Pre GE2025 Umoja wa Bodaboda na Bajaji: Hatutashiriki Maandamano ya CHADEMA

Pre GE2025 Umoja wa Bodaboda na Bajaji: Hatutashiriki Maandamano ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni lini Walishiriki?
Swali ni, kwani CHADEMA na raia wasio kubaliana na siasa za CCM waliwaendea hawa watu na kuomba washiriki hayo maandamano?
Je, wanachama wao wasiokubaliana na msimamo huo na wao watazuiwa kuandamana?

Ni nini hasa kilicho fanya hawa viongozi wajitokeze na kutangaza hivyo. Walitumwa na CCM?
 
Shirikisho la waendesha bodaboda na bajaji Nchi Tanzania leo Septemba 22, 2024 wametoa msimamo wa kutokushiriki maandamano ambayo yamepangwa kufanyika siku ya Septemba 23, 2024 Mkoani Dar Es Salaam yaliyotangazwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Msimamo huo umetolewa na Mwenyekiti wa Shirikisho la waendesha bodaboda na bajaji kwaniaba ya wanachama wote Nchini na kusema kuwa tunu ya amani ya Nchi ni kubwa kuliko kitu chochote hivyo hawawezi kuishi kwa wasiwasi endapo wataandamana hawataweza kuthamini mali zao.

Pia soma:
~ Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea
~ Kuelekea 2025 - Rais Samia: Pikipiki zako za CCM zimeongeza ufanisi wa kiutendaji, zilizobaki naomba wapewe wenyeviti wa kata

Pia Katibu wa Shirikisho hilo Michael Liganya amesema wakishiriki maandamano hayo watakuwa wametengeneza matatizo makubwa kwa sasa katika Nchi ya Tanzania bodaboda hawapo tayari kuwa miongoni mwa wavunjifu wa amani.

Aidha msemaji wa Shirikisho la waendesha bodaboda na bajaji Tito Lazaro amesema hakuna bodaboda atakae andamana siku ya Septemba 23 hivyo wataendelea na shughuli zao za kila siku zinazowawezesha kupata kipato na kuendesha maisha yao.

Sema samia aliona mbali kugawa zile boda
 
Swali ni, kwani CHADEMA na raia wasio kubaliana na siasa za CCM waliwaendea hawa watu na kuomba washiriki hayo maandamano?
Je, wanachama wao wasiokubaliana na msimamo huo na wao watazuiwa kuandamana?

Ni nini hasa kilicho fanya hawa viongozi wajitokeze na kutangaza hivyo. Walitumwa na CCM?
Nyie leo ndiyo mnawajali sana bodaboda

Ova
 
Tunamsubiri mtu mmoja tu Freeman Mbowe atupe amri kuanzia saa 5:30 jioni leo. Kwa taarifa yako maandamo yalishafanyika na hao hao polisi na keshi ni hitimisho tu.
ushirikina na Ramli ni vitu vya hovyo sana aise 🤣
 
Back
Top Bottom