Ummy Mwalimu: Tozo ya uzalendo ni ubunifu, tunajenga barabara vijijini

Ummy Mwalimu: Tozo ya uzalendo ni ubunifu, tunajenga barabara vijijini

The Saver

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2014
Posts
202
Reaction score
651
Hii nchi haina uongozi aiseee

Tumepigwa

Mama anaupiga mwingii

=====

Tozo mpya iliyoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Sita kupitia mitandao ya simu na mafuta katika vyombo vya usafiri, zinaenda kuwanufaisha wananchi wa vijijini kwa kufungua mtandao wa barabara vijijini.

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi Rais Tamisemi (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Santa Maria - Kabage yenye urefu wa kilomita 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tnganyika Mkoani Katavi.

“Nadhani Mlitusikia Mimi na Waziri wa Fedha kuwa ni jinsi gani fedha hizi za tozo ya mitandao ya simu na mafuta zinaenda kufungua barabara vijijini. Mmemsikia Mbunge wenu kuwa hii barabara haikuwa inapitika kutoka kijiji cha Santa Maria hadi Kijiji cha Kabage ambako ni muhimu kwa uzalishaji mkubwa wa chakula hasa maza ya mpunga, lakini sasa imefunguka, “alisema Ummy.

Alieleza kuwa Serikali iliamua kufanya ubunifu baada ya kujuliza ni jinsi gani wataboresha barabara za vijijini, hivyo kubuni chanzo hicho cha tozo za simu na mafuta ambacho sasa kinaleta matokeo chanya yanayoonekana.

“Mmemsikia meneja wa Tarura Tanganyika kwamba alikuwa na bajeti ya shilingi milioni 150 tu kwa wilaya nzima ya Tanganyika, lakini sasa kwa sababu ya tozo hii mpya,bajeti yake ya maendeleo ya ujenzi wa barabara inaenda kuongezeka mpaka shilingi bilioni moja na milioni mia tano (1.5 bilioni), “alisema Ummy.

Alisema kuwa kama milioni 150 zimeweza kujenga Km 16 za barabara ni wazi kwa bilioni 1.5 zitaenda kufungua barabara nyingi sana vijijini na kuondoa kero ya muda mrefu kwa wananchi.

Aliwataka watanzania kuendelea kuchangia tozo hiyo ambayo inaenda kuleta ukombozi mkubwa vijijini.

Chanzo: Clouds TV
 
Cool!!

Waache sasa upumbavu wa kuzunguka kutwa kucha Dodoma-dar Dodoma-dar wanachoma mafuta ya kodi za uzalendo

Kama budget 75% ingekuwa inatumika kwenye maendeleo Mimi sioni tatizo la kulipa kodi

Ila tatizo wanatumia pesa kufanya anasa sana hawa mawaziri na Rais wao.
 
1626335304995.png
 
Tatizo Chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya Watanzania yanatekelezeka!

Yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, Watanzania wanajiuliza nia ya Chadema ni nn haswa?

Kwanini wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
 
Kodi hii imepitishwa na BUNGE letu tukufu, wabunge walio chaguliwa kihalali ambao wamewakilisha mawazo ya watanzania wote kwa manufaa ya watanzania wote, kodi hii lazima tuilipe, wapuuzi wachache wasitusumbue wala wasituharibie malengo yetu kama hawataki waende wakaishi Ubeligiji.
 
Cool!!

Waache sasa upumbavu wa kuzunguka kutwa kucha Dodoma-dar Dodoma-dar wanachoma mafuta ya kodi za uzalendo

Kama budget 75% ingekuwa inatumika kwenye maendeleo Mimi sioni tatizo la kulipa kodi

Ila tatizo wanatumia pesa kufanya anasa sana hawa mawaziri na Rais wao.
Waanze wao kwa kutonyesha uzalendo kwa kubana matumizi. Waanze kutumia PASO badala ya V8 hizo, watokekwenye nyumba wanazolipiwa kodi za gharama na serikali na mishahara yao ipungue angalau hata 25% ili pesa ije kwenye hiyo miradi ya kizalendo. wakifanya hivyo hata sisi tutalipa kodi bila manung"uniko. Wanatuambia uzalendo huku wao wanazidi kula kiyoyozi na semina kibao zisizo na kichwa wala miguu za kula perdiem hatutakubali
 
Hii nchi haina uongozi aiseee

Tumepigwa

Mama anaupiga mwingiiView attachment 1854505
Yaani huyu mama muimba tarabu anampa wizara ya TAMISEMI kweli Samia yuko serious? Yaani ni mswahili tu hana la maana na kazi yake ni kuongea sana, Pia tatizo la mama anadhani kubalance jinsia ndo suluhisho. Ukiangalia hata Marekani mawaziri wanawake ni wachache lakini sisi waafrika tunataka kubalance bila kuangalia ufanisi.

Nashauri mama ajikite kuweka watu wenye weredi na uwezo wa kufanya maamzi sahihi sio watu wa kutwa kubweka huku matokeo hamna kama huyu na Mwigulu Nchemba.
 
Toxin za mwendazake hazina weledi wowote hakuchagua watu smart alichagua watu atawaendesha kama rimoti na sio wanaoleta tija kwa wananchi.

Hakuna tozo kama hizi duniani kote
 
Toxin za mwendazake hazina weledi wowote hakuchagua watu smart alichagua watu atawaendesha kama rimoti na sio wanaoleta tija kwa wananchi.
Hakuna tozo kama hizi duniani kote
Mzimu bado unakuchapa mbele na nyuma.
 
Tatizo chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya watanzania yanatekelezeka!!!
yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, watanzania wanajiuliza nia ya chadema ni nn haswa?
kwa nn wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
We Ni mjinga sana
 
Back
Top Bottom