Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Samia nchi imeshamshinda yaani huyu Mama katupeleka kusikojulikana
 
Na sisi walimu tutaanza kutumia shule za serikali kama private schools baada ya muda wa kazi. Daktari na wagonjwa wake mwalimu na wanafunzi wake.
Si mnatumiaga madarasa baada ya muda wa kazi kufundishia tution
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hatariii tupuu.
20230711_164918.jpg
 
Jambo hili nafikiri lingesubiri kwanza na lisifanyike kabisa katika ofisi na hospitali za umma. Kwa sababu Daktari ameajiliwa na kusaini mkataba wa kutumikia umma wa watanzania kwa muda wote atakaohitajika hospitalini kuhudumia wagonjwa.

Hatua hii na ruhusa hii ya Waziri ni hatari Sana kwa watanzania wanyonge wasio na uwezo wa kumuona daktari kwa muda huo wa ziada. Kwa kuwa hii inaweza kuwafanya madaktari na watumishi wa Afya kugeuza hospitali za umma Kama hospitali binafsi katika koti la hospitali ya umma, pia hatua hii itazolotesha utoaji wa huduma kwa watanzania wanyonge ili kuwalazimisha waje muda wa ziada ambapo gharama lazima ziwe za juu Sana

Watanzania wengi watapoteza maisha kwa kukosa huduma Bora na kukosa hela ya kumuona daktari muda huo ambao dactari atasema Ni wa ziada na anatakiwa alipwe hela kwa makubaliano binafsi,pia hatua hii itawafanya baadhi ya madaktari kupunguza ufanisi muda wa kazi ili wawavute wagonjwa wengi muda wa ziada wanaojuwa watajipatia pesa Yao binafsi.

Hospitali za umma zibaki kuwa hospitali za umma tu na siyo kufanya hivyo,Kama serikali inaona vipato vyao yaani mishahara na stahiki zingine haziwatoshi Basi iwaongezee mishahara zaidi,marupurupu, fedha za over time iwalipe kwa wakati,iboreshe mazingira ya hospitali kwa kuhakikisha vifaa Tiba,Dawa na wahudumu wa Afya wapo wa kutosha ili wasielemewa na mzigo wa kuhudumia wagonjwa.

Tunaweza kufanyia majaribio maeneo mengine lakini katu na kamwe hatupaswi kuleta mzaha Wala majaribio na Afya za watanzania wanyonge, hatupaswi kuweka maisha ya watanzania rehani,hatupaswi kuwatelekeza watanzania kwa kuweka hospitali ndani ya hospitali,mfumo ndani ya mfumo pasipo hata maandalizi ,hili nasema hapana Tena hapana.maisha yetu watanzania nayafahamu Sana na hata Mimi nikiona mzazi wangu anaumwa huwa Namuomba Mungu amponye maana hatuna uwezo wa kugharamia au kubeba gharama kubwa pale tutakapo hitajika kufanya hivyo.

Hospital za umma ziendelee kuboreshwa na kuwaboreshea maslahi watumishi wake ili kuongeza morali ya kazi lakini siyo kwa njia hiyo pendekezwa na mh Waziri ummy mwalimu, nasema jambo hili lisifanyike na pia viongozi wetu wa kisiasa yawapasa kuwa makini katika utoaji wa matamko kwa kuwa mengine yanaweza kuleta athari kubwa Sana hasa kwetu wa kipato Cha chini ambao hatuna uwezo wa kuwaona madaktari huo muda wa ziada.

Unafikiri Ni Daktari yupi ambaye hatapenda kuwekeza muda wa ziada kuhudumia wagonjwa? Unafikiri Daktari yupi ambaye hatawashawishi wagonjwa wake muda wa ziada? Unafikiri daktari atafanya kazi kwa juhudi muda wa kazi Kama ule wa ziada? Sasa Kama tunaruhusu hili kufanyika kulikuwa na kunakuwa na haja gani ya kupiga marufuku maduka ya watu binafsi kuwa karibu na hospitali za umma?

Mimi Nafikiri Kama serikali inalenga kuwaongezea vipato madaktari wetu ambao nami pia nawapenda ,Kuwaheshimu na kuthamini mchago wao Basi ingejikita katika kuwaongezea maslahi yao na kuboresha zaidi mazingira ya kazi.

Namshauri mh Waziri wangu kutengua kauli yake kabla haijaanza kufanyiwa kazi,.Nasema kuwa Afya za watanzania Ni muhimu Sana,sisi uwezo wetu wa kipato Ni mdogo Sana na ndio maana wengi Sana hatuna hata tu bima ya Afya Wala kuwa na uwezo wa kufanya vipimo binafsi vya Afya walau kila mwaka,chonde Sana serikali yangu nawaombeni Sana katika hili kutuonea huruma wanyonge nakutambua kuwa Afya ndio mtaji wetu.
Daktari anafanya saa 8 kwa siku, kwa wiki saa 40! Badala ya kwenda kijiweni baada ya saa tisa na nusu, kuna ubaya gani akianza kula vichwa hapo hospitalini?
 
Kwaleo
Ndonimegundua kwann ,aliibaga vile vitu maduka yamlimacity enzi anasoma chuo
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa ruhusa rasmi kwa Madaktari nchini walioajiriwa na serikali kufanya kazi Binafsi kwenye Hospitali za serikali baada ya muda wa kazi kuisha.

Waziri Ummy ametangaza uamuzi huo leo Mkoani Simiyu, wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika ziara yake Mkoani humo.

Waziri Ummy amesema

"Tusiweke urasimu Daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu afanye shughuli zake za Private hapa, atawaona mnakubaliana percentage, Ocean Road nilifanya hivyo. Turuhusu hapa ni kuweka utaratibu tu, kuna Mgonjwa anataka aje wakati hakuna fujo.

Hata mimi kuna watu hawapendi kwenda hospitali za Serikali, mchukulie kama RC yupo busy aanze kupanga mafoleni, anataka akienda sehemu nimekuta chumba maalumu kimetengwa, kina makochi, kuna maji, kuna chai, kuna kahawa, kuna soda.

Daktari atamuita Muuguzi, Daktari atanisikiliza, Muuguzi atanichukua sampuli zangu kama nimeondoka ni kufanyiwa radiology tu lakini vitu vingine nitafanyiwa hapohapo."

Wataalamu wa Afya waonywa kupunguza Semina

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amewataka Wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiogea na Viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”

Waziri Ummy pia amesema katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya Hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la Wataalamu wa Afya ni kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri Wataalamu na sasa ni jukumu letu Wataalau kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”
Hizi HOJA uchwara, kamwe hazitatutoa kwenye mjadala muhimu juu ya nchi yetu unaohusu bandari.
 
Ambacho hamjaelewa wengi kama si wote ni kwamba hospital ya serikali ni saa 24 huduma, kwahiyo huduma zitendelea kama kawaida,

Aliyeruhusiwa ni daktari, yaani badala ya kuhangaika kwenda private basi aendelee tu hapo hapo, kwahiyo pataekwa mfumo na utaratibu mzuri kwa ajili lengo ni kuhudumia wananchi

Hivi daktari huyo huyo akitoka hapo si anakwenda private za wahindi huko? Si pia anaweza kukushauri umfate huko? Ndio maana ya hili
Acheni mihemko
Hawana mantiki na hii pia haina mantiki kwakuwa daktari hayupo mmoja kwenye hospitali labda vituo vya afya na zahanati. Akitoka huyu anaingia huyu, hakukosekagi daktari. Pili, kumuachia daktari aendeshe shughuli za private kwenye hospitali ya umma unaiingizia hasara serikari maana vifaa na dawa utakazotumia ni za hospitali sio za kwako. Private hospital zinaendeshwa kwa mlengo wa biashara ila sio za serikari, ukianza kuintroduce concept ya biashara kwenye serikari basi serikari iikatae katiba yake. Ila la kuwataka wabaki sijui extra time ni concept ya human resorces hivyo ni upuuzi wao wa kutoajiri madaktari wakutosha, wanaajiri halafu wakishawaweka vituoni wanawasahau kabisa hivyo watumishi wengi huendelea na mishe zao za kuongeza pesa maana hata pesa ya kujikimu kwa hawa wapya umesikia wengine hawajapewa. Mishahara kuwaongezea hamtaki, solution ndio mkaamua kuidefy katiba kabisa. Hii serikari ya ajabu balaa. Wanaspend millions kwa mwanasiasa ila sio wataalamu. Yaani alichokifanya haipo justifiable hata kidogo. Kwaujumla, hii ni serikari ya wazembe kuwahi tokea.
 
Walikuwa hawafanyi kwa kuibia haya mambo yalikuwa wazi na kihalali kabisa. Ilikuwa unaenda kumuona Dr Hosp na anakuhudumia sio kwamba anafanya uzembe unapata huduma kama zote ila inajulikana baada ya kazi huyo huyo Dr ana clinic yake nje na anahudumia. Mimi binafsi sijawahi kuhudumiwa tofauti japo ukiwa Hosp ya serikali process zake ni tofauti. Lakini hata hizi Hosp za serikali ziko huduma za fast track ukitaka kuonana na Dr bingwa express bila foleni unalipa tu hutaki unapiga foleni haya mambo yapo kila siku.

Waziri nia yake ni nzuri kwamba hawa ma Dr nje ya kazi badala ya mfano kwenda kulipia xray nje wanaweza kutumia za Hosp na wakalipia mimi sidhani kama ni issue kubwa sababu tayari haya mambo yapo Hosp zote kubwa za serikali.
Hapo inatofauti gani na kuiendesha hospitali kwa 24hrs isipokuwa jioni umeamua kufanya biashara. Kumbuka serikari haifanyi biashara. Pia private hospital ni pure business. Pia jua, hospitali kuanzia ngazi ya kituo cha afya mpaka juu zinaoperate 24hrs, sio 12hrs. Huwezi kuigeuza usiku kuwa biashara, ni makosa. Pia, mgonjwa kupata consultation tu usiku ni uamuzi wake ila hamna mgonjwa mwenye emergence au urging condition asiyehudumiwa usiku au jioni, laasivyo more than that it can wait, hufi. Acheni siasa!
 
Huu usengeh wa hali ya juu sana! Nchi imevaa dera sasa hivi.
 
Aliyeleta Mada ndio kaleta mvurugano.

Nilivyoelewa ni kwamba Madaktari wamepewa ruhusa kufanya Part time jobs ktk hospitali binafsi. Na sio kutumia hospital za umma kugeuza binafsi baada ya masaa ya kazi.
 
Uwwwwiiii.....🙆‍♂️
Tumekwisha.....😭

Yaani ameamua kuwapa rungu kabisa...... ili waanze kufanya ucheleweshaji wa makusudi ili wajipatie kipato cha lazima baada ya muda wa kazi....🤔
Hili ni pigo kwenye sector ya afya, Sasa tutegemee wagonjwa kucheleweshwa makusudikally ili madokta na wauguzi wajipigie hela zao binafsi. Mtanzania akipewa nafasi anajua kuitumia effectively kwaajili ya kujineemesha. Tusubiri tuone
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa ruhusa rasmi kwa Madaktari nchini walioajiriwa na serikali kufanya kazi Binafsi kwenye Hospitali za serikali baada ya muda wa kazi kuisha.

Waziri Ummy ametangaza uamuzi huo leo Mkoani Simiyu, wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika ziara yake Mkoani humo.

Waziri Ummy amesema

"Tusiweke urasimu Daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu afanye shughuli zake za Private hapa, atawaona mnakubaliana percentage, Ocean Road nilifanya hivyo. Turuhusu hapa ni kuweka utaratibu tu, kuna Mgonjwa anataka aje wakati hakuna fujo.

Hata mimi kuna watu hawapendi kwenda hospitali za Serikali, mchukulie kama RC yupo busy aanze kupanga mafoleni, anataka akienda sehemu nimekuta chumba maalumu kimetengwa, kina makochi, kuna maji, kuna chai, kuna kahawa, kuna soda.

Daktari atamuita Muuguzi, Daktari atanisikiliza, Muuguzi atanichukua sampuli zangu kama nimeondoka ni kufanyiwa radiology tu lakini vitu vingine nitafanyiwa hapohapo."

Wataalamu wa Afya waonywa kupunguza Semina

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amewataka Wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiogea na Viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”

Waziri Ummy pia amesema katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya Hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la Wataalamu wa Afya ni kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri Wataalamu na sasa ni jukumu letu Wataalau kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”
Haya ndio matatizo ya kuwa na viongizi wamama.. hawapendi shida, shortcut kila kitu..
 
Uamuzi mbovu wenye unintended consequences nyingi sana
 
Back
Top Bottom