi au ufinyu wa muda ulionao umekupelekea Kutowahi kukaa ata dakika moja kwenye vijiwe vya bodaboda, basi zifuatazo ndio mada au agenda pendwa kwenye vijiwe hivyo.
Tips za kubeti;
kama we ni mdau wa betting hususani kwenye upande wa soka, basi jaribu kutembelea kwenye vijiwe vya bodaboda utakuja kunishukuru. Hawa jamaa wanafatilia ligi zote duniani na wajua timu nyingi sijawahi kuona, huku ndipo kuna mashabiki wa kisampasa ya uturuki, huku ndio unakuta mtu anaijua 1st eleven ya FC Basel.
Wake za watu;
Bodaboda wana siri sana, ila ukijichanganya kwenye vijiwe vyao siku mbili tatu, utajua mke wa nani analiwa na nani na mke wa nani anaenda guest gani? Yaani unaweza kukuta wanamjua mke wako kuliko unavyomjua wewe, aisee usiwadharau. Kiufupi wanaongoza kujua michepuko ya watu wengi wa mitaa husika especially wakina mama.
Ukisikia manzi yako anakwambia ana boda wake, basi ishi vizuri na huyo boda wake utakuja kunishukuru.
Wasanii wa bongofleva;
Kwenye vijiwe vya bodaboda hua kuna takwimu za ajabu sana za wasanii, yaani huku utaambiwa mpaka bei ya kiatu alichovaa diamond kwenye wasafi festival ya mwaka jana, bado ubishi wa mond na kiba nao haumalizi week mbili unaibuka.
Story ambazo ni nadra sana kuzisikia kwenye vijiwe vya bodaboda ni story za siasa, hawa jamaa unaweza kuwawekea 10000 wakutajie nafasi ya doto biteko serikalini na wakashindwa. Na hii ndio sababu wanatumika sana na wanasiasa unapokaribia wakati wa uchaguzi.
Usilojua kuhusu bodaboda hawa ndio wameukuza mziki wa singeli mpaka hapa ulipofika leo.
Niambie wewe umesikia story zipi kwenye vijiwe vya bodaboda.