Nilikuwa dogo mwenye upako mwingi, tulienda kumtembelea mtumishi mmoja anaumwa, tukafika pale piga story na mgonjwa kabla ya kuondoka tukaomba, wakati wa maombi mimi nilisimama kando ya mgonjwa karibu na mkono wake, katikati ya maombi mgonjwa akawa ananishika vidole vyangu kama anataka kunishika mkono wangu, alifanya hivyo kwa kurudia kama mara nne au less, tulivyomaliza maombi tukawa tunamuaga mgonjwa, kila tukiita kimya kila tukiita kimyaaa, kumbe jamaa ndo tayarii amekufa kwa mtindo huo.
Nilikuwa mdogo nakumbuka tunaondoka pale njia nzima nilikuwa natetemeka na kujiuliza marehemu alikuwa anataka kuniambia nini kwa kujaribu kunivuta vidole vilee? Marehemu alikuwa kijana tu 22yrs