Pre GE2025 Ummy Mwalimu aanzisha "Amka na Samia Jogging" katika maandalizi ya kumpokea Rais Samia Tanga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi nini sababu ya Ummy mwalimu kuenguliwa baraza la mawaziri?
Sababu kubwa ni kwa kuwa cheo ni Dhamana. Leo unaweza kuwa Waziri na kesho usiwe Waziri lakini Kesho Kutwa ukarudishwa tena kwenye Uwaziri. Kama ambavyo ilikuwa na kutokea kwa viongozi kama Mheshimiwa Dkt Mwigulu Lameck Nchemba aliyekuwa waziri akatolewa na baadaye akarejeshwa tena na ni waziri mpaka leo.

Ilikuwa hivyo pia kwa Mheshimiwa George Simbachawene, Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi, Mheshimiwa William Lukuvi na wengine wengi ambao sasa ni Mawaziri lakini wamewahi kuwekwa pembeni kwa Muda na kisha wakarejeshwa tena Barazani.

Kwa hiyo katika serikali,uongozi na utumishi kwa Watu ni jambo la kawaida sana ambalo hutokea na kufanyika. Ni kama Timu ya Mpira tu ambapo leo kocha anaweza kukuanzisha kikosi cha kwanza lakini kesho ukawekwa Benchi au usipangwe kabisa hata Benchi.

Kwa hiyo hata Mheshimiwa Ummy Mwalimu Leo siyo Waziri lakini kesho Mheshimiwa Rais anaweza kumrejesha Katika Baraza la Mawaziri .

Kama una swali jingine wewe uliza tu mimi nitakujibu vizuri kabisa.
 
Tabia yake ya kumteta mama kaacha?
Kimsingi TISS wasicheze mbali na huyu kidudu mtu anaitwa UMMY. Huyo ni kirusi mbaya sana.

Rais Samia usije ingia kwenye mfumo, kaa mbali na Odo
 
Sawa Lucas, Nime understand
 
Tabia yake ya kumteta mama kaacha?
Mama a
Mama anafanya kazi kubwa sana, ila kazi hizo hazionekaniki pasipotokeza watu wa kuzisemea. Umenikumbusha kisa cha Abdul (sio huyu wa mama) aliyejenga kibanda mbugani akatangaza kuwa amemuona malaika na kuwaalika watu waende kibandani ambamo wangeweza kumuona. Ila aliweka sharti kuwa wenye dhambi wasingeweza kumuona, bali alikuwa anaonekanika kwa wasio na dhambi tu. Basi watu wengi wakaandamana kwenda kibandani wakitaka kumuona malaika. Kila aliyeingia aliona kiti na kandambili tu bali hakuna aliyemuona malaika. Ikawa kila aliyekuwa anatoka kibandani alipoulizwa kama amemuona malaika alijibu kuwa amemuona ili asijeonekana kuwa ana dhambi. Kila mwanaccm anajitahidi kuonesha kuwa anaziona kazi za mama, japo kiuhalisia hazioni, asijeonekana kuwa ni mdhambi (sio mwenzetu). Utumwa ni ugonjwa mbaya
 
Kwa kushindwa kusimamia MSD na NHIF, hawezi kuachaa kufanya hivyo (Kwa Neema ya mazao ya msd na nhif hawezi kuachaa kufanya hivyo) mpaka mashirika yamekonda bila jogging
 
Sasa kawandikia huu ujumbe wana Tanga watafika kweli uwanjani maana watu wa Tanga hawajasoma, wao wanajuwa kukariri Kiarab tu lakini lugha yao hawajuwi kusoma.
 
Kazi za Rais Samia zinaonekana vyema kabisa kwa kila mwenye macho
 
Mnamfanya Rais kama celebrity sasa.
Haya mambo yanashusha hadhi ya mamlaka ya Urais.
Haya mnayofanya haya tofauti na yanayofanyika North Korea kwa Kim Jong.

Hatuhitaji kumpamba Rais na mapambio, bali tunahitaji kuona utumishi wake kwa watanzania.
Kazi yake Kwa Watanzania ndio inapaswa kumpa mileage na sio kelele za wasanii Kila Kona na nyimbo za mapambio.
 
Ummy bado.amajipendekexa tuuuu?? Hutakiwii kaa pembenii wewe ni empty box .....
 
Acha wivu wako hapa wewe. Kwani wewe ni kipofu hadi ushindwe kuona makubwa yaliyofanywa na Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…