Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

Nilikuwa dogo mwenye upako mwingi, tulienda kumtembelea mtumishi mmoja anaumwa, tukafika pale piga story na mgonjwa kabla ya kuondoka tukaomba, wakati wa maombi mimi nilisimama kando ya mgonjwa karibu na mkono wake, katikati ya maombi mgonjwa akawa ananishika vidole vyangu kama anataka kunishika mkono wangu, alifanya hivyo kwa kurudia kama mara nne au less, tulivyomaliza maombi tukawa tunamuaga mgonjwa, kila tukiita kimya kila tukiita kimyaaa, kumbe jamaa ndo tayarii amekufa kwa mtindo huo.

Nilikuwa mdogo nakumbuka tunaondoka pale njia nzima nilikuwa natetemeka na kujiuliza marehemu alikuwa anataka kuniambia nini kwa kujaribu kunivuta vidole vilee? Marehemu alikuwa kijana tu 22yrs
Ulikuwa umefunga macho?
 
Mwezi wa tano mwaka huu mtoto wangu alikuwa kalazwa KCMC kwa shida ya moyo. Saa 7 usiku daktari akanipigia simu kuwa hali ya mtoto imebadilika ghafla. Niliwasha gari na kuelekea hospitali haraka na kufika tu dogo akanishika mkono akakata roho....

Natamani sana nisingepigiwa ile simu. Mzazi hapaswi kuzika mtoto bali mtoto ndio amzike mzazi
Ni bora umepigiwa simu, mtoto amekuona na kukushika kwa mara ya mwisho.
 
Pole sana na Mwenye Enzi Mungu ani epushilie mbali walahi [emoji22]
Rip kwa aliye kufa!
 
Ndio maana tunatakiwa tuishi, tuna nafasi ya kuishi mara moja tu, ikipita hiyo haiji tena. Kuishi na kufa ni kitu cha dk moja tu..mzee wangu alinifia mikononi, sekunde kadhaa tu tunaongea ananiambia "hatutafika hospital ", wakati naendelea kutafakari alichoongea huku naendesha kama chizi barabarani, akageuka upande wa pili na hadithi ikaishia pale.
 
Week 2 zilizopita Jumapili wakati tunavuka barabara kuna mzee aligongwa na bodaboda mbele yangu ilimrusha akaanguka akazimia nadhani, maana walimbeba pale wakamlaza pembeni wakawa wanampepea.
Natumai alipona yule mzee.

Lile tukio kila nikikumbuka mwili unasisimka, kweli kifo tunatembea nacho.
Ukiamka na ukirudi nyumbani kwako salama umshukuru Mungu
Kama ni pale tegeta yule mzee alikufa
 
Kuna waziri flani wa zamani enzi za nyerere kipindi cha corona ilimshikaa yani alitengwaa yule mzee hata ndugu zake walikuwa wanakuja kwa nadra sana mpka nikawa najiuliza hivi hana watoto??? aise nikajifunza kitu kikubwa sana MAISHA YAKO NI WEWE MWENYEWE muda ukifika huna nguvu bhasi ur on ur own kiufupi alifariki pale siku nikiwa off nkasikia tu redioni. Live to the fullest while u can.
 
Maisha tuliyo nayo ni mafupi sana ,haina haja ya kuchukiana hata kidogo.
 
Nilisoma huko nyuma uliandika hivi(sijui kwa nini nimefungua huu uzi), leo tena umeandika the same. Huu uzi nimeusoma leo yote kila nikipata mda, nimewakumbuka wapendwa wangu.
Mi najibu quotes zako tu sisomi tena comments nyingine
 
Mi najibu quotes zako tu sisomi tena comments nyingine
Acha woga, ukiwa mkubwa unatakiwa ujue kuwa mume anaweza kukufia mkiwa ndani wawili, mama/baba yako, mtoto wako. Ni aibu kuanza kupiga mayowe kabla ya kumuweka sawa mtu wako...hahaha nazidi kukuogopesha🤣🤣
 
Kwaheri...sirudi tena hapa nakwambia
 
Kuna waziri flani wa zamani enzi za nyerere kipindi cha corona ilimshikaa yani alitengwaa yule mzee hata ndugu zake walikuwa wanakuja kwa nadra sana mpka nikawa najiuliza hivi hana watoto??? aise nikajifunza kitu kikubwa sana MAISHA YAKO NI WEWE MWENYEWE muda ukifika huna nguvu bhasi ur on ur own kiufupi alifariki pale siku nikiwa off nkasikia tu redioni. Live to the fullest while u can.
Maisha ni ubatili.
Vyote tunavyotafuta ni bure.
 
Back
Top Bottom