Ummy Mwalimu: Tozo ya uzalendo ni ubunifu, tunajenga barabara vijijini

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi Rais Tamisemi (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Santa Maria - Kabage yenye urefu wa kilomita 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tnganyika Mkoani Katavi.
Ummy nilikuona una focus lakini kwa haya maneno yako naanza kukuogopa huenda si wewe niliyekupa credit
 
Kwa hiyo hakuna vyanzo vingine vya mapato visivyoumiza wananchi wanyonge?
 
Cool!!

Waache sasa upumbavu wa kuzunguka kutwa kucha Dodoma-dar Dodoma-dar wanachoma mafuta ya kodi za uzalendo

Kama budget 75% ingekuwa inatumika kwenye maendeleo Mimi sioni tatizo la kulipa kodi

Ila tatizo wanatumia pesa kufanya anasa sana hawa mawaziri na Rais wao.
Yaani hapo watapandishiana mpka posho zao
 
Hii nchi haina uongozi aiseee

Tumepigwa

Mama anaupiga mwingii

=====

Tozo mpya iliyoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Sita kupitia mitandao ya simu na mafuta katika vyombo vya usafiri, zinaenda kuwanufaisha wananchi wa vijijini kwa kufungua mtandao wa barabara vijijini.

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi Rais Tamisemi (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Santa Maria - Kabage yenye urefu wa kilomita 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tnganyika Mkoani Katavi.

“Nadhani Mlitusikia Mimi na Waziri wa Fedha kuwa ni jinsi gani fedha hizi za tozo ya mitandao ya simu na mafuta zinaenda kufungua barabara vijijini. Mmemsikia Mbunge wenu kuwa hii barabara haikuwa inapitika kutoka kijiji cha Santa Maria hadi Kijiji cha Kabage ambako ni muhimu kwa uzalishaji mkubwa wa chakula hasa maza ya mpunga, lakini sasa imefunguka, “alisema Ummy.

Alieleza kuwa Serikali iliamua kufanya ubunifu baada ya kujuliza ni jinsi gani wataboresha barabara za vijijini, hivyo kubuni chanzo hicho cha tozo za simu na mafuta ambacho sasa kinaleta matokeo chanya yanayoonekana.

“Mmemsikia meneja wa Tarura Tanganyika kwamba alikuwa na bajeti ya shilingi milioni 150 tu kwa wilaya nzima ya Tanganyika, lakini sasa kwa sababu ya tozo hii mpya,bajeti yake ya maendeleo ya ujenzi wa barabara inaenda kuongezeka mpaka shilingi bilioni moja na milioni mia tano (1.5 bilioni), “alisema Ummy.

Alisema kuwa kama milioni 150 zimeweza kujenga Km 16 za barabara ni wazi kwa bilioni 1.5 zitaenda kufungua barabara nyingi sana vijijini na kuondoa kero ya muda mrefu kwa wananchi.

Aliwataka watanzania kuendelea kuchangia tozo hiyo ambayo inaenda kuleta ukombozi mkubwa vijijini.

Chanzo: Clouds TV
Huyo mgosi shida nae ni tarumbeta kma domo lake
 
Kweli kabisa Ummy ongezeni kodi maradufu tunataka vifurushi vya kodi yaani unalipia mfano kifurushi cha uzalendo plus au uzalendo premium unakuwa unaongeza makato zaidi ukitumia simu....acheni tuijenge nchi yetu nyie🤣
 
Tatizo Chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya Watanzania yanatekelezeka!

Yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, Watanzania wanajiuliza nia ya Chadema ni nn haswa?

Kwanini wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
we jamaa nadhani kichwani kuna funza howcomes Chadema wamepinga wakati swala ili linaumiza kila mtu kuanzia mwenye kipato cha chini mpaka cha juuu wakati mwingine ni bora utoe mawazo yako bila kuweka bias ya chama
 
Punguzeni Mishahara na Punguzeni Safari na Magari ya ANASA ACHENI KUWAUMIZA WANANCHI KWA KODI ZA AJABU
Kuna zile Suzuki Jimny new model za halmashauri zile wangenunuliwa Wabunge wote watumie zile kwanza ni 4x4 halafu imara sana zingewafaa sana wazalendo wenzetu wa Mjengoni!😅

Pili posho zipigwe panga nazo some percent iende kwenye solidarity funds! Mishahara pia walipe PAYE na VAT kama watumishi wengine tu! Kinachobaki kifyekwe by 10% kiende kwenye mfuko wa mshikamano!

Zile zikiongozana 10 ni sawa na Mafuta ya VX 2 tu!
 
Pumbavu kabisa kwanini huo ubunifu usianzie bungeni kwenye marupurupu yao Kisha uende kwenye Baraza la mawaziri...

Wanasiasa Wengi wa ki Afrika wana upungufu wa Akili kichwani.
Halafu ni uzalendo kwa wenye simu tu? Rubbish statement ever.
 
Hii nchi haina uongozi aiseee

Tumepigwa

Mama anaupiga mwingii

=====

Tozo mpya iliyoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Sita kupitia mitandao ya simu na mafuta katika vyombo vya usafiri, zinaenda kuwanufaisha wananchi wa vijijini kwa kufungua mtandao wa barabara vijijini.

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi Rais Tamisemi (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Santa Maria - Kabage yenye urefu wa kilomita 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tnganyika Mkoani Katavi.

“Nadhani Mlitusikia Mimi na Waziri wa Fedha kuwa ni jinsi gani fedha hizi za tozo ya mitandao ya simu na mafuta zinaenda kufungua barabara vijijini. Mmemsikia Mbunge wenu kuwa hii barabara haikuwa inapitika kutoka kijiji cha Santa Maria hadi Kijiji cha Kabage ambako ni muhimu kwa uzalishaji mkubwa wa chakula hasa maza ya mpunga, lakini sasa imefunguka, “alisema Ummy.

Alieleza kuwa Serikali iliamua kufanya ubunifu baada ya kujuliza ni jinsi gani wataboresha barabara za vijijini, hivyo kubuni chanzo hicho cha tozo za simu na mafuta ambacho sasa kinaleta matokeo chanya yanayoonekana.

“Mmemsikia meneja wa Tarura Tanganyika kwamba alikuwa na bajeti ya shilingi milioni 150 tu kwa wilaya nzima ya Tanganyika, lakini sasa kwa sababu ya tozo hii mpya,bajeti yake ya maendeleo ya ujenzi wa barabara inaenda kuongezeka mpaka shilingi bilioni moja na milioni mia tano (1.5 bilioni), “alisema Ummy.

Alisema kuwa kama milioni 150 zimeweza kujenga Km 16 za barabara ni wazi kwa bilioni 1.5 zitaenda kufungua barabara nyingi sana vijijini na kuondoa kero ya muda mrefu kwa wananchi.

Aliwataka watanzania kuendelea kuchangia tozo hiyo ambayo inaenda kuleta ukombozi mkubwa vijijini.

Chanzo: Clouds TNT
Ubunifu ni kuumiza wananchi kwa tozo kubwa? Ngoja na sisi tuwe na tozo ya ubunifu 2025.
 
Tatizo Chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya Watanzania yanatekelezeka!

Yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, Watanzania wanajiuliza nia ya Chadema ni nn haswa?

Kwanini wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?

20210709_122837.jpg
 
Mh,upigaji umeanza mapema?!!mi nilijua hizo tozo zitasaidia barabara za vijijini kuwekwa lami kumbe ni kuchonga na kuzifanya zipitike tuuu!!!mbona tozo zilizowekwa ni kubwa mnoo?!
 
kodi hii lazima tuilipe
Inawezekana ukawa na hoja nzuri, lakini ni kukumbushe tu kuwa kodi hii ni tozo la kufanya miamala ya tukutuma pesa kwa njia ya simu, so Ulazima wa kulipa inategemea na utumiaji wa huduma hiyo.....kuna watakao amua kuacha kutumia huduma hizo...Pia kuna watakao amua kupunguza uwezo wao wa ku recharge vifurushi kwenye simu zao, mfano mtu alikuwa ana recharge 5000 kwa siku anaweza kurudi kwenye buku kwa siku ili akatwe tshs 5 tu.....hapo inaweza ikawa imekula kwetu!
 
Tatizo Chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya Watanzania yanatekelezeka!

Yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, Watanzania wanajiuliza nia ya Chadema ni nn haswa?

Kwanini wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
Sikiliza hoja zao acha mihemko ya kichama wewe, hakuna mpinzan ambae anapinga maendeleo. Hua wanahoja zao jinsi gan ya kufanya jambo fulani
 
Lengo la hizi tozo ni kuuwa ajira na uchumi, badala ya kuchochea export wamekalia matozo.Bidhaa moja kodi mara 4 uliona nchi gani duniani wanafanya hivi
 
Nimeshaongea sana kuwa wanaoturudisha nyuma nchi hii ni wabunge. Hiki cheo hakina maana zaidi ya kutuletea matabaka.

Bunge lisiwepo. Hata hao wanaopigania Katiba mpya, hawajabeba ajenda ya kitaifa zaidi ya kutafuta upenyo wa kwenda bungeni kuendelea kuwanyonya watanzania.

Tunaweza kuendelea kuwa na mabaraza ya madiwani yanatosha kabisa. Pia kukawa na Baraza kuu la madiwani lenye uwakilishi wa madiwani wawili au watatu kila mkoa kwa ajili ya kuishauri serikali na kutunga sheria.

Wabunge ndio maadui wa maendeleo ya Tanzania. Tuanze kupunguza hizi takataka ndio tuhimize Katiba mpya
 
Hii nchi haina uongozi aiseee

Tumepigwa

Mama anaupiga mwingii

=====

Tozo mpya iliyoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Sita kupitia mitandao ya simu na mafuta katika vyombo vya usafiri, zinaenda kuwanufaisha wananchi wa vijijini kwa kufungua mtandao wa barabara vijijini.

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi Rais Tamisemi (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Santa Maria - Kabage yenye urefu wa kilomita 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tnganyika Mkoani Katavi.

“Nadhani Mlitusikia Mimi na Waziri wa Fedha kuwa ni jinsi gani fedha hizi za tozo ya mitandao ya simu na mafuta zinaenda kufungua barabara vijijini. Mmemsikia Mbunge wenu kuwa hii barabara haikuwa inapitika kutoka kijiji cha Santa Maria hadi Kijiji cha Kabage ambako ni muhimu kwa uzalishaji mkubwa wa chakula hasa maza ya mpunga, lakini sasa imefunguka, “alisema Ummy.

Alieleza kuwa Serikali iliamua kufanya ubunifu baada ya kujuliza ni jinsi gani wataboresha barabara za vijijini, hivyo kubuni chanzo hicho cha tozo za simu na mafuta ambacho sasa kinaleta matokeo chanya yanayoonekana.

“Mmemsikia meneja wa Tarura Tanganyika kwamba alikuwa na bajeti ya shilingi milioni 150 tu kwa wilaya nzima ya Tanganyika, lakini sasa kwa sababu ya tozo hii mpya,bajeti yake ya maendeleo ya ujenzi wa barabara inaenda kuongezeka mpaka shilingi bilioni moja na milioni mia tano (1.5 bilioni), “alisema Ummy.

Alisema kuwa kama milioni 150 zimeweza kujenga Km 16 za barabara ni wazi kwa bilioni 1.5 zitaenda kufungua barabara nyingi sana vijijini na kuondoa kero ya muda mrefu kwa wananchi.

Aliwataka watanzania kuendelea kuchangia tozo hiyo ambayo inaenda kuleta ukombozi mkubwa vijijini.

Chanzo: Clouds TV
Na wao kama wabunge wachangie 10% ya mishahara yao kama kuonyesha uzalendo na kuunga mkono juhudi za kutengenezwa barabara za vijijini kwa wapiga kura wao.
 
Back
Top Bottom