#COVID19 Umoja wa Afrika (AU) waitengea Tanzania dozi milioni 17 za COVID-19

#COVID19 Umoja wa Afrika (AU) waitengea Tanzania dozi milioni 17 za COVID-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Umoja wa Afrika umeitengea Tanzania dozi milioni 17 za chanjo za UVIKO- 19 kupitia mpango wa Umoja huo wa kuzisaidia Nchi wanachama kupata chanjo kwa ajili ya Wananchi wake.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo Addis Ababa Nchini Ethiopia alipokutana kwa mazungumzo na Jumuiya ya Watanzania waishio Nchini Ethiopia (Diaspora) waliotaka kufahamu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na UVIKO -19 ikiwa ni pamoja na suala la chanjo.

Aidha Balozi Mulamula amewataka Watanzania wanaofanya kazi katika Mashirika na Taasisi mbalimbali za Kimataifa kusaidia upatikanaji dozi nyingine za chanjo ya UVIKO 19 ili kuwawezesha Watanzania wengi kupata chanjo hiyo kutokana na mwamko wa Watanzania kuongezeka mara baada ya kuzinduliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ethiopia Mhe Sahle – Work Zewde Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo Tanzania na Ethiopia zimekubalina kuendelea kutumia ndege za shirika la Ethiopia kutangaza vivutio na kusafirisha Watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja Tanzania.

Aidha Balozi Mulamula amemhakikishia Rais Sahle – Work Zewde kuwa Tanzania itaendelea kutekeleza maeneo yote ya ushirikiano ambayo Rais Zewde alikubaliana na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ziara ya Rais huyo Chato nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na suala la kuwarejesha Nchini Ethiopia wahamiaji wanaoshikiliwa katika magereza mbalimbali.

Kwa upande wake Rais wa Ethiopia Mhe. Sahle – Work Zewde amesisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Nchi hiyo hususani katika kutatua changamoto zinazozuia maendeleo miongoni mwa Mataifa hayo.
 
Huyu mulamula zaidi ya kuomba omba huko anakokwenda hana lingine lolote?
 
Daaah, watawachoma ng’ombe hizo chanjo.., pia tutumie ndege zetu na sio za Ethiopia
 
Serikali iendelee kutoa takwimu za Uviko kama nchi nyingine wafanyavyo...
 
Back
Top Bottom