Umoja wa Afrika wasema Nzige wa jangwani waweza kuwa janga kubwa Afrika

Umoja wa Afrika wasema Nzige wa jangwani waweza kuwa janga kubwa Afrika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Taarifa iliyotolewa kwenye mkutano ya kamati ya amani na usalama ya Umoja wa Afrika imeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu uvamizi wa nzige wa jangwani ulioanzia mwezi Juni mwaka jana na kuendelea kuziathiri nchi za Afrika Mashariki

Wameonya kuwa tatizo hilo huenda litakuwa janga la bara nzima kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa pia wameonya mapema kuwa kuzaliana kwa nzige wa jangwani kutaendelea katika Eneo la Pembe ya Afrika, na kusababisha ongezeko la idadi ya nzige katika nchi za eneo hilo na kuwa na makundi mapya ya nzige katika mwezi Machi na Aprili.
 
Hawa nzige hatuwezi kuwageuza kuwa kitoweo kweli ikawa mboga nzuri tu au ?hawaliki.
 
Huko Kenya nako wamevamiwa na makundi ya Nairobi flies {narrow bees}
 
Back
Top Bottom