Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Hao madaktari wengi wana clinics zao kwenye hospital binafsi baada ya muda wa kazi.

Kuna mgongano mkubwa kuwaruhusu kutumia ofisi hizohizo kutoa huduma binafsi.

Ngoja tuone!
 
Hakuna siku mafuta na maji yaliwahi kuchanganyikana...🤨

Na sio siku nyingi serikali itakuja kujutia uamuzi wake huu...😏

Au kama vipi, Kila mtumishi atumie ofisi ya serikali kujiongezea kipato baada ya muda wa kazi uliopangwa kuisha...😊
Alafu mnawakataza walimu kitumia madalasa ya serikali kitumia kwa muda wa ziada!
 
Hawa Viongozi kutoka ukanda wa pwani ya bahari wanashida gani vichwani mwao? Ajabu sana
 
Ndiyo utajua tofauti ya ummy kama waziri na Dr gwajima kama katibu na wizara yao ya afya na wizara ya ummy kama waziri.
 
Kwa jambo hili SERIKALI yangu haijatafakari kwa kina. Kuna tatizo sana hasa swala la Uzalendo.

Hela imewekwa mbele sana hapa ndio patakua kichaka cha kuwalazimisha wahitaji kulazimika kumuona Dkt private badala ya SAA za kazi.

SERIKALI uenda ikawa na nia nzuri lakini wale wanaotoa huduma wana Uzalendo?

Mfanotu unaandikiwa Dawa unaelekezwa ukanunue pharmacy...... Kwa sababu duka la MSD hawana hizo Dawa hapo ndipo mwenye Akili Ujiongeze.
 
SO kwa SASA Madakatari nao wanaanza kufungua TUITION ZA KITABIBU HOSPITALINI.

Kama hamuwezi kuwalipa,Ingieni na Mkataba wa Kitaalam kama Specialists Muwaache waajiriwe na Sketa Binafsi.
 
Duuh aiseee nimecheka hadi nimeogopa aiseee ! Hivi huyu anafikiri kweli kweli?
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa ruhusa rasmi kwa Madaktari nchini walioajiriwa na serikali kufanya kazi Binafsi kwenye Hospitali za serikali baada ya muda wa kazi kuisha.

Waziri Ummy ametangaza uamuzi huo leo Mkoani Simiyu, wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika ziara yake Mkoani humo.

Waziri Ummy amesema

"Tusiweke urasimu Daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu afanye shughuli zake za Private hapa, atawaona mnakubaliana percentage, Ocean Road nilifanya hivyo. Turuhusu hapa ni kuweka utaratibu tu, kuna Mgonjwa anataka aje wakati hakuna fujo.

Hata mimi kuna watu hawapendi kwenda hospitali za Serikali, mchukulie kama RC yupo busy aanze kupanga mafoleni, anataka akienda sehemu nimekuta chumba maalumu kimetengwa, kina makochi, kuna maji, kuna chai, kuna kahawa, kuna soda.

Daktari atamuita Muuguzi, Daktari atanisikiliza, Muuguzi atanichukua sampuli zangu kama nimeondoka ni kufanyiwa radiology tu lakini vitu vingine nitafanyiwa hapohapo."

Wataalamu wa Afya waonywa kupunguza Semina

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amewataka Wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiogea na Viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”

Waziri Ummy pia amesema katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya Hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la Wataalamu wa Afya ni kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri Wataalamu na sasa ni jukumu letu Wataalau kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”
Alaa kumbee eh sasa na mimi nitatumia madarasa ya shule kufanyia tuition baada ya muda wa kufundisha kwisha.
 
Makosa tayari,wagonjwa wangu ntawambia wanione jioni kwa gharama nafuu,waachane na foleni
Hivi mama umewaza vyema,umetafakari kabla ya kutoa kauli hii?

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo Ummy umeruhusu Tuition hospitalini siyo, basi na sisi waalimu wa shule za msingi na Sekondari mturuhusu tutumie majengo ya shule kufundishia tuisheni.
 
Back
Top Bottom