babu M
JF-Expert Member
- Mar 4, 2010
- 5,222
- 3,173
Mchapa kazi, ana ushawishi mkubwa ndani ya CCM na nje ya CCM, amekuwa akifanyia kazi kwa haraka na ufanisi mkubwa pale malalamiko yanapotokea kwenye wizara anazozisimamia, mtu wa kujituma nani mfuatiliaji yanayofanyika kwenye wizara yake kwa ukaribu zaidi(hana u-mangi meza!), Sio mtu wa kujikweza na kadhalika.
Baadhi ya historia ya Ummy mwenye wizara alizoziongoza:
Wizara ya Afya - Zika.
Ummy Mwalimu sio bendera fuata upepo. Ni kiongozi anayejiamini na kusimamia anachokiamini lakini asiye jikweza. Lilipotokea swala la zika
na imeingia Tanzania. Ummy alitoa msimamo wa wizara yake na leo tunaona yale maamuzi aliyoyafanya ndio yaliyokuwa sahihi.
Wizaya ya Afya - Mapambano dhidi ya UVIKO19:
Ummy Mwalimu alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake wa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaotokana na virusi vya Corona, kwa jina la kitaalamu COVID -19. Ugonjwa huu uliingia nchini Tanzania tarehe 15 Machi 2020. Ummy aliitisha mkutano na waandishi wa habari nchini kwa weledi mkubwa kabisa alizungumza na taifa kwa lengo la kupunguza taharuki na hofu kwa wananchi.
Ummy alizingatia weledi na kanuni za kukabiliana na majanga, jambo ambalo likiwawezesha Watanzania kuendelea kufanya kazi bila hofu.
TAMISEMI - Mkopo wa UVIKO 19.
Ummy amefanya kazi nzuri kwenye hii wizara kwa muda mfupi sana. Ameoneka akifanya kazi kila kukicha kuhakikisha agizo la raisi dhidi ya pesa za UVIKO 19 linatekelezwa. Amezunguka nchi nzima kuhakikisha ujenzi wa madarasa unafanyika kwa haraka na ufanisi mkubwa.
Vile vile, Ummy Mwalimu ana elimu nzuri ya darasani; UDSM L LB, Pretoria L LM na Oxford University