ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Una bahati sitaki tu bankodi hii imepitishwa na BUNGE letu tukufu, wabunge walio chaguliwa kihalali ambao wamewakilisha mawazo ya watanzania wote kwa manufaa ya watanzania wote, kodi hii lazima tuilipe, wapuuzi wachache wasitusumbue wala wasituharibie malengo yetu kama hawataki waende wakaishi ubeligiji.
Uoni tozo za ajabu kabisa hizoMzimu bado unakuchapa mbele na nyuma...
Cool!!
Waache sasa upumbavu wa kuzunguka kutwa kucha Dodoma-dar Dodoma-dar wanachoma mafuta ya kodi za uzalendo
Kama budget 75% ingekuwa inatumika kwenye maendeleo Mimi sioni tatizo la kulipa kodi
Ila tatizo wanatumia pesa kufanya anasa sana hawa mawaziri na Rais wao.
Hayo maendeleo tuyasubirie miaka mingapi aseeeee?Tatizo chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya watanzania yanatekelezeka!!!
yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, watanzania wanajiuliza nia ya chadema ni nn haswa?
kwa nn wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
Sio za Magu.....Uoni tozo za ajabu kabisa hizo
Zimeharibu toxin za jiweSio za Magu.....
deal na mama ambae yupo....
maza akifanya vizuri mnamsifu...
akiharibu Magu....!!? kumbaf kabisa
Tangu ccm iyanze kutawala kodi walikua hawatozi??Tatizo chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya watanzania yanatekelezeka!!!
yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, watanzania wanajiuliza nia ya chadema ni nn haswa?
kwa nn wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
Si kila anayehoji ni chadema. Ni muhimu haya maoni kwa ajili ya tafakuri.Tatizo chadema sikuzote hawapendi kuona maendeleo ya watanzania yanatekelezeka!!!
yaaani wao wanapenda kuona watanzania wanakosa madawa hospitalini, wanakosa barabara, wanakosa elimu n.k, watanzania wanajiuliza nia ya chadema ni nn haswa?
kwa nn wanapinga watanzania kuchangia maendeleo yao?
Uzalendo uanze na yeye wabunge wakatwe Kodi.Hii nchi haina uongozi aiseee
Tumepigwa
Mama anaupiga mwingii
=====
Tozo mpya iliyoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Sita kupitia mitandao ya simu na mafuta katika vyombo vya usafiri, zinaenda kuwanufaisha wananchi wa vijijini kwa kufungua mtandao wa barabara vijijini.
Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi Rais Tamisemi (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Santa Maria - Kabage yenye urefu wa kilomita 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tnganyika Mkoani Katavi.
“Nadhani Mlitusikia Mimi na Waziri wa Fedha kuwa ni jinsi gani fedha hizi za tozo ya mitandao ya simu na mafuta zinaenda kufungua barabara vijijini. Mmemsikia Mbunge wenu kuwa hii barabara haikuwa inapitika kutoka kijiji cha Santa Maria hadi Kijiji cha Kabage ambako ni muhimu kwa uzalishaji mkubwa wa chakula hasa maza ya mpunga, lakini sasa imefunguka, “alisema Ummy.
Alieleza kuwa Serikali iliamua kufanya ubunifu baada ya kujuliza ni jinsi gani wataboresha barabara za vijijini, hivyo kubuni chanzo hicho cha tozo za simu na mafuta ambacho sasa kinaleta matokeo chanya yanayoonekana.
“Mmemsikia meneja wa Tarura Tanganyika kwamba alikuwa na bajeti ya shilingi milioni 150 tu kwa wilaya nzima ya Tanganyika, lakini sasa kwa sababu ya tozo hii mpya,bajeti yake ya maendeleo ya ujenzi wa barabara inaenda kuongezeka mpaka shilingi bilioni moja na milioni mia tano (1.5 bilioni), “alisema Ummy.
Alisema kuwa kama milioni 150 zimeweza kujenga Km 16 za barabara ni wazi kwa bilioni 1.5 zitaenda kufungua barabara nyingi sana vijijini na kuondoa kero ya muda mrefu kwa wananchi.
Aliwataka watanzania kuendelea kuchangia tozo hiyo ambayo inaenda kuleta ukombozi mkubwa vijijini.
Chanzo: Clouds TV
kwa hiyo unapenda vya buree eeehh!!!Si kila anayehoji ni chadema. Ni muhimu haya maoni kwa ajili ya tafakuri.
Hizi tozo zikizidi ni sawa na kumkamua ng'ombe maziwa mengi hata kama ndama atadhoofika ili mradi unataka uuze upate pesa uwajengee kibanda kizuri.
Mama na ndama watadhoofika na maziwa hayatatosha na pesa haitazidi na kibanda hakitajengwa.