Ummy Mwalimu: Wachangiaji damu, kupewa kipaumbele wanapohitaji damu hospitalini. Watapewa kadi Maalum

Ummy Mwalimu: Wachangiaji damu, kupewa kipaumbele wanapohitaji damu hospitalini. Watapewa kadi Maalum

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Posts
11,966
Reaction score
11,218

Hivi huyu mtu anafahamu hata Medical Ethics?

Waziri wa afya jifunze ‘medical ethics’ under the concept of ‘non malificence’ you can’t do harm to a patience.

Hakuna priority kwenye afya who deserve the resources than another. It’s either first come first served or who needs it the most based on their poor medical condition.

Lakini hakuna sera ya kuchangia, upendelewe. Ni jukumu la wizara ya afya kukusanya damu na watu wana mbinu za kufanya hiyo shughuli.

Wanakupenda huko kwa sababu siyo mtaalamu unaeongea ujinga mtupu na aliekupa hayo mapendekezo ni mjinga vile vile.

=====

Na. WAF - Dar Es Salaam
WhatsApp Image 2022-02-25 at 4.11.17 PM (1).jpeg

Serikali kupitia wizara ya Afya imejipanga kutoa kadi za kieletroniki kwa wachangiaji damu wanaojitolea mara kwa mara angalau mara tatu kwa mwaka.

Hayo yamesemwa leo Februari 25, 2022 na Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa katika ziara ya kutembelea makao kuu ya mpango wa taifa wa damu salama jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amesema Kadi za kieletroniki zitaepusha usumbufu kwa wachangia damu endapo watahitaji huduma ya damu kwani kadi hizo zitaonesha jina la mchangiaji damu, kundi la damu yake na namba ya kadi, na mchangiaji huyu atapewa kipaumbele akiwa na mgonjwa hata yeye mwenyewe.

"Kila Mtanzania ana haki ya kupata damu lakini kwa wale ambao watakaokuwa na kadi watapewa kipaumbele cha kwanza". Amesema Waziri Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kutoa bure mifuko ya kukusanyia damu salama pamoja na vifaa vya ukusanyaji kwa Halmashauri zote nchini 184 ili kwenda kumaliza changamoto ya ukusanyaji ambayo imejitokeza nchini hivi sasa na kusababisha uhaba wa damu katika vituo vya kutolea huduma za afya.

"Nitoe wito kwa waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanapokea vifaa hivyo vya kuchangia damu na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kutatua changamoto ya upatikanaji damu kwa kuwa damu inahitajika sana na mama wajawazito, watoto, watu waliopata ajali pamoja na wanaofanyiwa upasuaji". Amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema vifo vingi vya kina mama wajawazito hutokana na ukosefu wa damu salama na hivyo kuitaka jamii iweze kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji huku akieleza kuhamasisha vikundi mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya uchangiaji.

Nae, Meneja mpango wa Taifa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo ameishukuru Serikali kwa hatua inayochukua juu ya upatikanaji damu salama kwa urahisi.

"Sasa kazi ni kwetu kuhakikisha damu salama inapatikana kwa kuungana na wananchi juu ya uchangiaji damu na naamini tukishirikiana tutaokoa vifo vingi". Amesema Dkt. Lyimo.
 
Ndio waziri wenu wa afya huyo; ata policies anazozinadi hadharani aelewi aziendani na kanuni za afya.

Sasa tatizo siyo yeye ni washauri vilaza kwanza na waziri asiejua lolote kama hiyo sera inakidhi matakwa ya medical ethics.
 
"Kila Mtanzania ana haki ya kupata damu lakini kwa wale ambao watakaokuwa na kadi watapewa kipaumbele cha kwanza". Amesema Waziri Ummy.
Mkuu Kilatha , hata baada ya maneno haya ya Waziri Ummy, kweli bado ulihitaji kuandika haya?.
Waziri wa afya jifunze ‘medical ethics’ under the concept of ‘non malificence’ you do ujinga mtupu na aliekupa hayo mapendekezo ni mjinga vile vile.
Duh....!. Hii freedom of expression...
haya...
P
 
Hatari sana
but na nyinyi mnamvizia akosee ili mumseme!!
wabongo noma sana......
Mimi niko wazi nikimsikiliza Dr Gwajima ustawi wa jamii hana huo uwezo wa kutosha anajua mambo kadhaa but knowledge yake ni limited (siwezi mlaumu kwa sababu hayo ni mambo ya western philosophy and they vary from nation to nation) based on various factors amongst them social values and budget.

However Dr Gwajima alibobea kwenye management ya afya and that is technical inataka uwe daktari na mwelewa wa public health for you to be able to trouble shoot issues.
 
It’s not about freedom expression it’s medical ethics under ‘non malifence’ you can’t have such a policy.

Unafahamu medical ethics, zingine zinasemaje?
It’s not about freedom of expression it’s about medical ethics under ‘non malifence’ you can’t have such a policy.

Unafahamu medical ethics, zingine zinasemaje?
Mkuu Kilatha, a.k.a Eric Cartman, kiukweli mimi sio tuu namkubali sana huyu bidada, bali... kwa wale ambao hawajawahi kufika Tanga, au kupita Tanga, nawaomba Tanga muendelee kuisikia hivi hivi tuu!...sii mchezo !.
P
 
It’s not about freedom expression it’s medical ethics under ‘non malifence’ you can’t have such a policy.

Unafahamu medical ethics, zingine zinasemaje?
Mkuu hii kitu ipo tena Hospitali binafsi ndio shida zaidi, ukiwa na mgonjwa anahitaji damu na hakuna ndugu wa kutosha anaweza kufa hivi hivi huku unaona. Iliwahi kunipa frustration sana
 
Ndio waziri wenu wa afya huyo; ata policies anazozinadi hadharani aelewi aziendani na kanuni za afya.

Sasa tatizo siyo yeye ni washauri vilaza kwanza na waziri asiejua lolote kama hiyo sera inakidhi matakwa ya medical ethics.
Na wewe unaboa sana, unashindwa kuweka h! Hiyo ata umeitaja hadi katika title neno ni hata!!!!!!!
 
Mkuu hii kitu ipo tena Hospitali binafsi ndio shida zaidi, ukiwa na mgonjwa anahitaji damu na hakuna ndugu wa kutosha anaweza kufa hivi hivi huku unaona
I can understand that, desperate time needs desperate measures.

However inventory control ni jukumu la afya kama waziri alivyosema damu aiuzwi madukani na nijukumu lao kuikusanya yupo sahihi 100%.

With that in mind you have historical records on the blood demand, so you have the duty to ensure there is always enough stock to meet the future needs based on records.

This is why people learn about inventory management in public health. Listen story ni ndefu mnatoa wataalamu tunalilia watu ovyo wanakuja solution za kijinga nje kabisa ya medical ethics.

Good Morning, 👋 nimesema ya kusema.
 
Sijaona kosa la waziri. Toka uchangie damu hili na wewe ukiitaji damu salama uipate kirahisi.
 
Sijaona kosa la waziri. Toka uchangie damu hili na wewe ukiitaji damu salama uipate kirahisi.
Like I said mtu aliesomea management ya afya he would know about inventory control ya damu na resources zingine so as not to run out.

Pili hoja ya waziri inaenda kinyume na medical ethics (non malificence) uwezi kutoa priority ya access to medical resources based on favouritism criteria including uchanguaji.
 
Kwa lipi based na kazi yake?
P
 
Like I said mtu aliesomea management ya afya he would no about inventory control ya damu.

Pili hoja ya waziri inaenda kinyume na medical ethics ‘non malifence’ ya kuwa priority
Tatizo unachanganya vitu. Waziri ni mwanasiasa na hapa anahamashisha uchangiaji wa Damu period. Mtaalam katika wizara ni Mganga Mkuu na kidogo Katibu Mkuu ingawa nayo ni managerial post (ambapo si lazima awe Mtaalam). Waziri yupo sahihi na hajapanga damu itatumikaje huko kwenye field. Medical ethics ni somo ujue!

Kama hujaelewa nieleze nikuelewishe zaidi ili uone Waziri yupo sahihi kwa nafasi yake kama mhamasishaji.
 
Back
Top Bottom