Ummy Mwalimu ana sifa na anastahili kuwa Waziri Mkuu!

Kwenye ukoo wenu hakuna hata mmoja mwenye akili hata kidogo za kuweza kuwa kiongozi hadi uwe chawa wa wengine?
 
Nikiwa nimekaa hapa nikiota moto, imenijia akilini kuwa maadui wetu wa maendeleo TZ ni watatu tu.

• Uchawa ProMax wa Viongozi na Vijana wa UVCCM
• Kipaumbele Ni kwenye Next Election na sio Next Generation
• Presence of many Clueless Citizens

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si Itakua nchi ya wanwake Sasa hii[emoji848]

Maana ndugai akijiuzulu, Tulia anakua spika.
Kwanza niweke wazi mimi ni mwanaume.

Mwanamke si binadamu kama alivyo mwanaume!
Mbona miaka yote. Raisi ni mwanaume, Makamu wake ni mwanaume na waziri mkuu ni mwanaume.

Makinda alipokuwa Spika alifanya vizuri pia. Na Samia anafanya vizuri!

Tatizo ni lipo wapi wakiwa wanawake?
 
Samia akitaka kujiharibia aweke waziri Mkuu mwanamke atajua hajui atasagiwa kunguni balaa.
 
Shida ya wasomi akili zao sijui zikoje,unajenga madarasa likuki lkn walimu hamuwalipi vzri Sasa kunafaida gan ya kumsifia huyu wazir wenu? Kuna shida ktk hii nchi na watu wake!
 
Bado sijaona alichofanya
Kikatiba ni lazima tuwe na waziri mkuu. Ni tajie ni nani anayefaa kuteuliwa kati ya wabunge tulionao sasa. kama Majaliwa atatolewa?
 
Eti baadhi ya historia ya Ummy mwenye wizara alizoziongoza:

Samahani. No offence.
wewe ni kiazi.
 
Kikatiba ni lazima tuwe na waziri mkuu. Ni tajie ni nani anayefaa kuteuliwa kati ya wabunge tulionao sasa. kama Majaliwa atatolewa?
Muache rais yeye ndiyo anajua nani anamfaa na kufiti positions... Ya nini kupendekeza
 
Kwahiyo Ccm MnagawaNa Vyeo Sasa Hivi
 

Ummy Mwalimu aeleza mafanikio Serikali ya Tanzania kununua dawa kwa wazalishaji​

Thursday July 18 2019​

Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema tangu Serikali ianze kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi kutoka kwa wazalishaji imeokoa asilimia 40 ya fedha zilizokuwa zinatumika kwa mawakala.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema tangu Serikali ianze kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi kutoka kwa wazalishaji imeokoa asilimia 40 ya fedha zilizokuwa zinatumika kwa mawakala.
Akitoa mfano, amesema shuka moja lililokuwa likinunuliwa kwa Sh21,000, hivi sasa linanunuliwa kwa Sh11,200.
Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Julai 18, 2019 katika mkutano wa tatu wa wazalishaji na wasambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi na mkutano wa pili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa ajili ya kuokoa maisha kwa kusambaza huduma hiyo kwa ubora.
Waziri Ummy akieleza hali ilivyokuwa mwaka 2015 amesema, “Ndio tukaanza kununua kutoka kwa wazalishaji badala ya mawakala kwa kuwa na mikataba ya muda mrefu.”
Amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na wawekezaji kuimarisha huduma za dawa nchini na kupunguza gharama kubwa inayotumika kuagiza dawa nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu amesema mkutano huo unawezesha ushirikiano baina yao, wasambazaji na wazalishaji.
Amesema katika mkutano huo kuna wawekezaji na wazalishaji 150 kutoka nje na ndani ya nchi huku mkakati ukiwa kuwekeza katika viwanda vya ndani.
Naye mkurugenzi wa fedha na mipango wa MSD, Soko Mwakalobo amesema kuna viwanja katika Mikoa ya Mbeya, Mwanza na Kibaha kwa ajili ya kuwekeza viwanda vya dawa.

Source: Mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…