Ummy Mwalimu: Tozo ya uzalendo ni ubunifu, tunajenga barabara vijijini

Ummy Mwalimu: Tozo ya uzalendo ni ubunifu, tunajenga barabara vijijini

kodi hii imepitishwa na BUNGE letu tukufu, wabunge walio chaguliwa kihalali ambao wamewakilisha mawazo ya watanzania wote kwa manufaa ya watanzania wote, kodi hii lazima tuilipe, wapuuzi wachache wasitusumbue wala wasituharibie malengo yetu kama hawataki waende wakaishi ubeligiji.
Una bahati sitaki tu ban
 
Hayo ma v8 ni mzigo na hayana tija zaidi ya kutafunia kodi zetu na kupelekea watoto wao international school
 
Kweli kuna haja gani kuwa na ikulu mbili? Mama asubuhi yupo Dodoma jioni anakwea pipa kurudi Dar kwa mumewe. Ndani ya wiki akizunguka mara 5 ni mabilioni mangapi yanapotea. Hapo bado hujaweka mizunguko ya VP, PM na Mawaziri na wasaidizi wao. Wanatuua hawa.
Cool!!

Waache sasa upumbavu wa kuzunguka kutwa kucha Dodoma-dar Dodoma-dar wanachoma mafuta ya kodi za uzalendo

Kama budget 75% ingekuwa inatumika kwenye maendeleo Mimi sioni tatizo la kulipa kodi

Ila tatizo wanatumia pesa kufanya anasa sana hawa mawaziri na Rais wao.
 
Tatizo chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya watanzania yanatekelezeka!!!
yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, watanzania wanajiuliza nia ya chadema ni nn haswa?
kwa nn wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
Hayo maendeleo tuyasubirie miaka mingapi aseeeee?
 
Tatizo chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya watanzania yanatekelezeka!!!
yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, watanzania wanajiuliza nia ya chadema ni nn haswa?
kwa nn wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
Tangu ccm iyanze kutawala kodi walikua hawatozi??

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Yani hawa viongozi wetu hawa 🤣🤣🤨.. ....Tumewa-empower kiasi cha kwamb anakua na guts ya kutoka na kutoa kauli kama hii ya kukuongezea maumivu...naomba wakuu wa JF siku nyingine mambo kama haya yakitokea tuweke kwanza utaifa tuachane na vitu vidogo vidogo,hili suala halikupigiwa sana kelele humu kuliko lile la mabando... We engage in polemics zinazohusu vitu vya kupita pita na often zinaishia kua mada za pro/against mtu yule.watu tumekua very reactive baadala ya kua proactive. Nasikitika sababu kuna wenye akili kunizidi mm walinivutia Sana JF siku za nyuma ,siku hizi wamekua watu wa chuki tu,they offer no insights at all.
 
Tatizo chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya watanzania yanatekelezeka!!!
yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, watanzania wanajiuliza nia ya chadema ni nn haswa?
kwa nn wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
Si kila anayehoji ni chadema. Ni muhimu haya maoni kwa ajili ya tafakuri.
Hizi tozo zikizidi ni sawa na kumkamua ng'ombe maziwa mengi hata kama ndama atadhoofika ili mradi unataka uuze upate pesa uwajengee kibanda kizuri.

Mama na ndama watadhoofika na maziwa hayatatosha na pesa haitazidi na kibanda hakitajengwa.
 
Kodi ya uzalendo kwa Sheria ipi?

Huu ni uporaji Kama uporaji mwingine ule

Hao wezi siku zao hazitatimia 40
 
Inaonyesha roads za village hazikuwa na fungi lake Kama hizi za mjini so walikuwa wanazibagua ama ni nini
 
Hivi hata haya maoni yanayotolewa kwenye mitandao wanayaona kweli??
 
Hii nchi haina uongozi aiseee

Tumepigwa

Mama anaupiga mwingii

=====

Tozo mpya iliyoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Sita kupitia mitandao ya simu na mafuta katika vyombo vya usafiri, zinaenda kuwanufaisha wananchi wa vijijini kwa kufungua mtandao wa barabara vijijini.

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi Rais Tamisemi (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Santa Maria - Kabage yenye urefu wa kilomita 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tnganyika Mkoani Katavi.

“Nadhani Mlitusikia Mimi na Waziri wa Fedha kuwa ni jinsi gani fedha hizi za tozo ya mitandao ya simu na mafuta zinaenda kufungua barabara vijijini. Mmemsikia Mbunge wenu kuwa hii barabara haikuwa inapitika kutoka kijiji cha Santa Maria hadi Kijiji cha Kabage ambako ni muhimu kwa uzalishaji mkubwa wa chakula hasa maza ya mpunga, lakini sasa imefunguka, “alisema Ummy.

Alieleza kuwa Serikali iliamua kufanya ubunifu baada ya kujuliza ni jinsi gani wataboresha barabara za vijijini, hivyo kubuni chanzo hicho cha tozo za simu na mafuta ambacho sasa kinaleta matokeo chanya yanayoonekana.

“Mmemsikia meneja wa Tarura Tanganyika kwamba alikuwa na bajeti ya shilingi milioni 150 tu kwa wilaya nzima ya Tanganyika, lakini sasa kwa sababu ya tozo hii mpya,bajeti yake ya maendeleo ya ujenzi wa barabara inaenda kuongezeka mpaka shilingi bilioni moja na milioni mia tano (1.5 bilioni), “alisema Ummy.

Alisema kuwa kama milioni 150 zimeweza kujenga Km 16 za barabara ni wazi kwa bilioni 1.5 zitaenda kufungua barabara nyingi sana vijijini na kuondoa kero ya muda mrefu kwa wananchi.

Aliwataka watanzania kuendelea kuchangia tozo hiyo ambayo inaenda kuleta ukombozi mkubwa vijijini.

Chanzo: Clouds TV
Uzalendo uanze na yeye wabunge wakatwe Kodi.
 
Barabara ya Mombasa, moshi bar,kwa mkolemba, kanyigo mwembeni, fremu kumi hadi njia pandaya msongola ni kero ya muda mrefu. Vyombo vya usafiri wa moto bajaji, pikipiki na magari vinapata changamoto kwa hii njia mbovu sana! Sijui kama Jerry (mb)ameikumbuka hii njia katika 1.5 bilioni ambazomama yetu amesikia kilio chetu.

Uzuri siku hizi tunafatilia maana siku hizi tunasikiliza na kuweka kumbukumbu na mama amejipambanua vizuri kuwa fedha hizi zielekezwe kwenye kufanya matengenezo ya njia za vijijini/mtaani.
 
Si kila anayehoji ni chadema. Ni muhimu haya maoni kwa ajili ya tafakuri.
Hizi tozo zikizidi ni sawa na kumkamua ng'ombe maziwa mengi hata kama ndama atadhoofika ili mradi unataka uuze upate pesa uwajengee kibanda kizuri.

Mama na ndama watadhoofika na maziwa hayatatosha na pesa haitazidi na kibanda hakitajengwa.
kwa hiyo unapenda vya buree eeehh!!!
unataka usadiwe na mataifa ya ulaya eeeh!!!
kumbuka pia misaada tunayo ipata kutoka nchi za ulaya ni KODI ZA WANANCHI WA MAREKANI, UGERUMANI, DENMARK, NEWZELAND, FRANCE, CHINA, UINGEREZA N.K, wananchi wazalendo wa nchi hizo wanatozwa kodi ambazo zingine ndio tunapewa ss misaada na wakati mwengine tunakopeshwa.
acheni kuwa walemavu wa akili lipeni kodi ili itusaidie maendeleo yetu.
Taifa imara itajengwa na sisi watanzania wenyewe kwa kulipa kodi sio kutegemea misaada au mikopo.
 
Back
Top Bottom