Uchaguzi 2020 Ummy Mwalimu atangaza kugombea Ubunge Jimbo la Tanga mjini

Uchaguzi 2020 Ummy Mwalimu atangaza kugombea Ubunge Jimbo la Tanga mjini

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
Waziri wa Afya katika Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi kupitia Rais Magufuli, Ummy Mwalimu wakati akihitimisha kujibu hoja za wabunge wakati wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Afya amesema sasa ameiva na ameamua kuachana na ubunge wa viti maalum na sasa anaenda kugombea ubunge Tanga Mjini.

Ummy Mwalimu amesema anaenda kugombea Ubunge akiwa kifua mbele baada ya kufanya kazi kubwa ya kujenga hospitali za wilaya na Zahanati kila tarafa nchi nzima.

2454640_IMG_20200713_092422_569.jpeg

====

Ummy Ally Mwalimu (alizaliwa 5 Septemba 1973) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama tawala cha kisiasa

Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum vya Wanawake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2015. Akarudishwa tena bungeni

katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia tiketi ya CCM Viti Maalum vya Wanawake 2015.

Mwaka 2017 aliteuliwa kuwa waziri katika Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Elimu na kazi
Ummy Mwalimu alihitimu elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe mwaka 1998.

Alitunukiwa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1998. Mwaka 2001 alitunukiwa shahada ya uzamili ya sheria katika chuo kikuu cha Pretoria. Ummy Mwalimu amefanya kazi sehemu mbalimbali serikalini na katika mashirika yanayojihusisha na tafiti kuhusu sheria, uongozi unaozingatia Sheria na Utawala Bora.

Uzoefu katika siasa
Ummy Mwalimu ameshika nafasi mbalimbali katika ulingo wa siasa. Mwaka 2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na mwaka 2014-2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Mwaka 2015 alikuwa Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, mwaka 2014/5 alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mazingira na mwaka 2010-2014 alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

Pia Ummy Mwalimu amekuwa Mbunge kwa vipindi viwili (2010 hadi 2015 na mwaka 2015 hadi 2020) kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Viti Maalum kwa Wanawake.

Mwaka 2007-2015 Ummy alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga na mwaka 2008 hadi 2015 alikuwa mjumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) Tanga. Mwalimu ameshika nafasi nyingi za uongozi katika chama na serikali.
 
Waziri wa Afya katika serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha Mapinduzi kupitia rais Magufuli ,Ummy Mwalimu wakati akihitimisha kujibu hoja za wabunge wakati wa kupitisha bajeti ya wizara ya afya amesema sasa ameiva na ameamua kuachana na ubunge wa viti maalum na sasa anaenda kugombea ubunge Tanga mjini.

Ummy Mwalimu amesema anaenda kugombea ubunge akiwa kifua mbele baada ya kufanya kazi kubwa ya kujenga hospital za wilaya na Zahanati kila tarafa nchi nzima .

Sent using Jamii Forums mobile app
kashindwa barakoa ndio ataweza ubunge ?
 
Ni jambo la muda tu kama CCM itakupendekeza kusimama kwa tiketi yao!
 
Back
Top Bottom