GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Ingefaa kwamba Umoja wa Afrika (AU) ingekuwa kama baba kwa nchi za Afrika.
Uwepo wake ulipaswa kunufaisha raia wa nchi wanachama!
Pamoja na uwepo wa AU, bado nchi za Afrika zimeendelea kuwa kama watoto wasio na waangalizi.
1. Vita vya wenyewe kwa wenyewe, mfano ilivyotokea Rwanda na baadaye Congo na Somalia
2. Imeshindwa kukemea matafa makubwa yanayozinyanyasa wanachama wake. Mfano Zimbabwe ilivyowekewa vikwazo na nchi za Kimagharibi.
3. Imeshindwa kuepusha Mapinduzi ya kijeshi kwa kushawishi uwepo wa Serikali inayozingatia utawala bora
4. Imeshindwa kuifanya Afrika kuwa moja. Ona baadhi ya wanachama wake wanavyosigana, mfano DRC vs Rwanda
5. Bado inaburuzwa na mataifa makubwa. Hata mahakama ya The Heaque inasemekana ni kwa ajili ya Waafrika na si Wazungu
Kuna uhalali gani wa hayo kutokea ilhali AU ipo hai? Nitakosea nikisema AU haina msaada kwa Waafrika?
Au faida ya uwepo wake ni kwa ajili ya viongozi wa Afrika kukutana pamoja na kupiga picha?