Nafikiri hii inatokana na malezi pia ukaribu wa mzazi na mtoto.
Mzazi anae mjali mwanae ni ngumu kukutana na mambo kama hizi ikiwa mzazi atamlea mwanae katika yale yalio mema na akamuweka mwanae huru kwake.
Lakini pia haya yote yanatokana na wazazi kutokua wafuatiliaji wa watoto wao tangu utotoni, kumbuka hadi inatokea hivi maanayake mtoto hajabadilika kwa siku moja, bali alianza taratibu.
Na wazazi wanapo kua wakali kupita kiasi kwa watoto wao pia yaweza kuwa chanzo cha mambo kama haya kutokana na mtoto kujengewa hofu kubwa (kwamba wakijua nitauwawa), kumbe badala yake mtoto angesema pengine angesaidiwa mapema.
Anyways, nimecheka kwa aina hii ya utapeli, lakini nimejikuta napata uchungu kama mzazi.
Mambo ni mengi