Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Nenda ukajifunze jinsi ya kuandika na kuhakiki maandishi yako, ndipo uje kuwasilisha mawazo yako.
 
Kachemka tutegemee biashara zaidi matibabu mda wa kazi yatakua hovyo
 
Jamani hii nchi vipi nani ameilaani? Sasa wanajeshi nao baada ya saa za kazi wachukue bunduki zao wakatafute fedha .... Eeh Mungu tusaidie. Jana nilipita duka fulani niliona kibao unga wa sembe shs, 2200 miezi miwili iliyopita tulikuwa tunanunua shs. 700 kwa kilo
 
Daah aisee badala ya kufikiri kuwaboreshea malipo mazuri kwa muda wa ziada wao wanataka majengo tuliyochangia kwa kodi yatumike kama ya mtu binafsi Viongozi huwa hawajui Mali za Umma...hayo maamuzi hata Somalia au DRC sidhani kama wanaweza kuongea hivyo huyu mdada kachemka mno mno aisee...
 
Siasa unaziletea wewe sasa aliyekwambia serikali haifanyi biashara nani? kuna huduma za bure? 24Hrs ni kupokea watu wa dharura tu. Wewe una hiyari ya kuchagua kama unataka huduma za bei nafuu nenda muda wa kazi unataka special treatment nenda kwa muda wako shida iko wapi. Labda nimesema hujui haya Hosp zote zinafanya biashara hutaki kukaa foleni unalipa fast track hata sehemu za kupumzika ziko tofauti ni juu yako unataka nini. Kuna watu wana pesa zao wanataka special treatment ila mtu wa kawaida anapata huduma pia ila anaenda kwa muda wa kazi, huwezi kwenda jioni kumpata Dr labda iwe emergency na utapata Dr wa zamu tu sio bingwa kukupa kama huduma ya kwanza sio zaidi ya hapo.
 
Lipa walimu vizur upate madaktari wengi

Walimu wapatie hiyo amount for ten years tu utakuwa na madaktari wa kutosha
 
Msiwasahau Polisi Jamani. Nao wakimaliza Muda wa malindo waondoke na bunduki wakalinde benki binafsi.
 
Inaonyesha bado sana kwa mwanamke kuwa kiongozi, tumelazimisha tu sasa yanatupata makubwa hii ni aibu
 
Ni mwendo wa kubinafsisha kila kitu, waziri wa Elimu nae atoe maagizo haya kwa walimu.
Walimu wao walishaanza kitambo sana!! Hawakusubiri kibali cha serikali, ni maelewano tu na mkuu wa shule!! Shule inapata 40% ziolizobaki anachukua mwalimu!!
 
Yaani naweza kusema toka nchi ipate uhuru tumewahifanya makosa mengi ila hili la madaktari kufanya kufanya kazi binafsi katika hospitali za umma ni la kiwango cha juu kuyazidi makosa yote.
Majuto ya uamuzi huu yatagharimu damu na uhai wa wengi.
Soon ofisi zote za umma zitaomba kuwa vituo binafsi vya wafanyakazi baada ya mda wao wa kazi.
 
Madhara ya chanjo ya corona haya.wameanza kuwa mazombie
Kwa kweli!! Ina maana sasa hakuna daktari kuwa "on call". Ukimwita akitokea nyumbani hiyo ni private case!! ukimwita usiku hiyo ni private case!!! Hakuna tena kufanya kwa shift!! Ni saa moja na nusu hadi saa tisa na nusu!! Baada ya hapo hospitali ya serikali inabadilika kuwa hospitali ya binafsi!! Mtu akipata ajali jioni saa kumi, akienda hospitali atakuta imeshakuwa ya binafsi!!

Kwa nini tusiseme ni madhara ya chanjo ya corona?? Aliyesema hayo si mtu wa mitaani bali ni waziri wa afya!! Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyo!!
 
Kwa kweli!! Ina maana sasa hakuna daktari kuwa "on call". Ukimwita akitokea nyumbani hiyo ni private case!! ukimwita usiku hiyo ni private case!!! Hakuna tena kufanya kwa shift!! Ni saa moja na nusu hadi saa tisa na nusu!! Baada ya hapo hospitali ya serikali inabadilika kuwa hospitali ya binafsi!! Mtu akipata ajali jioni saa kumi, akienda hospitali atakuta imeshakuwa ya binafsi!!

Kwa nini tusiseme ni madhara ya chanjo ya corona?? Aliyesema hayo si mtu wa mitaani bali ni waziri wa afya!! Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyo!!
 
Tatizo hapa Tz mtu akiwa waziri, wizara anaifanya kama mali yake, anaweza kuamua chochote hata kama ni kituko!! Angalia mifano ifuatayo:

Kuna waziri mmoja wa elimu alilala akaamka siku moja na kupiga marufuku masomo ya kilimo na ufundi mashuleni na ikawa hivyo!!

Mwingine alilala akaamka na kuamuru masomo mawili yaunganishwe liwe somo moja !! somo la Physics with chemistry na ikawa hivyo, na serikali ikaingia gharama ya kugharimia utungaji wa kitabu hicho!!

Ndiyo maana Ndugai alisema siku moja tutajikuta nchi inapigwa bei!! Watu walimbeza lakini tumeyaona kwenye mkataba wa bandari!!

Hivi kweli waziri anaamua tu bila kuwashirikisha watanzania ambao ndio wamikiliki wa hizo hospitali kupitia kodi zao, kufanya maamuzi makubwa yatakayoathiri maslahi ya watanzania kiasi hicho!! Hospitali zetu anaamua kuzifanya za binafsi baada ya muda wa kazi!! Maana yake ni kwamba hata ukiwa kwenye foleni ikifika saa 9.30 jioni utahudumiwa kwa gharama za private!!
 
Nasikia athari za chanjo ya korona huanza hivyo!!
 
Hii serikali inaanguka soon. Dalili zipo wazi kwamba Mungu anawapumbaza.
 
Watanzania ukishawapa go ahead ya aina hiyo ndiyo watafanya hospitali za serikali kuwa za "private" muda wote.
Wakati mwingine naona huwa unagoma kujitoa ufahamu!! Kumbe huwa unajilazimisha tu kujitoa ufahamu wakati una ufahamu mzuri tu!! Naomba nisitoe mfano wa mahali ulipoamua kujitoa ufahamu kabisaa na wewe unapajua mahali hapo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…