Ummy Mwalimu na TAMISEMI kwanini makosa haya yanajirudiarudia au ni mradi wa watu?

Ummy kwa pyaya sana tamisemi hafai
Hapana Ummy anajitahidi sana mkuu Kuna mabadiliko makubwa sana. Makosa si mengi sana ingawa sijachambua sana lakini yupo vizuri tumpe muda.
 
Na Jamaa alikuwa na bahati kweli kavuta jiko na ajira ikamfuata. Lakina pia mwaka wa kumaliza chuo ni 2018 na si 2019 Kama ilivyoandikwa.
Hakika Bila koneksheni ajira kupata ni bahati nasibu!
 
Mkuu Kwa issue ya Christina kitu ambacho nimekiona hapo majina matatu yanayofanana namba tofauti za kufanyia mitihani, S2314-0013 na S2314-0014 labda tuamini hawa ni watu wawili tofauti waliosoma shule moja ya sekondari na kusoma digrii ya aina moja au
 
Hii nchi ni kizazi cha nyoka nkuu, system ina madudu mengi. Mwaka jana kuna mwamba anaitwa Abdala Shombe alijitokeza mara 196[emoji15]
 
Mfumo wa uhakiki ni mbovu... au tuseme ni wavivu, wanajaza na kupost bila kuhakiki...
Hakika mkuu na hali hiyo inaleta shida. Inaonesha wameajili 1000 kumbe ni 900 sasa sijui ni ulaji au
 
Hii nchi ni kizazi cha nyoka nkuu, system ina madudu mengi. Mwaka jana kuna mwamba anaitwa Abdala Shombe alijitokeza mara 196[emoji15]
Tutafanya nini mkuu? kuwakumbusha Kama hivi huenda ikasaidia. Maana suala la uwajibikaji inapotokea makosa kwa viongozi wa Afrika haipo!
 
Kuna mtu aliajiriwa 2015 nimeona Tena jina lake hivi juzi[emoji1787][emoji1787]
 
TAMISEMI ya Ummy tarajieni mauzauza. Yeye ni mtu wa porojo,jimbo limemshinda walio muweka wanakulatu hela za umma.
Ummy hapo ataondokatu na ninaamini hivyo
 
MHESHIMIWA WAZIRI SALAM
awali yote nipende kukupongeza kwa Kazi nzito unayoifanya Mheshimiwa Waziri Mungu akupe nguvu na hekima
Mheshimiwa Waziri utakapopata muda Tafadhari naomba upitie tena PDF ya ajira za walimu kuna mambo hayajakaa vizuri kiasi kwamba yamezusha mjadala hususani sisi tuliokosa

Mheshimiwa Waziri
Kuna Mwalimu namba 4115 na Namba 4116 Christina Edward Luhunga Index number S2324-0013/2010 na S2324-0014/2010 Kapangwa Kigoma wilaya Kasulu Dc
Index number S2324-0023 Kapangwa Mayonga Sekondari na
S2324-0014 Kapangwa Nyakitonta Shule ya Sekondari

Mheshimiwa Waziri mwingine ni Mwalimu namba 6571 NICHOLOUS DEUSDEDITH index number S0660-1409/2019 Mwalimu wa Physics na Biology Shida iko hapo kwenye taaluma yake Diploma yake ya ualimu kapata kwa wakati mmoja na Elimu ya Kidato cha Nne ? Na Kama ndiyo hivyo huo mfumo ulianza lini ?

Mheshimiwa Waziri mtu mwingine ni walimu Namba
5919 mwenye index number S4507-0035/2014
Namba 5857 index number S4166-0038/2014
Namba 5798 index number S1183-0035/2014
Namba 5791 index number S4463-0023/2014

Hao ni baadhi tu niliowaona mheshimiwa Hawa walimu ni walimu wa degree kwa Masomo yao
Mheshimiwa shida yangu na Hawa walimu ni kwamba wamemaliza Bachelor degree of education 2019 kitu ambacho siyo ukweli

Kwani walimu Hawa 2015 -2016 ni Kidato cha tano
2016 - 2017 ni Kidato cha sita

CHUO
Mwaka wa kwanza ni
2017- 2018
Mwaka wa pili
2018-2019
Mwaka wa tatu
2019-2020

Maana yake ni kwamba ofisi inatudanganya sisi kuwa Hawa watu wamemaliza Bachelor degree 2019 kitu ambacho siyo ukweli na hakuna Tanzania hii degree ya miaka miwili Mheshimiwa Waziri naomba uliangalie hilo

Kwa mjibu wa professor Karibu mkuu amesema wamechukua mwisho 2019 sasa hao wanatafuta nini ?

Mheshimiwa Waziri naomba hilo suala liangaliwe upya Watu tunakosa fursa kumbe Kuna watu wanapeana tu kindugu

Naomba kuwakilisha

Nategemea feedback mheshimiwa Waziri
 
Ingekua kuna uwajibikaji kama nchi za wenzetu,TAMISEMI ya Ummy na msambaa mwenzake Shemdoe karibu wa wizara wangeshaliwa vichwa.
Alipo Ummy mazingahombwe hayakosekani.
 
Kama una account twiter tuma hii lazima kuna shida mahali
 
Huyu mtu namfahamu na amehitimu 2018 na SI 2019 Kama ilivyoandikwa. Kuhusu kutoripoti na muajiriwa tena hata Kama masomo yanakubeba namna gani bado kunawahitimu wengi wenye masomo husika na hawajaajiriwa. Wewe unaona ni sawa hiyo?
Uliza kwa nini kuna watu wa 2012 wakati miaka hiyo watu wote walikuwa wanaajiriwa?,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…