Mbwichichi
JF-Expert Member
- Dec 19, 2018
- 297
- 1,687
Leo nimeona mtu akifa kama utani na mbele yangu.
Wakati nikivuka barabara ghafla mtu mwanaume aliyekuwa mbele yangu akaanguka kama kapigwa shoti ya umeme.
Akajibamiza vibaya sana chini na pote pakaanza kutapakaa damu, inatoka kila eneo la wazi la mwili.
Sababu ya butwaa nilikosa cha kusaidia ila wakaja wadau hapo wakasema ni kifafa huyo, jamaa keshameza ulimi n.k yaani kuna mzee akamgusa akasema huyo tayari kafa.
Basi ikawa ndio hata hatujui nini kifanyike
Ila ndio ikawa tayari amekufa. Nikaahirisha na safari nikarudi zangu nyumbani.
Umewahi shuhudia mtu kufa ghafla?