Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Serikali ya awamu ya 6 ni kevel nyingi e kwenye maamuxi sahihi kwa maskahi ya umma tumuunge mkono Oddo Ummy hili lidanikiwe, hawa madaktari kila siku wanatuita kwenye vijiwe vyao mida ya jioni, na ni watumishi wa serikali, wanatupima kwenye vijiwe vyao wanaenda kufanya uchunguzi kwenye maabara za Serikali.

Kwa maamuzi bora mengi unayofanya kwenye Sekta ya afya hili nalo lipo kwenye list 👏👏👏👏
Nenda ukajifunze jinsi ya kuandika na kuhakiki maandishi yako, ndipo uje kuwasilisha mawazo yako.
 
Kachemka tutegemee biashara zaidi matibabu mda wa kazi yatakua hovyo
 
Jamani hii nchi vipi nani ameilaani? Sasa wanajeshi nao baada ya saa za kazi wachukue bunduki zao wakatafute fedha .... Eeh Mungu tusaidie. Jana nilipita duka fulani niliona kibao unga wa sembe shs, 2200 miezi miwili iliyopita tulikuwa tunanunua shs. 700 kwa kilo
 
Daah aisee badala ya kufikiri kuwaboreshea malipo mazuri kwa muda wa ziada wao wanataka majengo tuliyochangia kwa kodi yatumike kama ya mtu binafsi Viongozi huwa hawajui Mali za Umma...hayo maamuzi hata Somalia au DRC sidhani kama wanaweza kuongea hivyo huyu mdada kachemka mno mno aisee...
 
Hapo inatofauti gani na kuiendesha hospitali kwa 24hrs isipokuwa jioni umeamua kufanya biashara. Kumbuka serikari haifanyi biashara. Pia private hospital ni pure business. Pia jua, hospitali kuanzia ngazi ya kituo cha afya mpaka juu zinaoperate 24hrs, sio 12hrs. Huwezi kuigeuza usiku kuwa biashara, ni makosa. Pia, mgonjwa kupata consultation tu usiku ni uamuzi wake ila hamna mgonjwa mwenye emergence au urging condition asiyehudumiwa usiku au jioni, laasivyo more than that it can wait, hufi. Acheni siasa!
Siasa unaziletea wewe sasa aliyekwambia serikali haifanyi biashara nani? kuna huduma za bure? 24Hrs ni kupokea watu wa dharura tu. Wewe una hiyari ya kuchagua kama unataka huduma za bei nafuu nenda muda wa kazi unataka special treatment nenda kwa muda wako shida iko wapi. Labda nimesema hujui haya Hosp zote zinafanya biashara hutaki kukaa foleni unalipa fast track hata sehemu za kupumzika ziko tofauti ni juu yako unataka nini. Kuna watu wana pesa zao wanataka special treatment ila mtu wa kawaida anapata huduma pia ila anaenda kwa muda wa kazi, huwezi kwenda jioni kumpata Dr labda iwe emergency na utapata Dr wa zamu tu sio bingwa kukupa kama huduma ya kwanza sio zaidi ya hapo.
 
Pay them well, utilize them to the maximum.

Kama unamlipa Dr net pay ya 10m/month na awepo hospitali 12hrs huku tena unamlipa nurse qualified 4mil netpay kwa mwezi ukamtumia naye 12hrs.

Tuache kutumia hela nyingi kwa wanasiasa baadala yake tulipe watendaji vizuri wawe na ufanisi na tuwatumie vizuri.
Lipa walimu vizur upate madaktari wengi

Walimu wapatie hiyo amount for ten years tu utakuwa na madaktari wa kutosha
 
Msiwasahau Polisi Jamani. Nao wakimaliza Muda wa malindo waondoke na bunduki wakalinde benki binafsi.
 
Inaonyesha bado sana kwa mwanamke kuwa kiongozi, tumelazimisha tu sasa yanatupata makubwa hii ni aibu
 
Ni mwendo wa kubinafsisha kila kitu, waziri wa Elimu nae atoe maagizo haya kwa walimu.
Walimu wao walishaanza kitambo sana!! Hawakusubiri kibali cha serikali, ni maelewano tu na mkuu wa shule!! Shule inapata 40% ziolizobaki anachukua mwalimu!!
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa ruhusa rasmi kwa Madaktari nchini walioajiriwa na serikali kufanya kazi Binafsi kwenye Hospitali za serikali baada ya muda wa kazi kuisha.

Waziri Ummy ametangaza uamuzi huo leo Mkoani Simiyu, wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika ziara yake Mkoani humo.

Waziri Ummy amesema

"Tusiweke urasimu Daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu afanye shughuli zake za Private hapa, atawaona mnakubaliana percentage, Ocean Road nilifanya hivyo. Turuhusu hapa ni kuweka utaratibu tu, kuna Mgonjwa anataka aje wakati hakuna fujo.

Hata mimi kuna watu hawapendi kwenda hospitali za Serikali, mchukulie kama RC yupo busy aanze kupanga mafoleni, anataka akienda sehemu nimekuta chumba maalumu kimetengwa, kina makochi, kuna maji, kuna chai, kuna kahawa, kuna soda.

Daktari atamuita Muuguzi, Daktari atanisikiliza, Muuguzi atanichukua sampuli zangu kama nimeondoka ni kufanyiwa radiology tu lakini vitu vingine nitafanyiwa hapohapo."

Wataalamu wa Afya waonywa kupunguza Semina

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amewataka Wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiogea na Viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”

Waziri Ummy pia amesema katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya Hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la Wataalamu wa Afya ni kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri Wataalamu na sasa ni jukumu letu Wataalau kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”
Yaani naweza kusema toka nchi ipate uhuru tumewahifanya makosa mengi ila hili la madaktari kufanya kufanya kazi binafsi katika hospitali za umma ni la kiwango cha juu kuyazidi makosa yote.
Majuto ya uamuzi huu yatagharimu damu na uhai wa wengi.
Soon ofisi zote za umma zitaomba kuwa vituo binafsi vya wafanyakazi baada ya mda wao wa kazi.
 
Madhara ya chanjo ya corona haya.wameanza kuwa mazombie
Kwa kweli!! Ina maana sasa hakuna daktari kuwa "on call". Ukimwita akitokea nyumbani hiyo ni private case!! ukimwita usiku hiyo ni private case!!! Hakuna tena kufanya kwa shift!! Ni saa moja na nusu hadi saa tisa na nusu!! Baada ya hapo hospitali ya serikali inabadilika kuwa hospitali ya binafsi!! Mtu akipata ajali jioni saa kumi, akienda hospitali atakuta imeshakuwa ya binafsi!!

Kwa nini tusiseme ni madhara ya chanjo ya corona?? Aliyesema hayo si mtu wa mitaani bali ni waziri wa afya!! Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyo!!
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa ruhusa rasmi kwa Madaktari nchini walioajiriwa na serikali kufanya kazi Binafsi kwenye Hospitali za serikali baada ya muda wa kazi kuisha.

Waziri Ummy ametangaza uamuzi huo leo Mkoani Simiyu, wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika ziara yake Mkoani humo.

Waziri Ummy amesema

"Tusiweke urasimu Daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu afanye shughuli zake za Private hapa, atawaona mnakubaliana percentage, Ocean Road nilifanya hivyo. Turuhusu hapa ni kuweka utaratibu tu, kuna Mgonjwa anataka aje wakati hakuna fujo.

Hata mimi kuna watu hawapendi kwenda hospitali za Serikali, mchukulie kama RC yupo busy aanze kupanga mafoleni, anataka akienda sehemu nimekuta chumba maalumu kimetengwa, kina makochi, kuna maji, kuna chai, kuna kahawa, kuna soda.

Daktari atamuita Muuguzi, Daktari atanisikiliza, Muuguzi atanichukua sampuli zangu kama nimeondoka ni kufanyiwa radiology tu lakini vitu vingine nitafanyiwa hapohapo."

Wataalamu wa Afya waonywa kupunguza Semina

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amewataka Wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiogea na Viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”

Waziri Ummy pia amesema katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya Hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la Wataalamu wa Afya ni kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri Wataalamu na sasa ni jukumu letu Wataalau kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”
Kwa kweli!! Ina maana sasa hakuna daktari kuwa "on call". Ukimwita akitokea nyumbani hiyo ni private case!! ukimwita usiku hiyo ni private case!!! Hakuna tena kufanya kwa shift!! Ni saa moja na nusu hadi saa tisa na nusu!! Baada ya hapo hospitali ya serikali inabadilika kuwa hospitali ya binafsi!! Mtu akipata ajali jioni saa kumi, akienda hospitali atakuta imeshakuwa ya binafsi!!

Kwa nini tusiseme ni madhara ya chanjo ya corona?? Aliyesema hayo si mtu wa mitaani bali ni waziri wa afya!! Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyo!!
 
Tatizo hapa Tz mtu akiwa waziri, wizara anaifanya kama mali yake, anaweza kuamua chochote hata kama ni kituko!! Angalia mifano ifuatayo:

Kuna waziri mmoja wa elimu alilala akaamka siku moja na kupiga marufuku masomo ya kilimo na ufundi mashuleni na ikawa hivyo!!

Mwingine alilala akaamka na kuamuru masomo mawili yaunganishwe liwe somo moja !! somo la Physics with chemistry na ikawa hivyo, na serikali ikaingia gharama ya kugharimia utungaji wa kitabu hicho!!

Ndiyo maana Ndugai alisema siku moja tutajikuta nchi inapigwa bei!! Watu walimbeza lakini tumeyaona kwenye mkataba wa bandari!!

Hivi kweli waziri anaamua tu bila kuwashirikisha watanzania ambao ndio wamikiliki wa hizo hospitali kupitia kodi zao, kufanya maamuzi makubwa yatakayoathiri maslahi ya watanzania kiasi hicho!! Hospitali zetu anaamua kuzifanya za binafsi baada ya muda wa kazi!! Maana yake ni kwamba hata ukiwa kwenye foleni ikifika saa 9.30 jioni utahudumiwa kwa gharama za private!!
 
Nimewaza kwa huu utaratibu wa Ummy kwa madaktari ufanyike pia kwa walimu. Wakimaliza muda wa kufundisha wa kawaida waanze kufundisha vipindi vyao vya kawaida. Itakuwa poa sana.

Na askari pia muda wao ukiisha zile bunduki wazitumie kwa namna ambayo wataweza zitumia.

Madereva wa magari ya serikali ukipita muda rasmi wa kazi watumie kwa nafasi zao.

Nimewaza sana logic hii ya ummy. Ana elimu gani huyu dada? Uelewa wake kweli ndo upo hivi.
Nasikia athari za chanjo ya korona huanza hivyo!!
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa ruhusa rasmi kwa Madaktari nchini walioajiriwa na serikali kufanya kazi Binafsi kwenye Hospitali za serikali baada ya muda wa kazi kuisha.

Waziri Ummy ametangaza uamuzi huo leo Mkoani Simiyu, wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika ziara yake Mkoani humo.

Waziri Ummy amesema

"Tusiweke urasimu Daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu afanye shughuli zake za Private hapa, atawaona mnakubaliana percentage, Ocean Road nilifanya hivyo. Turuhusu hapa ni kuweka utaratibu tu, kuna Mgonjwa anataka aje wakati hakuna fujo.

Hata mimi kuna watu hawapendi kwenda hospitali za Serikali, mchukulie kama RC yupo busy aanze kupanga mafoleni, anataka akienda sehemu nimekuta chumba maalumu kimetengwa, kina makochi, kuna maji, kuna chai, kuna kahawa, kuna soda.

Daktari atamuita Muuguzi, Daktari atanisikiliza, Muuguzi atanichukua sampuli zangu kama nimeondoka ni kufanyiwa radiology tu lakini vitu vingine nitafanyiwa hapohapo."

Wataalamu wa Afya waonywa kupunguza Semina

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amewataka Wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiogea na Viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”

Waziri Ummy pia amesema katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya Hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la Wataalamu wa Afya ni kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri Wataalamu na sasa ni jukumu letu Wataalau kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”
Hii serikali inaanguka soon. Dalili zipo wazi kwamba Mungu anawapumbaza.
 
Watanzania ukishawapa go ahead ya aina hiyo ndiyo watafanya hospitali za serikali kuwa za "private" muda wote.
Wakati mwingine naona huwa unagoma kujitoa ufahamu!! Kumbe huwa unajilazimisha tu kujitoa ufahamu wakati una ufahamu mzuri tu!! Naomba nisitoe mfano wa mahali ulipoamua kujitoa ufahamu kabisaa na wewe unapajua mahali hapo!!
 
Back
Top Bottom