Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

Mbwichichi

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2018
Posts
297
Reaction score
1,687
Leo nimeona mtu akifa kama utani na mbele yangu.

Wakati nikivuka barabara ghafla mtu mwanaume aliyekuwa mbele yangu akaanguka kama kapigwa shoti ya umeme.

Akajibamiza vibaya sana chini na pote pakaanza kutapakaa damu, inatoka kila eneo la wazi la mwili.

Sababu ya butwaa nilikosa cha kusaidia ila wakaja wadau hapo wakasema ni kifafa huyo, jamaa keshameza ulimi n.k yaani kuna mzee akamgusa akasema huyo tayari kafa.

Basi ikawa ndio hata hatujui nini kifanyike

Ila ndio ikawa tayari amekufa. Nikaahirisha na safari nikarudi zangu nyumbani.

Umewahi shuhudia mtu kufa ghafla?
 
Hatari sana.
Ombea Mungu usifiwe na demu ghetto, bora hotelini unaweza kutoka nduki
 
Watu wengi wanakufa kwa sababu ya kukosa huduma ya kwanza.. Kuna uwezekano huyo jamaa angepata mtoa huduma wa kwanza angeishi

Watu wengi hawajui kufanya ABC's (Airways, breathing and circulation )na Cadio pulmonary resuscitation (CPR) pindi kunapotokea dharura za kiafya mitaani

Kwa wenzetu FIRST AID Ni kitu kinachofundwa mashuleni tangu chekechea
____________________________
Siku moja nipo zangu mitaa ya mbagala rangi 3 Kuna mzee alikuwa anataka avuke barabara aingie pale stendi ya mabasi..akawa anatembea kwenye zile kingo za barababra ya mwendokasi huku anavizia gape la magari avuke...wakati umakini ameuweka ktk kuangalia magari avuke si akasahau km yupo juu ya yale matofali ya barabara(zile blocks zilizowekwa ili magari ya kawaida yasiingie ktk barababra ya BRT)..

Mzee akateleza akaangukia kule barabarani yanakopita magari (lane to city center) gari la Temeke-Magenge likamkanyaga kichwani na habari yake ikaishia hapo hapo sikuweza kutoa msaada wowote maana alishakufa hapo.Kuanzia ile siku nimekuwa making sn kutembea kwenye zile blocks nikitaka kuvuka maana hiyo tabia tunayo wengi sn hapa mjini kwenye barababra za BRT
 
"Akajibamiza vibaya sana chini na pote pakaanza kutapakaa damu, inatoka kila eneo la wazi la mwili".

Mshaanza kutengeneza taharuki mtaani.
 
Week 2 zilizopita Jumapili wakati tunavuka barabara kuna mzee aligongwa na bodaboda mbele yangu ilimrusha akaanguka akazimia nadhani, maana walimbeba pale wakamlaza pembeni wakawa wanampepea.
Natumai alipona yule mzee.

Lile tukio kila nikikumbuka mwili unasisimka, kweli kifo tunatembea nacho.
Ukiamka na ukirudi nyumbani kwako salama umshukuru Mungu
 
Sijawah na naomba isinitokee kabisa. Hivi ikifika hii hatua mtu unakua unawaona au vipi?
Can't wait to find out when I die
View attachment 2379823
I believe when we die the soul leave our bodies, therefore, the possibility of seeing such a thing does not arise, and if it does, then it will definitely not be in such a dimension, maybe utaweza kufika msibani kwako na kuona maiti yako ukiw kama mtu mwingine anavofika, hutokuwa ndani ya mwili bali hewani.
 
Mwaka 2001 hospital ya Agha Khan Mwanza......nilikuwa namuangalia mdogo wangu alikuwa kalazwa wodi moja na mzee mmoja wa Kihindi, usiku kama saa 5 hivi akaanza kuhangaikia pumzi akaniomba nimuwashie feni, nikawasha halafu nikaenda kumuita nesi aliyekuwa zamu.

Alipofika akamuangalia kisha akaniambia niwe namgandamiza kifuani upande wa moyo yeye anafuata vifaa, nikaanza hiyo kazi......yule mzee alinishika shati kifuani kama vile kunikwida, nikajua labda anaanza kupata nafuu, nikaongeza juhudi, nesi anakuja ile kumuangalia akaniambia huyu tayari keshafariki........niliumia sana moyoni.
 
Kuna siku nilikuwa na mgonjwa sijui ndo mwaisela Ile, Muhimbili kwa wanaume

Sasa nimeshafika juu ila nikakosea direction ile napepesa macho huku na kule nikamkuta mzee mmoja alikuwa kwenye kile kitanda cha kusukuma yupo peke yake.

Sekunde tu akaanza kurusha miguu na mikono nikabakia nimepigwa na butwaa

Kuja kushtuka amekakamaa nadhani ndo alifariki hivyo,

Kwa kweli lile tukio halijawahi kunitoka kichwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…