Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

Ni ngumu sana lakini ndio haki halisi ya binadamu kuja na kuondoka bila kujali mazingira muda na mahali.

Mwaka wa kumi mwezi huu bibi yangu nilikesha nae usiku kucha akiwa anahangaika sana kupigania uhai, niseme tu sikudhani kama usiku ule ulikuwa ndio ni mwisho wake, lakini tuliongea mengi tokea saa 12 jioni mpaka saa 11 asubuhi akaniambia niende nje au nikalale kumbe naye ndio analala daima.

Sidhani kama maumivu yale nitakuja kuyahisi tena, hadi naandika hapa chozi limenitoka aisee!

Kwa umri aliokuwa nao ilitosha kusema alistahili kuishia pale maana ilikua 102 ila mimi niliona haikustahili , yeye alinipokea kutoka kwa mama nikiwa na mwezi mmoja, miaka 2 mbele akaingia uzee asiejiweza , nikaingia mzigoni tokea nikiwa na miaka 4, mpaka anakufa maisha yalikua yameanza kuonyesha nuru walao ningefanya chochote juu yake but ndio tukaacha kihivyo [emoji24]

Wapumzike kwa amani ndugu zetu jamaa na marafiki , Duniani hapa tu wapitaji na uwenyeji ni mbinguni. Mungu atukuzwe.
 
Mwezi wa tano mwaka huu mtoto wangu alikuwa kalazwa KCMC kwa shida ya moyo. Saa 7 usiku daktari akanipigia simu kuwa hali ya mtoto imebadilika ghafla. Niliwasha gari na kuelekea hospitali haraka na kufika tu dogo akanishika mkono akakata roho....

Natamani sana nisingepigiwa ile simu. Mzazi hapaswi kuzika mtoto bali mtoto ndio amzike mzazi
Tusikalili mkuu, kifo atupangi sisi kwamba nani aanze kwa maana hiyo anaanza yoyote sisi tukubaliane tu na matokeo ndio maisha yalivyo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Wanangu watatu walikufa siku za weekend baada ya kutoka kula bata wakidrive

Nikitafakari vifo vyao huwa nayaelewa sana maneno dont drink and drive
Daah umenikumbusha hii stori yako, kuna jamaa alikuwa basketballer chuoni , alikuwa anaitwa Othmani aka Ochu. Jamaa nasikia alitoka kulewa na mwana , ye akiwa suka akapata ajari tukamkosa mwanetu
 
Daah umenikumbusha hii stori yako, kuna jamaa alikuwa basketballer chuoni , alikuwa anaitwa Othmani aka Ochu. Jamaa nasikia alitoka kulewa na mwana , ye akiwa suka akapata ajari tukamkosa mwanetu
Inasikitisha sana mwamba kaondoka na kipaji chake
 
Mama yangu mzazi, ilikuwa tarehe 1/5/2020.

Majira ya saa tatu usiku, nimekaa na mama tunazungumza huku tukiwa tunatazamana machoni. Hapohapo mama alifumba macho na hakufumbuwa tena.

Nilipatwa na mshangao usio wa kawaida, RIP mama
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom