Ummy Mwalimu: Wagonjwa kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti moja ya sababu kuyumba kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
images.jpg

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema chanzo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuyumba ni pamoja na kuwepo kwa matumizi yasiyo na tija kwa wagonjwa ikiwemo kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti.

“Kwanini NHIF iko katika hatari? ni sisi wenyewe wananchi. Leo nimeenda Muhimbili hospitali, nimeenda kufanya kipimo cha X-ray na vipimo vingine nimeandikiwa na dawa, kesho naenda private [hospitali binafsi] nafanya kipimo, naandikiwa dawa, ugonjwa huo huo. Sasa hapo kwanini NHIF isife kama tunaenda kwa mtindo huu?” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi na wanachama wa NHIF akieleza kuwa pamoja na mfuko huo kukabiliwa na changamoto nyingi bado utaendelea kuwepo na kutoa huduma bora za afya.

Ameongeza kuwa, ili mfuko uweze kuendelea vizuri mambo kadhaa yanapaswa kufanyika ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama, kudhibiti matumizi yasiyo na tija na kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma za afya.
 
Hili huwa namwambia hata mke wangu,kila mara anaenda hospital anapima magonjwa yote na anakutwa nayo kila anapopima na akunywa dawa lakini akienda tena anayakuta ananunua dawa tena kuna muda huwa nahisi kwavile pesa sio zake anaona rahisi kupima magonjwa yote kila anapohis kuumwa

Njia nzuri unapojihis homa anza kupima maralia usipokuwa nayo ndo upime mengine,sio kila siku unakomaa na U.T.I wakati wewe ni mzembe wa kunywa maji.

Jamani magonjwa mengine inabidi tukubali kuishi nayo kama hayakusumbui kama kichocho,U.T.I,TYPHOID

Mara nyingine maabara nao wanatudanganya kwavile wewe ni lijinga la kupenda kujipima pima hovyo ndo unajikuta unameza midawa kila mara.

Copy nyingine ya comment hii nimeituma kwa mke wangu
 
Huduma zikiwa Bora kwenye Kila kituo, hakuna mwanachama atakayehamahama, pia hakuna mtu anayependa kunywa dawa! NB: Huduma na watoa huduma wakiwa makini Hilo halitojitokeza mama
 
View attachment 2342142

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema chanzo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuyumba ni pamoja na kuwepo kwa matumizi yasiyo na tija kwa wagonjwa ikiwemo kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti.

“Kwanini NHIF iko katika hatari? ni sisi wenyewe wananchi. Leo nimeenda Muhimbili hospitali, nimeenda kufanya kipimo cha X-ray na vipimo vingine nimeandikiwa na dawa, kesho naenda private [hospitali binafsi] nafanya kipimo, naandikiwa dawa, ugonjwa huo huo. Sasa hapo kwanini NHIF isife kama tunaenda kwa mtindo huu?” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi na wanachama wa NHIF akieleza kuwa pamoja na mfuko huo kukabiliwa na changamoto nyingi bado utaendelea kuwepo na kutoa huduma bora za afya.

Ameongeza kuwa, ili mfuko uweze kuendelea vizuri mambo kadhaa yanapaswa kufanyika ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama, kudhibiti matumizi yasiyo na tija na kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma za afya.
Ubabaishaji kwenye hospitali nyingi ndio kisa cha watu kupima kwingine tena. Hospitali zimekaa kibiashara sana. Unaweza kuambiwa una tatizo kumbe huna ili wakamue hela za bima. Wanakupa madawa kibao wala hayahitajiki ili wauze tu dawa kumbe wanakudhuru afya yako.
Kila ugonjwa unaandikiwa madawa kibao mradi mlipaji ni bima.
 
View attachment 2342142

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema chanzo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuyumba ni pamoja na kuwepo kwa matumizi yasiyo na tija kwa wagonjwa ikiwemo kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti.

“Kwanini NHIF iko katika hatari? ni sisi wenyewe wananchi. Leo nimeenda Muhimbili hospitali, nimeenda kufanya kipimo cha X-ray na vipimo vingine nimeandikiwa na dawa, kesho naenda private [hospitali binafsi] nafanya kipimo, naandikiwa dawa, ugonjwa huo huo. Sasa hapo kwanini NHIF isife kama tunaenda kwa mtindo huu?” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi na wanachama wa NHIF akieleza kuwa pamoja na mfuko huo kukabiliwa na changamoto nyingi bado utaendelea kuwepo na kutoa huduma bora za afya.

Ameongeza kuwa, ili mfuko uweze kuendelea vizuri mambo kadhaa yanapaswa kufanyika ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama, kudhibiti matumizi yasiyo na tija na kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma za afya.
Hizo ni sababu mfu,waziri tunajua hawezi sema UKWELI ulio nyuma ya pazia.Akiusema ukweli atakuwa si wazir tena.
 
Back
Top Bottom