Umewahi tokewa na kitu gani kisicho cha kawaida mpaka ukamshukuru Mungu?

Umewahi tokewa na kitu gani kisicho cha kawaida mpaka ukamshukuru Mungu?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Mwaka 2013 nilipofika dar nilifikia maeneo ya magomeni mapipa kwa ajili ya kufanya kazi za ndani, basi bhana ratiba za kazi ilikuwa kama hivi;

Nikiamka saa 12 nichote maji nioshe vyombo, nifua ninywe chai, nibebe maji ya kandoro nikauze tripu ya kwanza maji 50, ya pili na yatatu, mpaka saa 11 jioni nakuwa tayari nimerudi nyumbani kwa ajili ya kuanza kufunga maji ya kesho.

Maisha na boss wangu yalikuwa hivi,

Mshahara 20000 kwa mwezi maji yanayobaki ni yakwangu yaani ananikata mshahara, sasa nikiwa nimefanya kazi ndani ya kama wiki mbili hivi nakumbuka hiyo siku nilibeba zangu maji hiyo ilikuwa tripu ya mwisho kama saa kumi hivi jioni nikiwa nimeshauza maji yamebaki kama mawili hivi nikafika kwenye kituo cha mabasi ya mwendokasi wakati huo bado havijaanza kutumika, nikawa nimekaa zangu juu miguu imening'inia chini nikaanza kuhesabu hela.

Yalaaaaaa! asalale! mahesabu si yakagoma buku halipo nikajisachi mifuko yote ya suruali hakuna.

Nikaanza kuwaza yule mama leo ntamweleza nini mpaka aniamini, maana kuna siku nilipoteza 500 ya karatasi wakati huo katika harakati za kutoa chenji hakunielewa. Je, leo hii 1000 si ataninyonga?

Wakati nafikiria hayo yote Kutazama chini macho yakakutana uso kwa uso na paketi ya sigara SM ikiwa haijafunguliwa nikateremka upesi na kuichukua nilienda kuiuza kwa wale jamaa wanauza sigara kwa kutembeza Tsh. 1400/- nikafidia kwenye maji 400 nikala vitumbua.

Hakika sitasahau kwani nilimshukuru sana Mungu.
 
Back
Top Bottom