Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 3,876
- 7,118
DuhBad memory! Kuna siku nipo zangu Ubungo pale riverside nataka kuvuka upande wa pili m, barabara ya kwanza nikavuka, nikawakuta wenzangu wengiwengi tu wanatafuta gap wamalizie barabara ya pili wavuke. Sasa kuna mmama mmoja ‘may her soul rest in peace’ alidhani gari iko mbali, aisee kitu kililia puuuu! Semi ilimburuta ikamwacha kwa mbele damu inatiririka tu barabarani na maisha yake yaliishia pale. Niliumia sana moyoni, nikarudi geto kulala siku hiyo sikutoka.